Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Habari za muda huu wadau nimeteseka sana na vidonda vya tumbo sasa nataka ushauri hospitali gani niende naweza pata vipimo vizuri vikanisaidia,hapo mwanzo nilikuwa naenda hospital za kawaida kutokana na kipato ila kwa sasa nimekusanya pesa kama laki tisa kwa ajili ya kwenda kupata vipimo vya uhakika,Nitangulize shukran kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Dawa ya vidonda ni kupunguza mawazo / stress.
Ukilala kunywa dawa ya kuleta usingizi kama vile Piriton, koflyin au pombe kali nusu glass. Ukilala unalala fofofo na wala hutosikia tumbo likikuuma.
 
Habari za muda huu wadau nimeteseka sana na vidonda vya tumbo sasa nataka ushauri hospitali gani niende naweza pata vipimo vizuri vikanisaidia,hapo mwanzo nilikuwa naenda hospital za kawaida kutokana na kipato ila kwa sasa nimekusanya pesa kama laki tisa kwa ajili ya kwenda kupata vipimo vya uhakika,Nitangulize shukran kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Badilisha diet ya uchafu unaoingia tumboni.....acha mavyakula yenye Acid tumboni mwako punguza kula damu (nyama) kula matunda kwa sana na mboga mboga ndio kiwe chakula chako. Na unywe maji mengi sana.
Acha na masoda ya gesi au energy drinks.
CHAKULA CHAKO NDIO UGONJWA WAKO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unataka kufanya endoscopy... inatisha na kuogopesa sana..!! sasa basi jitahidi kuacha vyakula vyote ulivyoshauriwa kisha ule sana maparachichi na kabage.. pia kunywa maji ya moto..

wewe fanya kuitibi kiu yako na maji ya moto.. utapona kabs.. anza sasa leo jioni usilale bila maji ya moto kuwa kinywaji chako cha mwisho.
 
Mimi nilitumia laki nne hospital..baadae Sana nikagundua nilifanya upuuzi..maana sikupata tiba hospital..wewe epuka vyakula ulivyokatazwa..tumia asali Sana..na ile dawa ya vidonda ipo Kama maziwa..la muhimu kuliko yote Ni Kula chakula kwa wakati..asubuhi Kula au kunywa chai na vitafunwa mchana kula na usiku kula hata Kama huna njaa..ukisikia maumivu tumia frajilini (nimeandika inavyotamkwa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.

stomach_ulcers
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
...Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
...Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
Kushindwa kumeza vizuri chakula.
Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
Kujisikia vibaya baada ya kula.
Kupungua uzito.
Kukosa hamu ya kula.

DALILI HATARI
Kutapika damu.
Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
Kichefuchefu & kutapika.

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-

Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

Kupima damu 'Blood test'

Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

Kupima pumzi 'Breath test'

Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'

Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'

Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs'

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

Matibabu kwa njia za asili, zipo dawa mbali mbali unazoweza tumia zikiwa kwenye mfumo wa unga au kimiminika

Kwa ushauri na tiba kwa maradhi mbali mbali wasiliana nasi.
what's app /call
+255 655 821 550
Sulayman Sangida

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuata ushauri kupitia hii post. Hosp waweza kuandikiwa Heligo kit, ina dawa zenye combination nzuri. Ukifuata masharti yake utapona kabisa!

Kikubwa angalia namna yako ya ulaji. Epuka vyakula vyenye maasidi. Utapona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
awali ya yote nikupe pole sana
Mkuu maradhi mengi ya kiafya yanaletwa na ulaji wetwa zaidi ya 90% kama ndivyo pia dawa yake ipo huko huko kwenye vyakula, unaweza tumia dawa za hospitali na mitishamba ila utapata nafuu baada ya muda utaona hali ni ile ile na ukijaribu kufuatiia wengi wenye vidonda vya tumbo hakuna aliyewahi kupona angalao mwaka mzima hajalalamika vidonda vya tumbo hata wale wanaotumia dawa za asili
Sababu ni kuwa watu hawajajua chanzo cha magonjwa na hatakama wakitumia hizodawa bado mwilini wanarudisha sumu ile ile ambayo inawaangamiza,
Ushauri wangu kwako achana na vyakula vyote vya wanga na sukari maanda ndivyo chimbuko la maradhi mengi ya mwili, nafahamu utaniuliza sasa ule niniii? utapataje nguvu? utawezaje kumudu gharama za vyakula vingineee?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom