Naomba ushauri kuhusu tatizo hili la jicho kulalia upande mmoja kwa mwanangu

mfuga kuku

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
750
544
Habari wana bodi,

Hivi karibuni nimepatwa na tatizo binti wa kazi kamdondosha mtoto wangu wa miezi minne. Alikuwa anambeba mgongoni, kwa maelezo yake, mtoto akadondoka.

Kilichoendelea hapo mama wa mtoto kuitwa na kumkimbizia mtoto hospitali.

Hali ya mtoto iko vizuri kiasi isipokuwa kile kiini cha jicho, kile cheusi, kimelalia upande mmoja hakichezi chezi kama zamani.

Baada ya kufika hospitali daktari ametoa maelekezo kuwa kuna mshipa umegandamizwa, mshipa wa fahamu na upo uwezekano mkubwa wa mshipa huo kurudi taratibu mahala pake na jicho kurejea katika hali ya kawaida, na ametoa muda wa kusubiria ni miezi 6.

Sasa je, nawauliza kwa yeyote anaejua, hofu yangu mtoto asije pata ulemavu wa kudumu. Hakuna tiba ya kurejesha hii hali? Hakuna hospitali ambayo naweza pata ufumbuzi wa kueleweka? Nisije kushtuka niambiwe umemchelewesha mtoto.

Please wanabodi, kama pia mtu ana uzoefu na hili anijulishe.

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Mkuu. Najaribu kuvaa viatu vyako hali uliyonayo haielezeki. Vuta subira kama ulivyoelekezwa lakini pia wataalam wa hyo sekta waje watoe neno
 
Back
Top Bottom