Naomba ushauri kuhusu kuachishwa kazi

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Messages
2,962
Points
2,000

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2017
2,962 2,000
Kuanzia siku ya kwanza tu kazini huwa unakuwa observed kuanzia matendo yako kazini, utendaji kazi wako na kauli zako, ndio maana huwa wanaweka probation (unapewa muda wa majaribio). huenda hujui walichokiona kwako na mara nyingi hawawezi kukuambiwa kwa undani walichokiona mpaka umpate mtu wa karibu sana na anayekupenda ndio anayeweza kukushauri fanya hivi, ishi namna hii na uwe unafanya kazi namna hii, vinginevyo utaambiwa tu huturudhishi.
 

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Messages
15,039
Points
2,000

Castr

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2014
15,039 2,000
Mimi sijasomea sheria ila nimesoma HR kama somo. Ni kwamba kwa kawaida unatakiwa uwepo mkataba wa kuonyesha kua wewe ni mfanyakazi ambaye upo chini ya uangalizi.

Mkataba huo unatakiwa uonyeshe muda wa uangalizi na malipo utakayopokea kipindi cha uangalizi. Mara nyingi malipo unayolipwa hua ni yale ambayo ungelipwa kama umeshakua mwajiriwa. Yaani mfano kwa levo yako ukiajiriwa unatakiwa ulipwe sh 300 basi na wakati wa uangalizi utalipwa sh 300 hiyo hiyo.

Kama walikua wakikulipa mshahara sioni kama una madai zaidi.

Kama hauna mkataba wa kwenye karatasi wala siyo ishu kubwa sana kwa sababu katika aina za mikataba kuna mkataba wa mdomo. Wewe siyo chizi uingie ofisini miezi miwili na wao siyo machizi wamuone mtu anaingia ofisini miezi miwili huku hawamjui.

So lazima kuna namna mlikubaliana. Na namna yenu ilikua ya mdomo.

Ukienda kwa mwanasheria au HR wa hapo anaweza akakupa muongozo juu ya swala lako. Ingawa kama ulikua ukilipwa mshahara naona hakuna la zaidi.
 

bora uhai

Member
Joined
Jan 15, 2019
Messages
44
Points
125

bora uhai

Member
Joined Jan 15, 2019
44 125
Queen Priya,

Twende taratibu kuna vitu havipo sawa hapo nitasema kwanini na vifungu vya kisheria

Code of good practice 2007 kifungu cha 10 inasema hivi wafanyakazi wote waliokwenye majaribio vipimo vya kuwapima lazima viwekwe wazi hapo wakimaanisha KPI yani key performance indicator kwa mfano unapoajiriwa kama sales unapimwa kwa yafuatayo 1. kufikia target ya kila mwezi 2. kuleta wateja wapya 3. kuwatunza wateja wazamani na hiyo KPI huwa unasainishwa kabla tu hujaaanza kazi sasa basi pale unaposhindwa kipindi cha majaribio cha miezi 6 ukishindwa kutimiza izo KPI boss lazima akupe progress improvment report ili uweze kufikia zile KPI mlizokubaliana

Pia katika Kifungu hichohicho cha 10 kifungu kidogo cha 7 yani 10(7) kinasema hivi kama muajiri hajarizishwa na utendaji wa kazi anatakiwa kumpa nafasi mfanyakazi ya kujitathimini na kujitetea kwanin anafanya kazi chini cha kiwango

kama hayakufanyika hayo yote una haki ya kwenda CMA kufungua shitaka lako maana icho kifungu wamekiuka yani wamekiuka CODE OF GOOD PRACTICE 2007 10(7)

Pia kosa jingine lililofanyika wamekufanyisha kazi bila mkataba ili ni kosa maana hata muda wa majaribio unakuwepo ndani ya mkataba sasa kwa kufanya hivi wamekiuka kitu kifuatacho

NSSF ACT 1997 kifungu cha 11 kinasema hivi mfanyakzi asajiliwe baada ya mwezi mmoja kuajiriwa wasipofanya hivyo kuna adhabu ya asilimia 5% ya michango hii inapatikana kifungu cha 14 katika NSSF ACT hivyo kwa kufanya hivyo hiyo kampuni ilikwepa kulipa michago yako NSSF kwa muda wa miezi 3 na ni kosa kisheria

Cha mwisho kama waliamua kukufanyia termination pia ilitakiwa taarifa ya siku 28 maana tayari ilishavuka mwezi,
Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 Kifungu cha 41 kinachomuhitaji muajiri kutoa taarifa ikieleza sababu za kukuachisha na tarehe utakayokuwa utambuliki kama mfanyakazi

Kama hakufanya hivyo maana yake kosa la 3 wamekiuka Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 Kifungu cha 41

Wahi zako tu CMA kabla siku 30 hazijavuka kajaze form ya kufungua shauri kwenye unfair termination shauri la kwanza shauri la pili wafungulie wamekwepa michango ya NSSF hapo lazima muajiri akili imkae sawa mtayajenga tu.
 

bora uhai

Member
Joined
Jan 15, 2019
Messages
44
Points
125

bora uhai

Member
Joined Jan 15, 2019
44 125
ntinanigwamvuyekule,

Sheria za Kazi ukiruka kipengele huwa inaleta utata hivi unajua kama mfanyakazi ukimtuhumu ni mwizi mahakama ikasibitisha sio mwizi na akirudi kazini kama umuhitaji unatakiwa kumlipa fidia ya miezi 12 na kipindi hicho kesi inaendelea mshahara wake unatakiwa umlipe kama kawaida.

