Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Mwitore

JF-Expert Member
Feb 9, 2021
399
2,065
Ushauri wenu ni muhimu sana.

Umri wangu ni miaka 50, nimeoa mke kanisani huu ni mwaka wa 25 naishi naye na tumejaliwa watoto wanne, wa kwanza na wapili wamemaliza tayari chuo kikuu na wa tatu yupo chuo kikuu mwaka wa pili. Wa nne kamaliza kidato cha 4 mwaka jana, katikati hapo miaka 18 iliyopita bahati mbaya nikajiingiza kwenye mahusiano na binti wa miaka 20 wakati huo na akapata ujauzito, nilipomwambia nimeoa ili aitoe mimba ile na kwa kuwa bado ni binti mdogo anaweza kupata wa kumwoa, alikataa katakata. Na mimi kwa kuogopa maana alinitamkia kuwa atajiua kama nitamlazimisha kutoa mimba na kuwa yupo tayari kuishi na mimi kama mke wa pili na ujauzito ule hawezi kutoa kamwe.

Niliendelea kumshawishi atoe, matokeo yake akakimbia akaenda kwao mpaka akajifungua huko.

Lakini kiufupi zaidi, alirudi tena na kunitafuta na kunitishia kumwambia mke wangu, hivi ninavyoandika ilibidi nirudishe nyuma majeshi na kuanza kuishi naye kama mke wa pili.

Nilimpangishia chumba na maisha yakaendelea, baada ya muda alipata mtoto wa pili, wote ni wa kike, baada ya muda nilianza kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka sasa hivi wa kwanza anafanya mtihani wa form Six mwaka huu na wa pili anafanya wa form 4 mwaka huu na wote wamesoma shule za Private toka chekechea mpaka sasa hivi na kwa wastani kila mmoja alikuwa ananigharibu 2.5m hasa shule za msingi mpaka secondary. Hapo bado michango mbalimbali na usafiri, kwa maana walikuwa wanasoma mikoani.

Baada ya kumpata mtoto wa kwanza akiwa kwenye chumba cha kupanga, niliona sina budi watoto wangu na mimi binafsi niwe na uhuru maana maisha ndio yalishaanza hivyo, na mimi upendo tayari ulishaingia na kuona ni maisha kama maisha mengine.

Ndipo nilipoamua kununua viwanja, kama unakumbuka miaka ile ya 2000 nadhani kuanzia 2006 serikali ilipima viwanja 20,000 maeneo mbalimbali ya DSM, mimi nilichukua viwanja viwili, wakati ule nakumbuka kimoja nilinua 1,800,000 na kingine 1,300,000 ml. Ukubwa ni sq m 1200 na 1000. Kimoja kikubwa nikamjengea nyumba ya mgongo wa tembo, vyumba 2 na sebule katikati na choo kizuri cha nje, nikaacha eneo kubwa tu kwa ajili ya kujipanga na kujenga nyumba kubwa baadaye, kumbuka huo ni mwaka 2007 alipohamia hapo au tulipohamia hapo.

Baadaye nimfungulia biashara ya saloon, akafanya kama miaka 2 vibaka wakaingia nakuiba kila kiatu, nikaona isiwe shida nikamfungulia mghahawa ambao ulikuwa na vitu 16 na meza nne kubwa, bado na wenyewe haukufanya kazi vizuri, nikamfungulia grocery ya bia na kuweka kila aina ya kinywaji kwa kutumia viti na meza za mghahawa.

Nayo haikufanya kazi vizuri, nikamnunulia Hiace iliyotumika tayari kama dala dala.

Na yenyewe usimamizi ukawa mgumu.

DA NITAENDELEA, MAANA DA SIPO VIZURI KABISA KIAKILI NI NIMECHANGANYIKIWA SASA HIVI.

MUENDELEZO WA TUKIO HILI SOMA HAPA CHINI:
SEHEMU YA 2

SEHEMU YA 3

SEHEMU YA 4

SEHEMU YA 5

SEHEMU YA 6

SEHEMU YA 7

SEHEMU YA 8

SEHEMU YA 9

SEHEMU YA 10

SEHEMU YA 11

SEHEMU YA 12

SEHEMU YA 13

SEHEMU YA 14

SEHEMU YA 15

SEHEMU YA 16

SEHEMU YA 17

SEHEMU YA 18

SEHEMU YA 19

SEHEMU YA 20

SEHEMU YA 21
 
Naona watoto wako wanakaribia kuoana

Au mke mdogo atakuwa amekudhulumu kila kitu.

Au labda mke mkubwa kashajua kila kitu.

Sasa unawaza hii aibu utaiweka wapi.

Lkn nakuhakikishia usijali, options zote hizo hapo juu zina solutions hivyo hamna haja ya kupagawa.

Cha msingi malizia stori tukupe ushauri tuu.
Unforgetable
 
Mkubwa mi5 tena inakupelekesha?

Ila wanaume kweli vichwa vya chini vinapelekesha kichwa ya juu, hapa kifuatacho, mke kajua katishia kubwaga manyanga, na kumpeleka mufilisi, binti naye anasema jamaa ni mzee hamtaki anataka serengeti walisongeshe..vile viwanja mali yake na watoto wake!

Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
NAENDELEA,

Kumbuka hapo tayari tumeshaamia kwenye nyumba yetu (YETU) na baada kama ya miezi sita niliingiza umeme ambao ulinigharimu kama 400000 wakati huo (nguzo 2).

Hapo watoto wamemaliza chekechea na wamiingia primary tayari.

Baada ya kuona biashara zake zote hazieleweki niliamua kumjengea banda la kuku hapo hapo nyumbani la kuingia kuku mpaka 1500 hawa wa kisasa, kidogo hii pamoja na ugumu wake lakini ilidumu si chini ya miaka 4.

Hapo mwanzo kabisa nilimpeleka chuo cha ushonaji kabla hajashika ujauzito kusomea kudarizi, kwa hiyo wakati anaangalia kuku huku anaendlea na ushonaji ingawa ilikuwa hailipi sana na hata kuku zenyewe pesa ilikuwa haionekani zaidi ya kujizungisha yenyewe,

Ila nisisahau kipindi chote hicho pesa yake ya matumizi ya nyumbani nilikuwa kwanza nikimpa sh 150,000 kila baada ya wiki mbili, watoto wawepo au wawe boarding , kwa hiyo muda mwingi alikuwa yupo mwenyewe na wakati mwingine nikiwepo na mimi.

Ila niseme ukweli sikuwahi kujua kama kweli alikuwa anapata faida au vipi maana sikuwahi kuona kama kuna kitu cha maana kimenunuliwa zaidi ya vitu Vidogo vidogo vya hapa na pale.

Baada ya muda kidogo nadhani ni mwaka 2010 nikabahatika kupata safari ya kikazi nje ya nchi ambapo nilikaa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, lakini nikirudi likizo kila baada ya miezi 3, kazi yenyewe kidogo ilikuwa na stress kwa hiyo kulikuwa na sharti la kurudi kuona familia kila baada ya muda huo.

Ooops, ngoja nipumzike kidogo.

Daah maana sijielewi.
 
Mkuu haya majanga yametupata wengi.
Tuko kimya tu!
:rolleyes::rolleyes:
Yaani wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika, kwanza hapo huenda hata hao watoto wa bi mdogo siyo wake, 😂 😂 😂 🤔 namuwazia tu mwanaume mwenzangu!
Asichanganyikiwe kawaida SANA!
Wanaume kusaidiana!

Nitangulize tu POLE.

Everyday is Saturday................................:cool:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom