afande kifimbo
JF-Expert Member
- Aug 31, 2015
- 6,254
- 2,678
WEKK SAID BRO, na mimi humu kwa kweli nakusanya maoni ya watu wanaotoa ili nifanya maamuzi yangu..maana kila mtu anasema kwa experience yake but utaona tu zilizotajwa tu zote zinafaa.....mengi tumeshakutajia mkuu. humu unganisha fikra ufanye maamuzi yako. ukiendekeza kila kitu uambiwe mwishowe utakosa la kufanya.
mimi nimekupa yangu kama mzoefu kimatumizi toka 2003 hadi sasa natumia pikipiki, sina gari, mara chache naendesha ya wadau lkn naukubali utamu wa pikipiki kuliko gari tofauti na kero za mvua.
pia mafundi na wauzaji wameshabwaga yao.
ukichambua kwa umakini utagundua washauri wengi wanapendekeza umiliki aina walizo nazo bila kuzingatia vigezo vyako ulivyoainisha ktk main post. hivyo kazi ni kwako.
NYONGEZA:
service ya maana ni ku-fix lolote kabla hakijaleta madhara, ukisubiri sana ukaendeleza kutembelea tatizo huzaa mengine.
mf. upepo mdogo hichana tairi na kuvinba/kutunishwa nyaya au kupasuka au kukata nali.
oil rojorojo (zaidi ya km 1000) huchakaza/ziba filters na kuzalisha moshi au kuunguza piston rings, plugs kuungua na kukosa nguvu.
jenga mazoea ya kuhudumiwa na fundi mmoja kwa service ya uhakika labda ukiwa mbali naye kwa dharula.
jenga hulka ya kutomwamini fundi. asikununulie spea nunua mwenyewe yeye awe mfungaji. aghalabu wanakula na wenye maduka. unatozwa bei ya spea halisi anakufungia bomu ya bei chee anajilia chenji na huku unamlipa kabhour charges, ukitembea km chache unarudi kwake.
jenga tabia ya kujifunza kutambua hitilafu kabla ya kupeleka kwa fundi. wapo wanaobadili spea. mf unaenda kubadili rings za piston unamuachia chombo, anafungua plates au plugs zako org. anamufungia mteja mwingine. hii ni tabia ya mafundi wengi hasa watz ndio waizi waizi toka tumeacha kunyonya.
usimpe ovyo mtu baki usafiri wako. wewe ndiye unayejua thamani na umuhimu wa hicho chombo. wapiga norinda kwenye lami, wacheuaji na upanguaji wa fujo mara nyingi. vyombo si vyao-wamekodi. fikiria kwanini iwe ngumu kumkabidhi mtu hata memsahibhu pochi yenye 1,500,000 akushikie ukienda msalani lkn iwe nyepesi kumpa ignition key mtu. aburuze boxer yako uliyotolea 2.3m eti aisikilize!!
thamini vyako hata kama utasemwa au wakiona ni cha bei chini. wangapi hawana? A MAN BRAGS HIS PENIS HOWEVER TINY (usitafsiri kwa kiswahili hii sio mada ya Piston)