robert sendabishaka
JF-Expert Member
- Dec 11, 2015
- 2,973
- 3,052
UIMARA/HADHI/BANA MATUMIZINilitaman mvuto pia ili kulinda status yng
kwa hadhi mkuu chukua Honda. zipo ndogo za cc 100, 125, 150 models mpya zilizoundiwa body kama pikipiki nyingi za mchina/india.
pia ni economical kwa mafuta kufikia 60-70 km/lt japo bei yake kiasi imechangamka. bei za kati ni 3-5m.
raha ya honda ni mkataba: hakuna uharibifu wa reja reja. unabaki na jukumu la oil exchange, filters, kusafisha air cleaner, chain adjustmen na petrol. sio rahisi kukutana na kukata shock up, cable, kuunguza clutch, kumaliza brake shoe, sprokets ndani ya mwaka.
wale yange yange pia sio wasumbufu upande wa hizi.
PUNDA/ROHO YA PAKA/RAFIKI WA OFF ROAD/MAFUNDI WENGI, VIPURI CHEE/HAPO KAZI TU
sanlg, sunlg, houjue(sina hakika speling), tan hero, kinglion, fekon
bei nafuu dukani kulinganisha na aina nyingine.
zina mtetemo (nyingi zina mfumo wa pushrods) hazifai kwa masafa, utachoka sana kiuno, mgongo, mikono hasa kwa wasio na uzoefu wa masafa.
kelele kubwa ya injini tofauti na tvs, boxer, honda
hizi kubebeshwa hadi kg 300 (kutegemeana na ujuzi/uzoefu wa dereva)
vipuri vipo kila kona na mafundi wengi wanazijulia. hata bila sevisi ya maana dude linatembea tu. wapo wanafunga hata kwa kamba likikata baadhi ya spea linakata milima tu.
haidumu muda mrefu sababu ya suluba zinazokutana nazo.
MASAFA/LIGI/CHOTARA
boxer (cc100, 125, 150 old na new)
*sina uhakika kama zipo za pushrods.
zinafaa sana kutembelea tu au kubeba mizigo isiyozidi 70kg (uzito wa abiria mmoja)
ni nyepesi sana, hazishiki barabara, ni rahisi kuhamishwa barabara maeneo yenye upepo. ##ilinitokea biharamulo 2016)
very and dangerous in terms of speed.
(ina mwendokasi usio wa kawaida japo dashboard ni kama inadanganya. inasoma 110 tu lkn wa magari mnatoana jasho)
inapenda kujaliwa sana (chotara) haitaki ubahiri kwenye spea na sio kila fundi anatengeneza kwa ubora. vipuri vyake ni aghali.
narudia tena; haipendi mizigo maana inapoteza spidi na huchakaa mapema
TVS hizi za kisasa sijawahi kutumia, sina uzoefu. waje wenyeji wake. ila nilimiliki na kutumia old model cc 100 na 110. sifa kama boxer. tofauti yake ni matumizi kidogo ya mafuta, starehe barabarani kwa shock ups zinazonesa kwa maringo lkn spea mmmh waweza kukimbia.
MWISHO.
uhai wa chombo huongezeka kulingana na matunzo na kujali kwa mtumiaji.