Naomba ushauri, nashindwa kubajeti fedha yangu

huku kwetu

Senior Member
Sep 7, 2016
145
194
Habarini wakuu,

Samahani mimi ni mwajiriwa wa serikalini ivi karibuni, shida yangu jmn siwezi kabisa kubajeti hela. Sawa mwanzoni mwa mwezi nanunua kila kitu.

Ambacho nakuwa sina labda mboga mboga hizi. Na nikasema labda nitumiage 10 per wiki kutokana na mazingira ya kijijini. Sasa yani nikichenji hiyo kumi ndani ya siku mbili au tatu sina hela.

Na hivi NMB wakala ni hapo nje naenda natoa. Siku mbili sina kitu. Sisaidieni nifanyeje niweze kuhimili maisha ukizingatia ndo naanza kazi na kamshahaea kenyewe la laki 4 na
 
Daah hongera kwanza kwa kupata ajira maana ni changamoto

Pili rafiki angu ‘What your goal to this life’ yaan Plan au mipango? Mimi naamini mtu mwenye mipango haez ishiwa to that extent.
 
Google kitu kinachoitwa Personal Budget Format zitakuja za kila aina utachagua inayoendana na Money Spending yako Daily, Monthly, Weekly or Yearly. Good luck pal and God watch over you.
 
Kupanga ni kuchagua, chagua unavyotaka kununua ambavyo ni vya lazima, andaa bajeti yake na ukanunue vya kukutosha muda unaotaka wewe na uache kununua vitu vya muhimu ila siyo vya lazima kwa jinsi wewe mwenyewe utakavyoona
 
Daah hongera kwanza kwa kupata ajira maana ni changamoto

Pili rafiki angu ‘What your goal to this life’ yaan Plan au mipango? Mimi naamini mtu mwenye mipango haez ishiwa to that extent.
Asante kwa pongezi, pili sijui nina pepo gan hata niweke tustrategy utakuta ela matumia tu.
 
Google kitu kinachoitwa Personal Budget Format zitakuja za kila aina utachagua inayoendana na Daily Money Spending yako Monthly, Weekly or Yearly. Good luck pal and God watch over you.
Nashukuru kwa kunipa aida hiyo mpendwa
 
kupanga ni kuchagua, chagua unavyotaka kununua ambavyo ni vya lazima, andaa bajeti yake na ukanunue vya kukutosha muda unaotaka wewe na uache kununua vitu vya muhimu ila siyo vya lazima kwa jinsi wewe mwenyewe utakavyoona
Asante ntafuata ushauri
 
Huo ni ugonjwa wa wengi. Desire ndiyo inayotumaliza. Njia nzuri na nyepesi ni jitengenezee madeni ya lazima ili baadae hayo madeni yaje kukufaidisha.

Madeni ninayozungumzia hapa ni pamoja na ule mchezo wa kupeana hela anatoka mtu, ule mchezo ni wa kijinga lakin unasaidia sana
 
Acha kula vitu vya bei kubwa hasa breakfast jibane kidogo.

Home re-budget yaani panga upya hakikisha mnakula kwa nusu ya bajeti ya sasa,

Punguza misaada, punguza kutembelea ndugu.

Usikopeshe / usihonge mtu mshahara.
 
Basi funga icecream uuzie kwako au fuga kuku uuze mayai utapata alternative income kama utaweza lakini.
Nilipo nimepanga kwa hizo biashara haiwezekan icecream umeme tupo wapangaji wawili, kuku hamna sehemu ya kufugia
 
Acha kula vitu vya bei kubwa hasa breakfast jibane kidogo.

Home re-budget yaani panga upya hakikisha mnakula kwa nusu ya bajeti ya sasa,

Punguza misaada, punguza kutembelea ndugu.

Usikopeshe / usihonge mtu mshahara.
Nashukuru kwa ushauri
 
Habarini wakuu,

Samahani mimi ni mwajiriwa wa serikalini ivi karibuni, shida yangu jmn siwezi kabisa kubajeti hela. Sawa mwanzoni mwa mwezi nanunua kila kitu.

Ambacho nakuwa sina labda mboga mboga hizi. Na nikasema labda nitumiage 10 per wiki kutokana na mazingira ya kijijini. Sasa yani nikichenji hiyo kumi ndani ya siku mbili au tatu sina hela.

Na hivi NMB wakala ni hapo nje naenda natoa. Siku mbili sina kitu. Sisaidieni nifanyeje niweze kuhimili maisha ukizingatia ndo naanza kazi na kamshahaea kenyewe la laki 4 na
Hizo hela zinazokushinda kubajeti ni kiasi gani??
 
Back
Top Bottom