Naomba ushauri: Nataka kuhairisha masomo kwa kushindwa kukidhi gharama

Idrisa1510

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
252
350
Naombeni msaada wa mawazo. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wakwanza wa chuo kikuu Dodoma (UDOM). Nilichaguliwa chuoni hapa kusoma BACHELOR OF SCIENCE WITH EDUCATION bahati mbaya sikufanikiwa kupata mkopo wa kujikimu nakugharamikia masomo.

Mzazi ni masikini na alijichangachanga nikafanikiwa kulipa nusu ya Ada ya mwaka na direct costs nikawa nimeanza asomo.

Lakini mpaka kufikia sasa naona kabisa mzazi kashindwa kuendelea kunilipia gharama za kimaisha za kila siku zahapa chuoni kiasi cha kulosa alternative way Zaid ya kufikiria nirudi nyumban kusubilia mwaka ujao kwani nililenga na kutegemea Sana kusoma Kwa mkopo wa serikali.

MSAADA KWENU NAOHITAJI NI NJIA AU HATUA NAZOWEZA FUATA ILI NIAHIRISHE AU NIONDOLEWE KABISA MIONGONI MWA WANAFUNZ WA CHUO HIKI ILI NIPATE FURSA YA KUOMBA TENA MWAKANI. AU KAMA UNA LAKUNISHAURI JUU YA SWALA HILI ITAKUA VYEMA

Kwa Aliye na uziefu au anafahamu kunusiana na jambo hili anisaidie.
 
Hapo umesajiliwa tayari..kwaio kama unataka kaahirisha ni rahisi sana. Uone uongozi wa chuo
 
Nakushaur wakufute kabisa kweny system ya chuo chao ili mwakani uapply upya!! Nakwambia hv kwasababu ukiomba mkopo kama mwanafunzi aliyeahirisha mwaka inakuwa ngumu kidogo kupata kuliko ukiwa ni fresher student!!La pili Mikopo ya wanafunz walioahirisha mwaka majibu yao yanachelewa sana kutoka!!!
 
Ungekekuwa hujasajiliwa ungeondoka kimya kimya apo chuo, ila kwa vile umesajiliwa una postpone, unakuja kuendeleza mwakani ukipata pesa ila hio hio koz,

Ungekuwa unaweza nakushaur ukafutilie mbali usajil wako apoo chuo na tcu kabisa, usionekane kwenye data base yao kama ulishawahi kuchaguliwa then omba tena mwakan, nakuhakikishia hutakosa, rafiki zangu weng wamefanya ivo mwaka jana japo wanaume wazima walikuwa wanalia, mwaka huu na wamepata

Note :ukiomba mkopo wakat inaonesha we n mwanachuo (continues) hutakuja kukutana na huo mkopo, loan board nawajua sana
 
Naamini ukienda TCU wanaweza kukufutia usajili wako kwenye data base zao na hiyo ni baada ya kumalizana na chuo..Yaani unawaomba chuo wakufutie usajili then unaenda TCU

Faida ya kufanya hivi ni kuwa utaomba next year ukiwa ni kama fresher..lakini still bado sio guarantee kuwa utapata mkopo..kuomba mkopo kama continuing student,bodi kama wanawaweka nyuma sana..
 
Fanya kama ulivoshauriwa na wadau hapo juu, jitahidi tcu wakuondoe kwenye database zao, uombe mwakani kozi uitakayo, ualimu huenda haikuwa wito wako na kwa mjibu wa thread yako nyingne inaonesha ulifaulu vyema, just relax! utasoma kile roho inataka.
 
Lakini mpaka kufikia sasa naona kabisa mzazi kashindwa kuendelea kunilipia gharama za kimaisha za kila siku zahapa chuoni kiasi cha kulosa alternative way Zaid ya kufikiria nirudi nyumban kusubilia mwaka ujao kwani nililenga na kutegemea Sana kusoma Kwa mkopo wa serikali.
Kwanza nikupe pole, haya madhira yanawakuta wengi ingawapo huwa nawasikia wakubwa wakisema mwenye shida hatakosa mkopo lakini huu ni mfano hai. Nini cha kufanya? Kama uli-appeal ni vizuri zaidi, omba kuahirisha masomo kwa mwaka mmoja, halafu chuo kikukubalia andika barua tatu. Ya kwanza iende HESLB ukiwaeleza kuwa una ahirisha masomo kwa kushindwa gharama zake na ulikosa mkopo na hata hivyo kuendelea na masomo mwakani itategemea kama utapata mkopo. Ililie bodi ikusaidie.Ya pili peleka TCU kuwaeleza yaliyo kusibu na wajue umeahirisha masomo ili rekodi zao ziwe sawa. Barua ya tatu peleka wizara ya elimu kwa Mama Ndalichako na kwa unyenyekevu kabisa mueleze hali halisi na kwamba imebidi kuahirisha masomo kwa mwaka mmoja lakini hata hivyo huna uhakika wa kurudi kwani bila mkopo gharama zitakushinda na omba msada wake ikiwezekana aingilie kati. Hata hivyo wasiliana na wakina Abdul Nondo huenda wakaweza kukusaidia kwa njia wajuazo wao (ni memba hapa JF unaweza kuingia PM yake). Nikupe pole tena na wote wenye hali kama yako.
 
Shukran sana
 
Mimi nilichaguliwa vyuo viwili na nikaconfrim kimoja. Lakini kulingana na hali ya uchumi hata kusajil sijasajili. Mim napaswa kufanya nin wapendwa?
 
Back
Top Bottom