Naomba ushauri: Mpenzi wangu haelewani na ndugu zake. Nimsaidiaje?

Jul 5, 2015
8
9
Kunae demu nimejuana naye kwa miezi 6 sasa, kiufupi ni Mwanamke wangu na mahusiano yetu yanaenda poa kabisa.

Yeye ni mtu wa Arusha but anaishi Dar kwa ndugu zake, Majuzi kati kulitokea kutokuelewana yeye na ndugu zake hali inayomfanya asiishi kwa amani.

Binafsi sitaki kuingilia ugomvi wao lakini demu anataka kuhama na msaada pekee alionao sasa hivi huku Dar ni mimi.

Nahofia kumpangia nyumba ya kuishi huenda nikaonekana kama chanzo cha ugomvi wake na ndugu zake, but honestly nakapenda haka kabinti na nikazuri mashaallah.

Ushauri wako tafadhali.
 
Kunae demu nimejuana naye kwa miezi 6 sasa, kiufupi ni Mwanamke wangu na mahusiano yetu yanaenda poa kabisa.Yeye ni mtu wa Arusha but anaishi Dar kwa ndugu zake, Majuzi kati kulitokea kutokuelewana yeye na ndugu
Acha ubahili wewe! Kwahiyo wapenda aendelee kunyanyaswa na ndugu zake?
 
Ukishamhamisha kwao akipata bwana mwingine?...au ukimchoka na kumuacha utaendelea kulipa Kodi na kumtunza?
 
Unajua ugomvi wao? Usiingilie mambo ya familia?
 
Kikubwa wewe nenda kajitambulishe kwao. Ili hata wakikupa nafasi basi utaelezwa yote either na ndugu au huyo demu wako yupoje. Kazi kwako
 
Kama kweli unapenda, naamini tayari utakuwa umemuuliza chanzo cha ugomvi wao. Yawezekana akakupa na uongo humohumo kaongezea chumvi ili umhifadhi, lakini Usimtoroshe kwa ndugu zake, Bali mfundishe/mwelekeze kuwatii na kumaliza migogoro wao.
 
Kwanza linapokuja swala la msingi na la maamuZi uzuri wa mwanamke usituwekee kwenye post kabisaaa sababu uzuri wake utakusaidia mwenyewe kitandani na wazuri wapo wengi tuambie unampenda tutakuelewa ila sio ni mzuri as if wanawake wazuri ni wachache.

Pili,una uhakika amegombana na ndugu zake kwa ushahidi maana isigekuwa anatafuta gear ya kuanza maisha yake ila kaja na sababu hizo.

Swala la kumpangia mwanamke nyumba ni sawa as long as gharama yake haitakuathiri kwa chochote kumbuka huyo sio mke wako ni mpenzi hivyo gharama yeyote utakayotumia kwa mpenzi inabidi ujiridhishe kwamba hata ikitokea leo hii tumeshindwa sitadai wala kunung’unika kwa lolote lile na sio unampangia nyumba,umejaza furniture,umenunua simu ya macho 3 hlf unagombana nae unataka kuleta canter isafishe nyumba mixer kupora simu.
Tumia gharama ambayo hata ikipotea leo hautaanza kumlaani mtu “sijui nilimpa kila kitu ni kwa upuuzi wako mwenyewe”

Kuweka kinyumba ila ndo BIG NO
 
Back
Top Bottom