Naomba ushauri kuhusu mpenzi niliye naye

bado Ana akili za kitoto,
ujadili maisha ya mbeleni na MTU anae resit mtihani wa 4m4

huwezi kuwa serious....
hivi chuo wanawa fundishaga nini?
kuna haja ya walimu kuwafundisha kujitambua!
msimdiscourage kijana et ana akili za kitoto , ana mawazo mazuri tu na anafikiria mbali na thats why anataka kujua future yake, there's nothing wrong with that
Maisha ya mbeleni wakat ndio kwanza mpo kwny balehe...soma kwanza mtt dudu lipo tu
 
Mimi ni msichana wa miaka 20 nipo Chuo Kikuu mwaka wa kwanza lakini nilitokea kuanzisha mhusiano na Mwanaume nikiwa form three. Nampenda na nimekuwa mwaminifu kwake toka nilivyoanzisha mahusiano naye.

Lakini yeye alikuwa mbele yangu kimasomo na alivyomaliza kidato cha nne hakufanikiwa kujiunga na kidato cha tano hivyo akaamua kurudia mtihani mara ya pili. Mimi nilivyomaliza kidato cha nne nilifanikiwa kujiunga na kidato cha tano hivyo nikawa nimemwacha hatua kadhaa nyuma.

Matokeo yake yalivyotoka akawa amefeli tena kwa mara ya pili lakinihakukata tamaa akarudia mtihani kwa mara ya tatu. Sasa mimi nipo Mwaka wa kwanza na yeye anasubiri matokeo ya kidato cha nne.

TATIZO NI KWAMBA NIKIMUULIZA MAISHA YETU YA MBELENI HATAKI TUZUNGUMZIE HILO na ninaona kuwa tayari kila mtu anahitji kutimiza malengo yake na mimi nataka nikimaliza chuo niolewe ila atakuwa bado anasoma.

NAOMBENI USHAURI WENU NIFANYEJE?
Usimuacha mwenzio, mmetoka mbali! ni bora uyo, kuliko uje mpata usie mfahamu kabisa!
 
Bado sijaanzisha mahusiano na mtu mwingine
Naomba jaribu kukaa nae tena muongeee japo najua kwa sasa anajiona hana umhimu kwako due to education inferioty coz ur so far beyond him. But Cc* naomba tumia lugha ya kumfariji ili arudi kwenye hali ya kawaida huenda akakupa jibu la umsubirie kama utaweza au akupe ruhusa uolewe ila ukimwacha tu tambua malipo yatakuwa hapa duniani. So plz take a time then if ur not so far from where ur partner found make sure u meet with him then u may use polite lovely language u can hear a lot of things from him about what he feels on u. Yangu hayo kama kweli wampenda
 
Naomba jaribu kukaa nae tena muongeee japo najua kwa sasa anajiona hana umhimu kwako due to education inferioty coz ur so far beyond him. But Cc* naomba tumia lugha ya kumfariji ili arudi kwenye hali ya kawaida huenda akakupa jibu la umsubirie kama utaweza au akupe ruhusa uolewe ila ukimwacha tu tambua malipo yatakuwa hapa duniani. So plz take a time then if ur not so far from where ur partner found make sure u meet with him then u may use polite lovely language u can hear a lot of things from him about what he feels on u. Yangu hayo kama kweli wampenda
Ok asante sana
 
Du! Ndio maana wanasema msianze mahusiano mkiwa masoni sasa hilo ni tatizo na jamaa ana umia kisaikoloji Labda utafute mwingine,afu wewe usome acha ujinga bado ni mdogo sana zingatia elimu,"sawa binti yangu"
 
Sema ukweli kwamba ushampata mwingine huko chuo yaan hapa hata bado test hazijachanganya vizur ushaanza kuwaza ndoa,wewe binti kuwa makini utachezewa sana na kuachwa maana unaweka wazi unataka ndoa.

Soma, ndoa itakuja tu either kwa huyo jamaa au kwa mwingine. Supplementary na carry sio za mchezo mchezo hasa ukiziletea stress za mapenzi
Huu ndiyo ukweli hakuna nini wala sijui imekwendaje umegonga nyundo ya kichwa
 
Akahitimu kidato cha nne wewe ukiwa kidato cha tatu, akafeli. Akarudia mtihani wewe ukiwa kidato cha nne wewe ukafaulu kwenda Kidato cha tano yeye akafeli. Hakukata tamaa amerudi mtihani mwaka jana na sasa anasubiri matokeo. Kwa hiyo wewe umehitimu kidato cha nne mwaka juzi 2015. Halafu unatuambia umehitimu kidato cha sita na upo chuo mwaka wa kwanza. Usitudanganye dada,
 
Mm nadhani anaogopa kukuweka wazi.
Kwasababu zifuatazo:
1.anaamini kuwa huko uliko unawezakuwa na mpenzi mwingine hivyo ni kama unamchora tu.
2.maisha yake yanategemea elimu hivyo hana vitrga uchumi na hajui wap aanzie kuweka mipango
3. Mapenzi ni hisia za ndani kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na hivyo lazima uangalie,
Je atakufanya kuwa na amani pindi utakapokuwa unamsubiri au utaweza kukaa miaka mingine tena ukisubilia amalize shule ili wewe na yy muishi pamoja

Jambo la mwisho ni kuwa angalia usawa wako wewe kama wewe kwake mchukulie kama option
 
Back
Top Bottom