Naomba ushauri kuhusu vidonda vya tumbo


Jumong S

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Messages
4,863
Points
2,000
Jumong S

Jumong S

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2013
4,863 2,000
VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.

stomach_ulcers
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

SABABU ZA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
...Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
...Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
Kushindwa kumeza vizuri chakula.
Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
Kujisikia vibaya baada ya kula.
Kupungua uzito.
Kukosa hamu ya kula.

DALILI HATARI
Kutapika damu.
Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
Kichefuchefu & kutapika.

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-

Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

Kupima damu 'Blood test'

Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

Kupima pumzi 'Breath test'

Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'

Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'

Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs'

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

Matibabu kwa njia za asili, zipo dawa mbali mbali unazoweza tumia zikiwa kwenye mfumo wa unga au kimiminika

Kwa ushauri na tiba kwa maradhi mbali mbali wasiliana nasi.
what's app /call
+255 655 821 550
Sulayman Sangida

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuata ushauri kupitia hii post. Hosp waweza kuandikiwa Heligo kit, ina dawa zenye combination nzuri. Ukifuata masharti yake utapona kabisa!

Kikubwa angalia namna yako ya ulaji. Epuka vyakula vyenye maasidi. Utapona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thanos

thanos

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Messages
884
Points
1,000
thanos

thanos

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2018
884 1,000
Kwa navyo jua vidonda vya tumba havina dawa.... badilisha aina ya lifestyle yako... mimi nilikua napata shida sana mwanzoni lakini saivi niko safi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
1,272
Points
2,000
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
1,272 2,000
awali ya yote nikupe pole sana
Mkuu maradhi mengi ya kiafya yanaletwa na ulaji wetwa zaidi ya 90% kama ndivyo pia dawa yake ipo huko huko kwenye vyakula, unaweza tumia dawa za hospitali na mitishamba ila utapata nafuu baada ya muda utaona hali ni ile ile na ukijaribu kufuatiia wengi wenye vidonda vya tumbo hakuna aliyewahi kupona angalao mwaka mzima hajalalamika vidonda vya tumbo hata wale wanaotumia dawa za asili
Sababu ni kuwa watu hawajajua chanzo cha magonjwa na hatakama wakitumia hizodawa bado mwilini wanarudisha sumu ile ile ambayo inawaangamiza,
Ushauri wangu kwako achana na vyakula vyote vya wanga na sukari maanda ndivyo chimbuko la maradhi mengi ya mwili, nafahamu utaniuliza sasa ule niniii? utapataje nguvu? utawezaje kumudu gharama za vyakula vingineee?
 
S

Salim athumani

Member
Joined
Jan 18, 2019
Messages
5
Points
20
S

Salim athumani

Member
Joined Jan 18, 2019
5 20
tumia majani ya msagi sagi chemsha kisha kunywa kikombe kimoja kutwa mara tatu siku kumi 4 km huyajui njoo what's app nikutumie picha 0710 271 852

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nzory Mussa

Nzory Mussa

Senior Member
Joined
Jan 20, 2017
Messages
187
Points
250
Nzory Mussa

Nzory Mussa

Senior Member
Joined Jan 20, 2017
187 250
Ukienda hospital unaweza ukapewa HELIGO KIT, hii ni dawa nzuri sana ya vidonda vya tumbo na ukizingatia maelekezo utakayopewa unaweza ukapona kabisa.

Lakini kitu kikubwa ni DIET, Jaribu kufuatilia ushauri juu ya vyakula gani ule na vyakula gani usile uliotolewa na wachangiaji waliotangulia kabla yangu.

POLE SANA, MWENYEZIMUNGU ATAKUPONYA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
5,377
Points
2,000
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
5,377 2,000
Habari za muda huu wadau nimeteseka sana na vidonda vya tumbo sasa nataka ushauri hospitali gani niende naweza pata vipimo vizuri vikanisaidia,hapo mwanzo nilikuwa naenda hospital za kawaida kutokana na kipato ila kwa sasa nimekusanya pesa kama laki tisa kwa ajili ya kwenda kupata vipimo vya uhakika,Nitangulize shukran kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nikupe ushauri wa bure na inaweza kukugharimu kiasi tu kama ushapimwa ukakutwa na bakteria wa hpyrol basi omba vidonge vya Heligo kit hizo dawa ni bomba ila madaktari wengi humpa mgonjwa dozi moja tu yaani dawa za siku saba tu kisha hukupa dawa zingine kwa muda wa mwezi mzima. Sasa ushauri nilipata kwa Dr mzoefu. Hizo dawa unatakiwa uzinywe set tatu kila siku hadi wiki tatu ziishe tumia ujanja wako maana madokta watakukatalia wakijua ushatumia zaidi ya wiki mbili. Tatufa hata mtu akununulie ukishindwa wewe.

