Naomba ushauri kuhusu hili tatizo la pikipiki yangu ya TVS

leadermoe

R I P
Feb 15, 2017
1,392
4,573
Wakuu amani kwenu,
(nimeulizwa swali na mdau, kwa kuwa sijui mambo ya pikipiki nimewaailisha kwenu anaomba msaada wa mawazo)

Nisipoteze muda nimepata changamoto kidogo kwenye hizi piki piki za Tvs 150. Nilimchukulia dogo mwaka jana mwezi wa 3. Mpaka sasa imetembea km 12000.

Shida ni kwamba alipata ajali ya kugonga daladala akiwa speed 60kph, alichomekewa. Hakuumia na pikipiki ilionyesha matatizo kidogo so akarekebishiwa wakamalizana. Lakini baada ya kama wiki hivi nilitoka nayo nikagundua Stelling imepinda, kwenda kwa mafundi wakadai chuma kinaitwa T ndio kimepinda na wala hakifai kunyoshwa.(hapa nilishangaa kidogo maana najua T ni ngumu sana ingawa imetengenezwa kwa udongo, na ajali haikuwa kubwa maana hakuumia hata kuchubuka)

Baada ya kama mwezi hivi engine imepungua nguvu hasa mlimani na mwanzo kuna sehemu nilikuwa napita na gia namba 3 sasa hivi nalazimika kutumia 1 au 2 ya mafuta mengi. Swali langu kwa wataalam shida inaweza kuwa nini kwa engine na Stelling (hapa siamini kama T imepinda maana ajali haikuwa kubwa)

Nb: Imefanyiwa service pamoja na kubadili oil (Total) siku 5 zilizopita ila bado nguvu haijarudi. Nisaidieni wakuu maana naona kama mafundi wanakula hela tu jibu la maana hakuna.
 
Pole sana hilo tatizo la kuishiwa nguvu hata mimi linaisumbua pikipiki yangu tvs 125 clutch plates na ring piston nilibadili lakini bado pikipiki haina nguvu.

Sasa sijui tatizo ni nini!
 
Ngoja wataalamu zaidi waje bila shaka nyote mtapata ufumbuzi wa matatizo yenu.

JamiiForums kamwe haijawahi kushindwa.
 
Ingia makubaliano na huyo fundi aliyekwambia T imepinda. Endapo tatizo litaendelea hakuna kumlipa.
 
Back
Top Bottom