Naomba Ushauri-mavazi

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Nimekuwa nikiangalia sana mitindo ya mavazi hasa ya kina dada na kina mama. Mitindo ya nywele, mavazi, viatu, mapambo (acessories) na kadhalika.
Pia nimekuwa nikisikiliza maoni na sababu zao za kuwa na machaguo yao mbalimbali.
Pia kuna mawazo na maoni ya kina kaka na kina baba kuhusu huu mwenendo.
Kwa sasa nimejikuta nimechanganyakiwa.
hivi tunavaa nguo za kubana, kutuacha uchi au kujifunika mwili mzima kwa ajili yao?
Hivi tunavaa kwa ajili ya fasheni? ili tuonekane vizuri na wasichana wenzetu?
Au tunavaa ili tujisikie vizuri wenyewe?
Manake kuna manywele ya kubandika, vipodozi vya kila aina, nguo za kila aina. Je alie muhimu kuona kama nimependeza ni nani?
Kuna wakatu navaa nguo very uncomfortable, mfano kuzuia baridi, tunaenda pati na migongo wazi, tunatembea na viatu virefu. nguo inabana mpaka inaacha alama nk nk
 
Haika,

There are so many reasons these days za kuva nguo ... what people dont know ni kwamba Nguo in someway potrays how one wants to be perceived by the public .. it has its own language that people can read easily ... basing on maybe status ya mtu au position ... some wanafollow mkumbo ... kama yu belong to some age group or society others wanavaa depending on the occassion maybe anaenda party n.k. ..some have special errands za kuattract someones attention ..

I think the best here ni kujiheshimu ... ujikaguwe mwenyewe nafsi yako iridhike kwamba .. niko comfortable na sijajidhalilisha na hata nikikutana na mzazi au mtu mzima sitofedheheka ... halafu you can consult anyother person.

Unajua Haika ... tunakuwa mbali na diini zetu ndiyo maana aibu inatutoka .. navyofahamu ni kwamba hakuna diini inayotangaza mtu kutembea uchi .. unamkuta mtu kavaa hivi visuruari ambavyo, ukiinama vinakuwacha chupi nje ... worst still wengine wanapanda dala dala ... nyuma hajui kakaa nani akifika kituoni akiinama ... yaani unatamani umvamie maana mpaka makalio yote yanakuwa nje kwa kweli wanatutia aibu saaaana ... ama ni kuiga sijui .. au ushauri mbovu maana kuna watu wanakusifia huku pembeni wanakungonga
 
Nimekuwa nikiangalia sana mitindo ya mavazi hasa ya kina dada na kina mama. Mitindo ya nywele, mavazi, viatu, mapambo (acessories) na kadhalika.
Pia nimekuwa nikisikiliza maoni na sababu zao za kuwa na machaguo yao mbalimbali.
Pia kuna mawazo na maoni ya kina kaka na kina baba kuhusu huu mwenendo.
Kwa sasa nimejikuta nimechanganyakiwa.
hivi tunavaa nguo za kubana, kutuacha uchi au kujifunika mwili mzima kwa ajili yao?
Hivi tunavaa kwa ajili ya fasheni? ili tuonekane vizuri na wasichana wenzetu?
Au tunavaa ili tujisikie vizuri wenyewe?
Manake kuna manywele ya kubandika, vipodozi vya kila aina, nguo za kila aina. Je alie muhimu kuona kama nimependeza ni nani?
Kuna wakatu navaa nguo very uncomfortable, mfano kuzuia baridi, tunaenda pati na migongo wazi, tunatembea na viatu virefu. nguo inabana mpaka inaacha alama nk nk

Haika,
Hii topic ni murua maana tumekuwa tukiangalia siasa na mambo ya public domain tukajisahau na sisi wenyewe.We need to take care of ourselves too.

