Naomba ushauri napata maumivu makali ya kiuno hasa Alfajiri

kjembe

Member
Jan 9, 2015
45
29
Mimi ni mwanaume 29 (nimeoa), kwa sasa nipo Dar, miezi mitatu Iliyopita nilianza kujisikia vibaya hasa kupata maumivu ya kiuno na viungo vyote vya mwili, niliamua kwenda hospital moja hapa Dar baada ya kuchek nikaambiwa nina vidonda vya tumbo(H-Pylori) na nikaandikiwa dawa aina ya Omeprazole na flagly baadaye ndiyo maumivu yalizidi, basi nikarudi tena nikapewa H Pylori Kit mbili nikazitumia lakini bado nikawa napata maumivu ya tumbo na kiuno kiasi hata kuamka najishauri hasa alfajiri.

Baadaye nikajikuta nimechanganya dawa za asili na za dukani lakini wapi, nikakata tamaa. Baada ya wiki mbili mbele niliamua kwenda Kanisani kwa ajili ya maombi na baadaye nikarudi nikaendelea kutumia Omeprazole baada ya daktari kunishauri hivyo. Baada ya miezi miwili nilipima na kuambiwa H-Pyroli ni Negative.

Sikuamini nikakaa tena wiki mbili nimepima nikapima tena nikakuta ni Neg. Cha kushangaza napata maumivu makali sana ya kiuno na juzi nimepima nikaambiwa nina U.T.I 80 basi nikaamua kuchoma sindano za Powerseff mbili na kumeza dawa za AZUMA ambazo nimemaliza jana usiku ingawa bado maumivu ya kiuno yananitesa.

Hospitali wanasema niendelee kunywa panadol /Tramadol lakini najiuliza sana hili tatizo ni nini?

Msaada wenu wataalamu, hapa nilipo nina maumivu ya kiuno hatari hata weekend naiona haifai.

Nawasilisha.
 
Shida ni kuwa unavokunywa anti pain unachokoza tena vidonda vya tumbo, course kupima nankukuta h pyroli negative sio mwisho wa vidonda vya tumbo.

Tiba inayokufaa nii..

1. Think about your body weight, fanya mazoezi unaweza ukaanza na kukimbia kimbia kidogo.

2. Kanunue CHIA SEEDS utumie.

3. Fanya sex, at least mala 2 kwa wiki.

5. Hakikisha huna stress.
 
Boss mazoezi mimi nina mwili wa kawaida sana na uzito wangu ni 58 so wakati mwingine nawaza au kwa kuwa mara kadhaa natumia pikipiki kama usafiri wangu na kufanyia kazi zangu za hapa na pale?? Na hizi Chia seeds naweza pata wapi kwa gharama ipi?

Supermarket

Back
Top Bottom