Naomba ushauri kuhusu flat TV

Naomba ushauri kabla sijaingizwa mjini mimi sio mzoefu wa hizi falt TV.

Ipo hivi kuna mfanyakazi mwenzangu hapa ni mzanzibari anafanya kazi bara. Nilimwambia nahitaji kununua tv ya bei ndogo ila nimwagize tokea zanzibar kwani huko bei afadhari akanambia hata yeye alichukulia huko kwao.

Akanishauri kama tv nichukue mtumba kwani hata yeye ndo aliyonayo na ni nch 43 kampuni ya toshiba. Basi nkamwambia aniuzie ya kwake akaanzia 500k tukavutana mpaka 400k nkamlipa nusu na nkaomba nikaione kwake. Baada ya kuiona nilishangaa kidogo kuona ipo tofauti kidogo na hizi nyingine za mchina.

kwani niliona kama ina nyama kubwa ya plastic yaan kioo kinaonekana kidogo ila likaver la juu yaan plastic inaonekana imechukua nafas kubwa sana. Sikuweza kumuuliza maana alikuwa tayari kashaisifia sana kuwa haichemshi wala nn inaweza piga mzigo siku mbili mfululizo.

sasa wadau naomba mnishauri kwa hili vipi hii tv inafaa kwa matumizi ya nyumbani au imekaa kilocal sana. Na je kwa bei yake hio nimepigwa au kanifanyia fair.

kwa wajuzi naomba mnisaidie ubaya na uzuri wa hizi tv flat za mtumba hasa kampuni ya TOSHIBA.

Nawasilisha.
Kwa ivo jamaa yangu huniamini hadi umekuja kuuliza huku?si uliniuliza kila kitu nikakujibu?hatuaminiani sheikh wangu!?
 
Sasa stat x inch 32 piruu ni 350k mwaka 2017
Chup mtumba
Nguo mtumba
Mke mtumba
Mpaka na TV tena duuu
 
Back
Top Bottom