.... kwa upande wangu nadhani ni combination of what you have said... but the bottom line is to go with what makes you feel confident and what is appropriate for the occassion ( looking good, feeling good)
Na katika kufanikisha hilo... lazima ufikirie pia umri wako, shape yako, where you are n.k.Kwa mfano unaweza kujisikia kuvaa nguo fupi lakini itakuweka matatani kama utapita uswahilini..watakutupia mawe bure!Unapaswa kuzingatia utamaduni wa mahali husika...
Kigezo kingine ni hali ya hewa...huwezi kuvaa boots kwa mfano ilhali kuna joto la kuua mtu..utaonekana mshamba na pia utakosa raha.
Viatu virefu - mwanamke shurti ujue kuvitembelea ndo utapendeza.Siyo kujilazimisha au kufa kishujaa huku miguu inakupwita kwa maumivu!
Make-up - inapendeza kama ukijijua rangi yako inaendana na make-up gani...inafaa upate ushauri ( get a make-over then buy what suits you!)
Accessories.... hii ni muhimu katika kuweka final touches..ila nazo zataka uzijulie kuendana na wewe ulivyo ....
nadhani wachangiaji wengine wataongezea ili kwa pamoja tuendelee kujifunza.
 
At least nimeisoma hii kutoka kwa mwanamke!!
Mimi nimekuwa nikijiuliza saana maana siku zote naona wanawake kama wanaenda extra mile in life just to look different!! mfano unakuta mdada yuko saluni kawekwa kwenye steamer sijui hadi anatoka machozi lakini akitoka hapo akipewa tu sifa anasahu maumivu ya steaming!!!

Viatu virefu > inafikia mahali unakuta mdada anatembea na viatu pea mbili, pea moja vya kutembelea umbali mrefu na pea nyingine anapokuwa kwenye maeneo anayotaka aonekane na yeye kapendeza!!

Mavazi > kwa wale wanaoenda party huku migongo iko wazi huishia kupigwa baridi kiasi kwamba wanapata vichomi. Mara nyingi baada ya party hukimbilia kuchukua makoti ya wapenzi/waume zao ili kujikinga na baridi (too bad urembo unawasababishia yote haya)

Mimi nadhani wanawake hupendeza katika hali ya kawaida kwa kuvaa nguo zinazowasitiri kwa heshima na pia wanapata heshima zaidi kutokana na nguo au urembo wanaoutumia. Just try to look smart and decent. Sio kila mtu ana haki ya kuiona chupi yako ila tu kama uko katika mazingira kama beach unaweza jivinjari kihivyo sio vinginevyo.
 
....vanity is the ar*e on this planet... so unfortunate, innit!!

....Haika, utanisamehe, sijatoa ushauri, naona wenzangu wamesha-discuss kwa kina hapo juu. Unless, unless unaomba ushauri katika style mojawapo unayotaka kuvaa, undoubtedly, i'll jump in to the rescue!! ;)
 
Nimekuwa nikiangalia sana mitindo ya mavazi hasa ya kina dada na kina mama. Mitindo ya nywele, mavazi, viatu, mapambo (acessories) na kadhalika.
Pia nimekuwa nikisikiliza maoni na sababu zao za kuwa na machaguo yao mbalimbali.
Pia kuna mawazo na maoni ya kina kaka na kina baba kuhusu huu mwenendo.
Kwa sasa nimejikuta nimechanganyakiwa.
hivi tunavaa nguo za kubana, kutuacha uchi au kujifunika mwili mzima kwa ajili yao?

Hivi tunavaa kwa ajili ya fasheni? ili tuonekane vizuri na wasichana wenzetu?
Au tunavaa ili tujisikie vizuri wenyewe?
Manake kuna manywele ya kubandika, vipodozi vya kila aina, nguo za kila aina. Je alie muhimu kuona kama nimependeza ni nani?
Kuna wakatu navaa nguo very uncomfortable, mfano kuzuia baridi, tunaenda pati na migongo wazi, tunatembea na viatu virefu. nguo inabana mpaka inaacha alama nk nk

"...modelling is a form of pornography. The beauty shows have been a major platform for the reduction of women from full human beings into mere objects to be admired". ~ Asher Mutsengi

.
 
