Naomba ushauri kuhusu kupata cheti changu cha taaluma

Twasha

Senior Member
Oct 26, 2015
170
134
Hii ni historia ya ukweli kabisa.

Imetokea mtu umesoma diploma 1 na 2 ukamaliza mwaka 2018. Baadae ukafuatilia cheti unaambiwa jina lako halipo.

Kuuliza nini tatizo wakajibu matokeo yako ya diploma 1 hatuna,kuja kufuatilia kwa co-ordinator wakasema coursework 2 hukufanya za diploma 1.

Wakati huo sheria ya chuo huwezi kuendelea diploma 2 kama hukufaulu vizuri diploma 1 kwa maana kufika wastani wao uliopangwa.

Pia nilikuwa sidaiwi ada kwahiyo kipindi cha mitihani sikubughudhiwa.

Nina copy ya barua ya class Co-ordinator ambayo iliandikwa kipindi hocho nafuatilia cheti changu imeamuru nisaidiwe kupata hicho cheti.

Walichukua ile Original wakaniambia niende watanipigia. Mpaka sasa huu mwaka wa 3 sijapata cheti changu cha diploma.

Anejua pa kuanzia asinitupe mkono anisaidie.
Natanguliza shukrani za dhati wana JF.
 
Back
Top Bottom