Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,277
- 8,492
Ndio hiyo mkuu nakuambia usijaribu. Nikupe uzoefu wangu nilioshuhudia.Sawa mkuu nimekuelewa ila naotesha pemben mwa shamba tu siyo shamba zima
Kuna shamba lenye heka 2 lilikuwa na rutuba na chemichemi ya maji likistawisha mazao yote. Chemchemi ilikuwa haikaushi maji msimu wote.
Ukaingia ulimbukeni wa hiyo mikaritusi ikapandwa kuzunguka shamba lote kila baada ya hatua mbili.
Yalipokua yalikausha chemchemi mpaka leo haipo na eneo limekuwa kavu kwelikweli.
Ndio maana nasema hawa wataalamu wetu wengi vilaza na hawafai kwani hawaelezi watu hasara na faida zake.
Kwa ujumla hiyo miti haifai usipande. Narudia, usipande