Naomba ushauri kuhusu kujifunza Gari ya Manual kwa Msichana

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
258
566
Mimi ni msichana nina umri wa miaka 23. Nimemaliza chuo nikaona ngoja nisomee udereva driving school moja hivi hapa Dar. Sasa hapo wanafunza manual tu.

Mpaka sasa nina week moja, tushafundishwa gia ya kwanza ya pili na ya tatu na reverse (gia ya kurudi nyuma).

Kwa ujumla naendelea vizuri kwa kaisi chake lakini nina hofu sana mpaka gari inazima kuna muda uwanjani.

Mwalimu kaniambia nina uwezo wa kufaulu vizuri ila sijiamini na nina hofu sana.

Nilikua ushauri wenu: hivi nitakuja kuwa dereva mzuri kweli? Baada ya mwezi kuisha?

Nifanyeje nisiwe na hofu? Na nijiamini.
 
Wengi mkitoka hapo, manual mnazisikia kwenye stori tu, kazania kujua mipaka ya gari, stability na udereva wa kujihami, zaidi ujue jinsi ya kutoa pesa ya kiwi.

Sioni ukiendesha manual baada ya hapo unless uajiriwe upande wa Sales/Marketing kwa hawa TCC, Serengeti na wafananao, wanaopewa zile Single cab kufanyia kazi.

Kila la kheri
 
Natoaje uoga jaman
Ukiendesha gari usiangalie gia lever,angalia mbele na kubadilisha gia ni rahisi na mara nyingi mnatumia no 2 kuendesha wakati wa kujifunza.
Gari Manual linakupa uzoefu wa kujua gear box inavyofanya kazi katika mchango wa kuongeza na kupunguza speed ya gari, na linakufanya ujue mambo ya muhimu wakati wa kuendesha gari.Ukija kuendesha automatic ni rahisi sana
 
Utakuja kuwa dereva mzuri sana.Usikate tamaa.Ni kawaida kuwa na hofu hapo mwanzo mwanzo.Halafu madereva wa kike ni wazuri kuliko madereva wa kiume.Madereva wa kike huwa wanaendesha gari vizuri sana na kwa kuzingatia sheria.
 
Back
Top Bottom