naomba ushauri kwa hili

mbalila

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
823
157
mimi ni mfanyakazi wa umma ,nataka kuomba mkopo wa mabati kutoka kwenye kampuni ya TUNAKOPESHA LIMITED malipo yao ni miezi 36 yaani miaka mitatu, sijaona mkataba wao ila viambatanisho ni salary slip mbili, bank statement ya miezi sita ya nyuma na photocopy ya kadi ya benk,sasa naomba kama wenye uzoefu na hawa watu anijuze naomba kuwasilisha .
 
Dah! mi mwenyewe mpango wangu ndo huo lakini siwajui vizuri!, ngoja 2wasubiri wadau!
 
Usithubutu kabisa, wanatumia compounding interest method kama sijakosea ukikopa mil 3 unaweza ukalipa mil 6 au 7 kwa hiyo miaka mitatu. Hao jamaa ni wezi sana
 
wala usijaribu mkuuu kwanza wanakata hela kubwa mno kama hivyo dunduliza tu uwe unanunua hata bando tatu mpaka umalize au kachukue mkopo benki hao ni wakoloni weusi tanzania
 
Back
Top Bottom