Naomba ushauri, nataka kununua pikipiki

Jay10

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
400
250
Habari za wakati huu wana JF, kama title inavyojieleza hapo juu;

A]
Nataka kununua pikipiki kwa ajili ya matumizi yangu binafsi na baadae kidogo kwa biashara. Hivyo naomba ushauri wa aina ya pikipiki itakayofaa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo;
1)mwonekano mzuri (mvuto)
2) injini kubwa (uwezo wa kuhimili milima -speed)
3)upatikanaji wa spear zake na bei nafuu
4)ubanifu wa mafuta (economical fuel consumption)
5)bei yake nafuu sana

KATI YA PIKIPIKI HIZI ( BOXER 150, TVS, HAOJUE /HONDA ACE, HERO, TANHERO)

NITOE USHAMBA TAFADHALI KTK HAYA
*Pia kati ya Boxer old model na New model ipo bora, na kwann?
*Boxer BM 150 na 125 ipi nzur/kubwa (injini)
*Je kuna boxer yenye gia 5 na ipi.?
* Hivi plate namba A inamaanisha chombo ni cha kitambo xana na uwezo/ubora wake ni mdogo ukilinganisha na namba B, C, na D,?
Mfano nikinunua chombo (gari au pikipiki kwa mtu Je ishu ya kubadilisha umiliki inakuaje?


#NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU KWAKO MWANA JF... %
 

kayimukaa

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
341
250
Chukua tvs ipo vizuri kuliko boxer hata ulaji wake wa mafuta ni mzuri lita kwa km 60 hadi 70 wakati boxer ni lita kwa km 30 hadi 40
 

Jay10

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
400
250
Chukua tvs ipo vizuri kuliko boxer hata ulaji wake wa mafuta ni mzuri lita kwa km 60 hadi 70 wakati boxer ni lita kwa km 30 hadi 40
Duuh kama ni hvyo kwel bas inaweza kuwa best kwenye mafuta...... Lakin napata wakati mgum napowaza Upatikanaji wa Spear parts zake mana inasemekana kutoka kwa watumiaji kuwa ni adim sana had Nairobi mana nipo Moshi... Wenye tvs kwa observation yang naona ni wachache kuliko wenye boxer na nyinginezo
 
Top Bottom