Ni hivi hizo dawa first wiki inaua wadudu ila sio wote second week inakausha vidonda na third week inatengeneza makovu sehemu zilizokuwa na vidonda. Hivyo ukipona hata pilipili utakula bila khofu.

Dawa huwa zinanguvu kama afya yako ni mgogolo hutaweza zimaliza na utapona kwa muda tu.

Unywaji wa dawa unafuata kama maelezo yake picha ya mwezi unakunywa usiku na picha ya jua unakunywa asubuhi. Kiujanja kula chakula robo sahani kisha meza dawa and then malizia msosi wote uufute sahanini . Hautasikia kabisa nguvu ya hizo dawa.

Amini Amini nakufahamisha wengi walionisikiliza walipona hata kama unaumwa kifua maana hao wadudu hutafuna hadi kifua njia ni hiyo hiyo.

Ukipona uje ugonge like.
 
mikumiyetu

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Messages
919
Points
1,000
Age
30
mikumiyetu

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2016
919 1,000
Mkuu nikupe ushauri wa bure na inaweza kukugharimu kiasi tu kana ushapimwa ukakutwa na bakteria wa hpyrol basi omba vidonge vya Heligo kit hizo dawa ni bomba ila madaktari wengi humpa mgonjwa dozi moja tu yaani dawa za siku saba tu kisha hukupa dawa zingine kwa muda wa mwezi mzima. Sasa ushauri nilipata kwa Dr mzoefu. Hizo dawa unatakiwa uzinywe set tatu kila siku hadi wiki tatu ziishe tumia ujanja wako maana madokta watakukatalia wakijua ushatumia zaidi ya wiki mbili. Tatufa hata mtu akununulie ukishindwa wewe.

Ni hivi hizo dawa first wiki inaua wadudu ila sio wote second week inakausha vidonda na third week inatengeneza makovu sehemu zilizokuwa na vidonda. Hivyo ukipona hata pilipili utakula bila khofu.

Dawa huwa zinanguvu kama afya yako ni mgogolo hutaweza zimaliza na utapona kwa muda tu.

Unywaji wa dawa unafuata kama maelezo yake picha ya mwezi unakunywa usiku na picha ya jua unakunywa asubuhi. Kiujanja kula chakula robo sahani kisha meza dawa and then malizia msosi wote uufute sahanini . Hautasikia kabisa nguvu ya hizo dawa.

Amini Amini nakufahamisha wengi walionisikiliza walipona hata kama unaumwa kifua maana hao wadudu hutafuna hadi kifua njia ni hiyo hiyo.

Ukipona uje ugonge like.
Asante kwa ushauri leo ndo naenda hospital moja iko makete inaitwa ikonda nikapime vipimo vyote vya tumbo nitarudisha feedback

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mikumiyetu

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Messages
919
Points
1,000
Age
30
mikumiyetu

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2016
919 1,000
Ukienda hospital unaweza ukapewa HELIGO KIT, hii ni dawa nzuri sana ya vidonda vya tumbo na ukizingatia maelekezo utakayopewa unaweza ukapona kabisa.

Lakini kitu kikubwa ni DIET, Jaribu kufuatilia ushauri juu ya vyakula gani ule na vyakula gani usile uliotolewa na wachangiaji waliotangulia kabla yangu.

POLE SANA, MWENYEZIMUNGU ATAKUPONYA

Sent using Jamii Forums mobile app
Asantee sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M2baki

M2baki

Member
Joined
Feb 25, 2013
Messages
52
Points
125
M2baki

M2baki

Member
Joined Feb 25, 2013
52 125
Pole na shida hyo, binafsi niliumwa na vidonda vya tumbo kwa miaka mitatu Lakini nilielekezwa na jamaa niliyekutana na ye. Niliekezwa bure nami natoa bure. Tafuta majani flani ntaatach hapa ya aina mbili nayo ambayo utayachuma na kuyatwanga yakiwa mabichi na kisha kuandaa maji ya uvuguvugu na kisha kuyachanganya na hiyo rojo na kisha chuja. Kikombe kimoja cha robo lita kwa siku 3. Nawe utaona kama nilivyopona. Nina mwaka wa 4sasa toka nione. So ni hakika na nisemalo. Majina ya hayo majani siyajui kwa majina yake ila picha zake ndio hizo hapo. Enjoy the remedy
img_20161215_154658_1555858127415-jpeg.1077568
img_20161215_150351_1555858098614-jpeg.1077569
 

Forum statistics

Threads 1,285,934
Members 494,834
Posts 30,879,420
Top