Suala lililokiukwa na kutofuata utaratibu wa kazi kama sheria inavyotaka basi.
 

bora uhai

Member
Joined
Jan 15, 2019
Messages
44
Points
125

bora uhai

Member
Joined Jan 15, 2019
44 125
Queen Priya,

Kwanza alikuwa anakulipa bei gani kwa mwezi ukute pia kakiuka minimum wage order ya 2013 kwa hotel ilo nalo ni kosa jipya na jingine kabisa.

Inasema Medium Hotel ni 150,000 na restaurant Bar and Guest 130,000 kwa mwezi kama alikuwa hafanyi hivyo pia ni kosa kisheria na kosa ni Under Minimum Wage. Hapo ukiwa tu na salary slip inawezekana au kama atakwepa hilo omba tume waletewe payroll kama sehemu ya kujiridhisha kwamba kampuni ilikuwa inalipa kima cha chini cha mshahara.
 

Chikwale

Member
Joined
Aug 2, 2019
Messages
29
Points
75

Chikwale

Member
Joined Aug 2, 2019
29 75
Kipindi cha probation ni kipindi cha unafiki, yaani inabidi uwe mfanyakazi bora kubembeleza ajira. Kama ni underperformance ndio basi tena.
Lakin na sisi tuwe fair. Inakuwaje unashindwa kuonyesha uwezo ndan ya miez miwili.!!??
Hizi kazi kuzipata watu wana sota sana. Sasa inakuwaje unapata kazi then ndan ya miez miwili unaonyesha weekness kubwa kiasi cha uongozi kuamua kusitisha mkataba wako. Ni aibu kwa kweli. Mungu amekufungulia mlango then ww umeshindwa kuishikilia hiyo nafasi.
 

AsajizzleDaGreat

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2018
Messages
1,190
Points
2,000

AsajizzleDaGreat

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2018
1,190 2,000
Lakin na sisi tuwe fair. Inakuwaje unashindwa kuonyesha uwezo ndan ya miez miwili.!!??
Hizi kazi kuzipata watu wana sota sana. Sasa inakuwaje unapata kazi then ndan ya miez miwili unaonyesha weekness kubwa kiasi cha uongozi kuamua kusitisha mkataba wako. Ni aibu kwa kweli. Mungu amekufungulia mlango then ww umeshindwa kuishikilia hiyo nafasi.
Usilolijua ni kama usiku wa giza
 

kifinga

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2011
Messages
3,186
Points
2,000

kifinga

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2011
3,186 2,000
Kipindi cha probation ni kipindi cha unafiki, yaani inabidi uwe mfanyakazi bora kubembeleza ajira. Kama ni underperformance ndio basi tena.
Sio probation tu muda wote wa ajira unatakiwa uwe mtu wa kujishusha na bosi always huwa hakosei
 

Njopino

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2014
Messages
2,939
Points
2,000

Njopino

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2014
2,939 2,000
Queen Priya, Kwanza napenda nikupe pole kwa changamoto iliyokukuta, lakini utambua njia moja ikifungwa, kuna njia nyingine inafunguliwa, kuwa na imani.

Tukirudi kwenye mada:

Kwa haraka haraka ni kwamba huna uthibitisho kuwa ni mfanyakazi wa hiyo kampuni, ni kama ulikuwa unajitolea ili uwashawishi wakupe kandarasi bahati mbaya umeshindwa kuwashawishi.

Binafsi sioni kama huna haki hapo maana hata waliopo kwenye uangalizi wanakwa na mkataba ambao unaelezea makubaliano ya muda wa kuwa kwenye uangalizi na vipengele vyake.
Well said mkuu, kuwa chini ya uangalizi (Probation period) haimaanishi kuwa usiwe na mkataba, unakuwa na mkataba ila kwenye terms zake ndio utaonyesha kipindi cha uangalizi mfano miezi mitatu, sita, mwaka n.k
Four years back, nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na taasisi fulani, ndani ya mkataba ulionyesha miezi mitatu ya uwangalizi, sasa nina mkataba wa miaka kadhaa ambao unaonesha mwaka mmoja wa uwangalizi ingawa nimeumaliza huo uwangalizi tokea 2017.
 

Forum statistics

Threads 1,358,436
Members 519,294
Posts 33,168,245
Top