I sometimes agree with lazydog.
But why is it being accepted by the wider community?
Hakuna kiongozi wa kukemea?
au kwa sababu (wanaume) wanaenjoy?

Najua wanasema tunachagua vazi : unalojisikia vizuri, au ambalo ni comfortable.
Sasa kama ini makosa kama ili ujisikie vizuri lazima ufeel sexy (kama wanavyosema wataalamu)?

I think i know what is proper dressing, but that is not what is in practise now.
Why is there such a great need for sensuality in dressing?

nimekuja na hii mada baada ya kupata shock alikuja mpwa wangu home na kinguo amabacho ilibidi nimseme kama nusu saa halafu baadae nikaanza kujiuliza kuna nini duniani. manake huyo mtot ni so innocent, hana mbele wala nyuma akidanganywa na yeyote tu ataenda kwa uhakika, nadhani hajui upeo wa alichokuwa anapotray, anadhani ni kupendeza tu basi.
 
This is where a parent gets involved ... lawama zote zinaelekea kwa mzazi ... how did this young girl get such clothings and how did she leave the house in that state ... where were the parents or someone matured to check that she wasnt properly dressed ... where were the neighbours .... au hata mwanamke mwenye uchungu na huyu mtoto kumkanya hata barabarani kwamba shes isnt dressed properly ... ingetokea mtoto kama huyu akabakwa (Mungu apishe mbali) watamlaumu nani kwa kinguo hicho???? WOMEN PLEASE WE HAVE TO START ACTING RESPONSIBLE ... by this kwanza tuvae nguo za heshima halafu tuwafundishe / tuwanunulie watoto wetu nguo za heshima pia ... halafu tuwe wazazi popote tulipo kwa kuwaangalia watoto wa wenzetu na kuwashauri
 
....Naima nadhani hapo kubwa ni kwa wazazi na au walezi kuelewa ni mavazi gani mtoto wa kike anastahili kuvaa lakini suala la kuwa wazazi wa watoto wote ni jambo gumu kutokana na mazingira ya kimaisha yalivyo siku hizi. Sio rahisi kwa mwanamke kumsemesha msichana kuwa nguo aliyovaa si ya heshima kwa kweli usishangae hata huyo binti akamtusi huyo mwanamama...heshima imeshuka kwa kiwango cha kutisha. Mi nadhani wazazi na walezi ndio wa kubeba lawama kwenye hili suala la mavazi kwani msichana yeye anakuwa kama kasuku kwa kupenda kuiga kila anachokiona bila ya kutambua kuwa mengine ni udhalilishaji na mzazi au mlezi anaona lakini anakuwa kimya..

Hakuna maadili kabisa wenyewe wanadai wanakwenda na wakati. Nakumbuka tukio moja katika hiace tuliyopanda aliingia binti wa kama miaka 17 au 20 amevaa suruali ya jeans na kitop kifuli sana alipokaa kwenye kiti kitop kikapanda juu na almost chupi yote aliyovaa (ilikuwa bikini) ilikuwa nje hakuna mtu aliyesema kitu na kulikuwa akina mama wakubwa wanaoweza hata kumzaa yule binti but watu wakabaki kutazamana tu... alipoteremka katika kituo alichotaka ukabaki mjadala kwa waliobaki kwenye gari juu ya kivazi cha binti...Sasa hapo kuna tiba ya tatizo kama hilo??? Tunatakiwa tujiangalia upya na haya mambo ya utandawazi na kuiga mambo yasiyofaa.
 
