Naomba ushauri kuhusu kazi za viwandani

pet geo pet

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
461
644
Wakuu kama kichwa kinavojieleza,mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu kinachotambulika kiserikali katika fani ya uwalimu nikijikita na masomo ya sanaa.

Nimejaribu kuomba kazi katika fani yangu lakini hali sio nzuri kwani sijapata hata shule moja.

Nimeona nibadili njia kwa kuanza kuomba kazi viwandani ingawa fani yangu ni mwalimu.

Naombeni ushauri ni kazi gani zinazonifaa kiwandani kwa mimi mwalimu ili hata nikienda kuonana na muajiri(H.R.M)niweze kumuelezea.

Nakaribisha ushauri wako hasa watu wanaofanya kazi kiwandani ili niweze kupata pakuanzia kwani yote hii inatokana na kukosa mtaji wa kufanyia biashara ili kuepukana na kuuza nguvu kazi.

Asanteni na karibuni wakuu.
 
Kiwandani hakuna mwanafunzi , hivyo utafanya kazi zinazo husiana na kiwandani, mf kubeba marobota na kuendesha mashine.Asante na mungu akuongoze.
 
Kiwandani hakuna mwanafunzi , hivyo utafanya kazi zinazo husiana na kiwandani, mf kubeba marobota na kuendesha mashine.Asante na mungu akuongoze.
Asante kaka,lakin hamna kazi ambayo nitafanya isioweza nimumiza yaan kushirikisha akir sana hafu nguvu kidogo
 
Nishauri niende kiwanda gani?kwani hapa nmepanga kwenda kiwanda cha backresa,pepsi,bia,mabati,na vingne vingi
 
Nakushauri rudi mikoani unaweza pata pakujishikiza kwa fani yako,kama unataka ubaki mjini,weka cheti chini angalia kazi unazoweza kufanya kwa kutumia nguvu nyingi akili kidogo,mfano kubeba mizigo,kukoroga zege n.k
 
Mpaka nakuonea huruma .
Dunia haiko fair, na wewe usiifanyie fair.
Nenda mkoani kashinde shamba kutwakutwa utapata mtaji au pesa za hongo ili uhonge upate kazi kwenye private organization . Huko mtu wa education utalipwa si chini ya million moja kwa mwezi + other syringe benefits.
Fight ukishindwa sana Januari tar 15 nishtue nikuunge mkono ktk juhudi zako
 
Ushauri wako mkuu sio kbs
 
Nakushauri rudi mikoani unaweza pata pakujishikiza kwa fani yako,kama unataka ubaki mjini,weka cheti chini angalia kazi unazoweza kufanya kwa kutumia nguvu nyingi akili kidogo,mfano kubeba mizigo,kukoroga zege n.k
Asante br.mawazo yapo vzr
 
Back
Top Bottom