Naomba ushauri namna ya kumshauri

lindunduru

JF-Expert Member
Aug 2, 2015
392
551
Nina mdogo wangu kaishi na mke wake kwa miaka kama mitano na mpaka mwezi march mwaka huu walikiwa pamoja.mola kawajalia mtoto mmoja.

Huyu shemeji yangu alimuaga dogo kuwa anaenda kusalimia kwao nq kuwasaidia kuvuna Mpunga.

Mwezi mmoja baadaye alimtumia taarifa dogo kuwa hana mpango wa kurudi tena kwake kwa sababu ameichoka ndoa,na kwamba anataka kuishi ki bachela.

Pamoja kuwa huko aliolewa na mwanaume mwingine akiwa mke wa pili anamuomba dogo kuwa anataka kurudi tena kwenye ndoa.
Nimshauri vipi?
 
Huyo anataka kurudi kwenye kabuli lake?hao ndio watu wanakutwa wameuawa tu
 
Arudi kufanya nini? Au kasahau nguo zake?

Huyo mwanamke angekua mstaarabu angebaki hukohuko!!
 
Hivi hata wewe umeshindwa kufanya uamuzi??? Umeoa mtu then kakuacha kaenda kuolewa tena yakamshinda karudi.

So akirudi siku ingine akipata kwingine akukimbie???

Mwambie kile alichokikimbia mwamzo kipo vile vile akijabadilika.

Mwambie dogo atafute mwingine. Hapo hata maandiko yanaruhusu
 
Mshaurii dogoo naee aletee yulee demuu akee ajee kuishi apoo..!! Afuu huyo mke wake hata asimjibu kitu...zaidi ya kumwambia Aendelee na maisha yakee
 
Alichokuwa anakitaka ndio hiko ameshakipata asiyefunzwa na mamaye ulimwengu humfunza ila inaonekana bado mdogo wako anampenda mkewe mwambie afanye vile moyo wake unataka
 
Hv ni kwamba Vijana siku hizi wanaoa bila kujuwa wajibu wao ama ni uwezo wao wa kufanya maamuzi ndo mdogo? Mana bado siamini kama Kijana alie ishi kwenye ndoa miaka 5 anaweza omba ushauri kama huu!!!
 
Ndio shida hiyo ya kufanya maamuzi pasi kuangalia pande zote za shilingi.

Amuache tu azidi kuona utamu wa kuwa na mke mwenza. Sababu ndio alichokuwa anakitaka hicho.
Avune alichopanda, lakini wakati mwingine maamuzi ya kimapenzi hua hayashirikishi akili bali ni moyo tu! Kwa akili ya kawaida tu(common sense) maamuzi ya hilo jambo wala hakupaswa kujiuliza na kutaka ushauri kwa watu wengine eti mtu aliyekusaliti kiasi hicho arudi a asirudi! Usishangae akapewa ushauri huyo mke asirudi lakini mume kimyakimya akamrudia!
 
Hivi huyo dogo bado anamuhesabu mkewe? wakati kishaolewa na jamaa mwengine. Hii ishu sidhani ya kuhitaji ushauri bali inahitaji uamuzi wa kumwambia huyo mdada tu. Halafu unasikia wanawake wapo kwenye madarasa ya makungwi sijui wanasomeshwa nini huko kwa makungwi.:D
 
Avune alichopanda, lakini wakati mwingine maamuzi ya kimapenzi hua hayashirikishi akili bali ni moyo tu! Kwa akili ya kawaida tu(common sense) maamuzi ya hilo jambo wala hakupaswa kujiuliza na kutaka ushauri kwa watu wengine eti mtu aliyekusaliti kiasi hicho arudi a asirudi! Usishangae akapewa ushauri huyo mke asirudi lakini mume kimyakimya akamrudia!
Kweli kabisa mapenzi kitu kingine bana.
 
Kijana hayo mambo waache waamue menyewe. Yeye ndo anajua anamuhitaji tena ama laaah. Halafu usikute mdogo wako alimfanyia shem vitimbi hadi akachoka ndo akaondoka sasa kama wote wanaamua kujirekebisha waache.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom