Naomba ushauri: Nahisi kuibiwa na wahudumu wa Halotel

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
3,880
4,508
Bila shaka mnaendelea na maandalizi ya sikukuu!Mida ya saa nne leo asubuhi kuna mtu kaniomba vocha nikaona isiwe kesi nikaingia kwenye Mobile App yangu ya NMB ili nimnununue mda wa maongezi mhusika.

Nimeingia nikamtumia elfu 10 kama mda wa maongezi ili ajiunge mwenyewe,Nmb wakanipa taarifa hela imetoka,mhusika kasema hela imeingia kwake.

Tatzo kila alipojaribu kujiunga anaambiwa salio halitoshi,ikabidi niwapigie wahudumu,mwanzo wakanambia hela ishaingia kwenye hyo namba kiasi cha elfu 10,nikakata simu nikamuuliza mhusika akasema bado anaambiwa salio halitoshi.Nikasema labda mtandao ngoja nisubir.

Baada ya nusu saa tena nawapigia simu wahudumu (hapa ndo wamenichosha)wananiambia hyo pesa haionekani baada ya kukorokochoa mitambo yake akasema hyo pesa ishafika kwa mhusika na imekatwa 550 salio lake la kawaida ni 9450 akaendelea kusema huyo mtu alikopa mia tano so kakatwa na riba sh 50.

Nikarudi kwa mhusika akasema hata hyo 9450 haipo,na jana tu kaweka vocha hakukatwa maana hajawahi kukopa.

Hapa nashindwa nifanyeje kupata pesa yangu maana kuna dalili ya wahudumu wa halotel kuitumia kesho kwenye sikukuu.

Wanamaliza kwa kusema WASILIANA NA HALOTEL KWA NO 100 TU KUEPUKA MATAPELI (wakati wao ndo matapeli wakubwa).

UPDATES:Nimewasiliana na watu wa TCRA wamenisaidia pakubwa sana na hela imerudi.Mama wa TCRA uliyenihudumia leo nakutabiria kufika mbali sana (very humble woman).
 
Duh! Hapo kweli Kuna dalili ya kupigwa.labda uende na huyo jamaa Yako kwenye ofisi zao,ili wakazibitishe deni lake.
 
Siku hizi hakuna wakumuamini, ukienda kununua dawa dukani wanakupiga cha juu, bia wahudumu hawarudishi chenchi, konda ukisahau chenchi harudishi..
 
Mkuu nilinunua umeme tangu mwezi wa 10 hadi leo sjawahi kupata token na hela walibeba
 
Mkuu nilinunua umeme tangu mwezi wa 10 hadi leo sjawahi kupata token na hela walibeba
Mi siibiwi kifala.Ningefika nao mbali sana hawa,Nawasikilizia tu siku wajichanganye tena.Nishaandaa timu ya mawakili kwa ajili yao.
 
Back
Top Bottom