This is where a parent gets involved ... lawama zote zinaelekea kwa mzazi ... how did this young girl get such clothings and how did she leave the house in that state ... where were the parents or someone matured to check that she wasnt properly dressed ... where were the neighbours .... au hata mwanamke mwenye uchungu na huyu mtoto kumkanya hata barabarani kwamba shes isnt dressed properly ... ingetokea mtoto kama huyu akabakwa (Mungu apishe mbali) watamlaumu nani kwa kinguo hicho???? WOMEN PLEASE WE HAVE TO START ACTING RESPONSIBLE ... by this kwanza tuvae nguo za heshima halafu tuwafundishe / tuwanunulie watoto wetu nguo za heshima pia ... halafu tuwe wazazi popote tulipo kwa kuwaangalia watoto wa wenzetu na kuwashauri

Wadau kwenye suala la malezi ni wengi. Hakuna shaka kuhusu mchango wa utandawizi kwenye hili; tuangalie upande mwingine wa shilingi.
Aliyekuwa msaada mkubwa sana kwenye malezi ni mwalimu. Sio rahisi sana leo kwa mzazi kumzuia bintie (miaka 12) asivae high-heels kwenda shule kungali wenzie wanafanya hivyo. Nafasi na thamani ya mwalimu sote twaifaham.

Mtoto wa darasa la tatu anaficha ki-top kwenye mfuko wa shule ili akavae akifika huko. (Ki-top hiki ni nguo yake ya utotoni ambayo keshakatazwa na mamake kuvaa). Unajiuliza hivi huko shule kuna waalimu? Baadae unang'amua kwamba kumnyoshea kidole mwalimu ni kumwonea.

.
 
Kipindi cha utawala wa kwanza wa MWL Nyerere ukivaa hizo nguo ambazo nyuma huku wanasoma plate number yako adhabu yake ilikuwa kufagia barabara,leo ukifanya hivyo unakiuka haki za binadamu.

Ukihudhuria sherehe yoyote au ngwasuma utaona jamii yetu imegeuka kabisa,akina dada wengine mwili ni bonge lakini utakuta kavalia kanguo ka ajabu yaani kanamfanya kituko,kifua chote nje na unasoma alama za nyakati.

Hili suala ni mtu mwenyewe kujiheshimu na kuthamini utu wake na pia kulinda familia zetu kwa bidii na huu ugonjwa wa magharibi.
 
Lets face it, hivi wakipita wanawake wawili, wote wanamaumbo ya kuvutia, mmoja kaexpose sehemu sensitive za mwili wake au kavaa vivazi cha kubana na mwingine kavaa kiheshima - nguo haija mbana na haja expose sehemu yoyote ya paja, titi, makalio, mgongo wala tumbo to be specific nani atakeayetizamwa zaidi?... Mimacho karibu yote (kiwaziwazi na kisirisiri) ya wanawake na wanaume yatamkodolea huyo mwenye kivazi, na wanaume wengine utaona kabisa wanamwangalia mwangalia kwa jicho la kumtamani
Mwanamke akipata attention kama hiyo anajisikia

amependeza
anatamaniwa na kupendwa hasa na wanaume
anaenda na fasheni
hayuko tofauti na wenzie

na ndio maaana hizi fasheni za kuanika anika na kubanabana haziishi, hasa kwa wasichana wadogowadogo, zinauzika sana tu, tena unaweza kuta mama na mwanae wanongozana mtoto nusu ya makalio nje nusu ya titi nje, mama ki jeans kimembanaa na kumchora maungo utadhani mfuko wa gitaa. Nadhani mabinti wakiwa karibu sana na familia zao hasa wazazi , na kupata upendo wa kweli kwenye familia zao, na kufundishwa hasa kwa kuangalia mfano, watakuwa tofauti kidogo

 
Mimi nadhani kila occasion na vazi lake jamani. Kuna hizo nguo zinaitwa night wear nyingi zinakuwa migongo wazi, na wanawake wengi wanakwenda na wakati. tofauti na wanaume. Mimi kwa hizo nguo sioni kama kuna matatizo, wewe mwenyewe ukitoka na mamsap wako unapenda kumuona kapendeza.

Kitu ambacho mimi nakipiga vita ni hizi suruali ambazo mwanamke akikaa nyuma chupi yote inaoneka au mfereji wa kwenda kule mahara wote unakaa wazi, hilo kwa kweli ni tatizo.

