Naomba ushauri kuhusu gari ya kununua kwa mara ya kwanza

Habarini za jioni wadau. Nimejikusanya nimepata kama mil 12 - 14. Malengo yangu nahitaji kununua gari kwa ajiri ya shughuli za kawaida kama kwenda na kurudi kazini, kwenda na familia ibadani, sokoni, kwenda kuwatembelea wazazi mikoani nk.

Hivyo naombeni wataalamu mnipe ushauri wa ni gari gani itanifaa kwa kuanzia kulingana na bajeti hiyo kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.

1. Kumbuka ni gari yangu ya kwanza.
2. Muonekano wa gari ni kipaumbele cha kwanza.
3. IST sio chaguo langu kabisa
4. Ulaji wa mafuta ni suala la pili kuzingatia baada ya mwonekano/shape

Asanteni sana na karibuni kwa mawazo.
Mkuuu hutaki IST alafu unaowaomba ushauri wote wantumia hiyo IST.. subiri kejeli na matusi
 
1645726042658.png
Kuna jamaa kanitumia hii gari inbox kesem naweza kuifikisha Dar mpaka registration kwa mil 14-15.
Make:SUBARU
Model:FORESTER - SG5
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2005
 
Hapo chukua gari yoyote ndogo ila hakikisha cc iwe chini ya 1500. napendelea Toyota naonaga mafundi wake ni weng na spea sio shida. usinunue demio cjui Mazda, passo, cami/terios, nissan xtrail hizo ni mimba
Passo,cami ni toyota mkuu,mimba zake zinakujaje mkuu tuelekezane tusiingie mikenge
 
Sisi, ( EAPGS )

Hatukushauri sana kuhusiana na subaru, hii ni kwa sababu ya kuzingatia angalizo ambalo umelitoa kwamba, ndio garibya kwanza, hivyo experience ni kipaumbele.

Kwa budget yako, gari ambazo zingekufaa sana ,

  • Corolla Rumion
  • Corolla Spacio
- Premio ( F )

Optional :

- Crown Athlete

Hizo ndizo tungeweza kupendekeza
Kulingana na budget yako
 
Crown nasikia nikishainunua nijenge na kisima cha mafuta kabisa nyumbani
 
Premio kwa 14M labda iwe ya mkononi si F,G wala X.

Jaribu Allex,Runx,Spacio,Raum,Probox,Vits,Sienta,Passo and the likes.
 
Hamna Premio wala Subaru humo
Japo umeonesha kutoitaka lakini ist ingekufaa ni gari nzuri sana ina sifa zote ni ngumu, spea kibao, matumiz mazuri ya wese, dizaini yake bado si mbaya. ila agiza nje usinunue hiz za watu mikononi.
 
Habarini za jioni wadau. Nimejikusanya nimepata kama mil 12 - 14. Malengo yangu nahitaji kununua gari kwa ajiri ya shughuli za kawaida kama kwenda na kurudi kazini, kwenda na familia ibadani, sokoni, kwenda kuwatembelea wazazi mikoani nk.

Hivyo naombeni wataalamu mnipe ushauri wa ni gari gani itanifaa kwa kuanzia kulingana na bajeti hiyo kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.

1. Kumbuka ni gari yangu ya kwanza.
2. Muonekano wa gari ni kipaumbele cha kwanza.
3. IST sio chaguo langu kabisa
4. Ulaji wa mafuta ni suala la pili kuzingatia baada ya mwonekano/shape

Asanteni sana na karibuni kwa mawazo.
chukua bmw series 1 au bmw x1

mimi.jpeg
 
Back
Top Bottom