Naomba ushauri kwa wanaojua ugonjwa huu wa Nguruwe

DENAMWE

JF-Expert Member
Dec 29, 2019
806
805
Habari za usiku?

Nguruwe wangu mmoja alipoteza hamu ya kula. Baada ya siku moja tulimtoa zizini tukamweka nje ambako hakuna sakafu.
Aliendelea kukataa chakula chochote. Hakutaka kunywa maji. Alitumia muda mwingi kufukua na kuchimba kwa pua yake.

Alikuwa na nguvu nyingi za kufukua. Alipokuwa akichoka analala. Tulihisi ni homa ya nguruwe lakini hakuwa na homa, hakutapika, hakuharisha.

Baada ya siku tano tangu kuona dalili tulimchinja ili kufanya uchunguzi wa tatizo alilokuwa nalo. Daktari alibaini alikuwa amevimba na kuoza ini mojawapo. Hakuwa na tatizo jingine.

Leo nimeona nguruwe wengine wawili wenye hali hiyo. Hao na wengine waliosalia amewadunga vetoxy.

Naomba msaada wenu wadau.
 
Ungemtembeza nguruwe kwenye majani angepata majani yenye tiba yake. Alipokua anachimba alikua anatafuta dawa.

Mbwa wa rafiki yangu alimeza kokoto na iliziba kwenye utumbo. Tulishngaa kumuona mbwa anakula maua ya bustani mpaka anaanza kutapika, kumbe alikua anatafuta njia ya kitoa ile kokoto.

Kuna siku alikula majani akaanza kuharisha, kwenye choo chake tuliona kokoto na baada ya hapo aliacha kula majani na maua.
 
Back
Top Bottom