Wanawake jamani jalibuni kujisitiri na pia mkae mkijua kila vazi na muda wake, sio nguo za usiku manavaa mchana na mnaanza kulandalanda jiji zima.
 
Wanawake jamani jalibuni kujisitiri na pia mkae mkijua kila vazi na muda wake, sio nguo za usiku manavaa mchana na mnaanza kulandalanda jiji zima.

Ukiona mtu kavaa vazi ambalo si wakati wake au pahala pake basi ujue uwezekano mkubwa ni kuwa kaazima! Hahaha!!
 
from a woman point of view, u can look sexy and still be decent, kwenda na wakati si mbaya ila ujue tu maana ya ustaarabu, waweza tofautisha kati ya classy na trashy, hakuna point ya kuvaa kitu ambacho kitakufanya uwe uncomfortable au kuwafanya wengine kuwa katika hali hiyo, cha kuzingatia kwenye mavazi ni kuwa lazima yaendane na umbo lako pia na wakati, kama ni usiku, mchana nk, pia ku reveal too much sehemu nyeti sio sexy, mwanamke anayejiheshimu na kupangilia mavazi yake ana mvuto wa kipekee, lakini yule anayejiachia achia hujishusha thamani na kuonekana cheap. so take a lesson from classy sexxy woman...me, always be classy dont wear it because everybody wears it.
 
What do you mean when you say sexy is okay?
Au labda un maana gani unaposema 'sexy'? ina uhusiano wowote na 'jina' (noun) la hicho kisifa? and is it okay kupita barabarani ukiwa na mtazamo huo?
Kwanini utake kuwa sexy wakati unajua unafukua sexual feelings za watu walio kwenye shughuli zao?
Does classy mean sexy (katika mavazi)
 
Last edited:
mwili wa mwanamke si wa kuonea haya.. uzuri hupambwa... na asiye mzuri hata ajipambe vipi haongezi uzuri wake, zaidi ana uangaza ubaya wake.. mwanamke asiyejipamba kuonesha uzuri wake ni sawa na waridi lilifichwa chunguni... katika yote kila kitu kwa kiasi kwani katika maisha yangu nimegundua vitu vichache kimoja ni kuwa uzuri na wema si kitu kile kile...
 
Tatizo ni pale unapowaambia watoto vazi lile na lile baya, halafu home hutaki kukaa kihasara hasara - unatia vivazi vya kumchanganya mzee..... halafu mtoto anatia - mama hiyo nguo mbaya........
Maswala ya mavazi ni very subjective
 
What do you mean when you say sexy is okay?
Au labda un maana gani unaposema 'sexy'? ina uhusiano wowote na 'jina' (noun) la hicho kisifa? and is it okay kupita barabarani ukiwa na mtazamo huo?
Kwanini utake kuwa sexy wakati unajua unafukua sexual feelings za watu walio kwenye shughuli zao?
Does classy mean sexy (katika mavazi)
Yaani nilikuwa namaanisha kuvutia bila kujidhalilisha. kuvutia huko sio lazima kufukue hisia za kimapenzi, bali kukuweka kwenye hadhi fulani watu wanaku admire na kukuheshimu that what i meant by classy. Trashy ni pale unapo over do kitu fulani na kinaishia kukufanya uonekane kituko mbele ya jamii. Kila mtu ana namna ya kutafsiri mambo, na hiyo ndo tafsiri yangu.
 
aisee mi ngoja niende kushoto kidogo,wanawake wanavaa ili wapendeze wanapotoka, ila suala wapendeze kwenye macho ya nani,hapa bwana ni kwa wote kwa wanawake wenzao na wanaume pia, lakini tukiweka percent hapa kwa ajili ya wanaume inaweza kua kama 90% hivi halafu hiyo 10% ndio kwa wenzao. mfano wanasema kimini mwenzake mguu (na mapaja,hii huwa haisemwi),sasa miguu na mapaja mazuri nani anatakiwa athaminishe hapa? eeh nadhani majibu mnayo mi sisemi,maana matangazo ya bia kwa wanywaji bwana eeeh.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom