Naomba ushauri mtoto wangu wa miaka 10 analia lia sana

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Wana bodi salaam,

Naombeni ushaur wenu hapa. Mtoto wang mdogo mwenye umri wa miezi 10 amekuwa na tabia ya kulia sana sana,asipo muona mama yake tuu ni kilio. Nilidhani pengine ana umwa nikampeleka hospitali kumpima malaria lakini imeonekana hana. Tabia hii ya kulia lia imeamza siku za karibuni pia akila chakula anatapika.

Ushauri wenu tafadhali
 
Suala la kulia ni utoto na kudekezwa sana. Akikua ataacha nashauri mtafutieni michezo ya kumuweka busy kidogo atasahau mama kwa muda.

Kuhusu kutapika watoto wana mtindo wa kujitapisha muda mwingine au inawezekana anatapika kwa sababu analia kipindi mnamlisha. Hapa inabidi mmkanye kidogo kwa kiaina.
 
1. Mama amefanikiwa kujenga ukaribu na mtoto kiasi cha kuwa mtoto haamini usalama wake bila uwepo wa mama yake. Anza kujenga mapenzi yenye uaminifu na mtoto, akuzoee na kuamini kuwa yuko salama akiwa na wewe.

2. Mtoto anapata choo kama kawaida? Mpeleke hospitali kwa uchunguzi zaidi.
 
Back
Top Bottom