Naomba ushauri kuhusu ugonjwa wa ngozi kwa huyu mtoto

Sangoma

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
342
162
Wakuu habari za majukumu leo katika pitapita zangu nimekutana na huyu mtoto sio siri amenigusa kwa hali aliyo nayo anateseka kwa maelezo ya wazazi wake huu ugonjwa anao tokea amezaliwa na hivi sasa anamiaka 2 ameshaenda hospital kadhaa kadhaa za kawaida kulingana na uwezo wake wa kifedha ila bado ajapata tiba sahihi msaada wenu wa mawazo kwa upande wangu nimeguswa nahitaji kusaidia kidogo ikiwa ni kumchukulia bima ya toto afya kadi.

IMG_9109.jpg

IMG_9107.jpg

IMG_9105.jpg
 
Kama umeguswa sidhani kama ni jambo la kuomba ushauri, wewe endelea na taratibu za kumkatia bima na Mungu atakubariki sana..
Ila umekosea kuweka sura yake mtandaoni, kwani sidhani kama mtoto ameridhia kitendo hiki ambacho pengine akukia mkubwa hatofurahishwa na kitendo cha yeye kuikuta picha yake ya utotoni kwenye mitandao ya kijamii..
 
Kama umeguswa sidhani kama ni jambo la kuomba ushauri, wewe endelea na taratibu za kumkatia bima na Mungu atakubariki sana..
Ila umekosea kuweka sura yake mtandaoni, kwani sidhani Kama mtoto ameridhia kitendo hiki ambacho pengine akukia mkubwa hatofurahishwa na kitendo cha yeye kuikuta picha yake ya utotoni kwenye mitandao ya kijamii..

Nisamehe mkuu na pia kumbuka insue ya toto afya kadi inachukua miezi 3 siku 90 lengo ni ushauri hata wa dawa kwa muda huo au chochote kitakacho kuwa msaada kwake
 
Back
Top Bottom