Naomba ushauri kuhusu dini

Napenda niende moja moja kwenye nukta muhimu ambayo ningependa kuiongelea kulingana na mada ya Uzi huu

Kwanza mleta Uzi ukimsoma vizuri namna anavoelezea kisa chake ni kana yuatafuta legitimacy (uhalali) wa kuwa mkristo

Unatafuta uhalali kwa nani hapa??? Huyo mwenye mandate ya kukuambia upo sahihi kufanya hivo then ujihisi huru from within??

According to my iman...swala la ibada ni mja na mola wake....tuache kutafuta legitimacy na kufanya campaign kwenye maswala muhimu kama haya..in the end it all fall on you


Kilichokugharimu ni kuwa huijui iman yako hizo nyingine ni drama coz kama since form 1 yuasoma kwa waroma huo uislam(imani yako) umejifunza muda gan wakati since form 1 umeanza shiriki ibada za waroma....utasema ulisoma madrasa.. Madrasa uliyosoma ya alif be te the ndio na al fatiha na sura nyingine za juzuu amma ndio una claim kuwa umeusoma uislam???

Ushauri

1. Wazazi somesheni wenu Leo upo nae kssho anaenda mikoa ya watu, Leo upo nae kesho haupo...acha aje achukue uamuzi wa kufanya atakaloliona ni sawa hali yakuwa wewe ushatimiza wajibu wako kama mzazi wa kumsomesha iman yake na academic pia

2.kama ambavyo ukiwa na ugonjwa unaulizia kwa watu daktari mzuri anapatikana wapi, ukitaka kujenga unatafuta fundi mzuri ni nani, ukitaka kuoa unatafuta binti mzuri wa tabia na sura yuko wapi, mwanasheria mzuri nan, shule nzuri ipi, bus gani ni zuri kwa safari vivo hivyo kwenye maswala ya imani yako ukiwa una jambo tafuta msomi mzuri ni nani, sheikh mzuri ni nani, mchungaji mzuri ni nani, padree mzuri ni nani...sio kwingine kote unatafuta mzuri wa kumpelekea haja yako ni nani afu kwenye maswala ya imani yako unauliza yeyote kila unaemuona bila kujua elimu yake, daraja yake...aya humu JF unawajua wote watakao comment kuhusia na na imani yako level zao za elimu katika imani yako???

Tuache kuzifanya imani zetu kama something subsdiary
 
Mkuu!Mimi naamini katika UZIMA WA MILELE kama alivyo ueleza Yesu mwenyewe:-

Yohana 17:3

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.




Lakini sarakasi nyingine sizihitaji hata.
Uzima wa milele, Wakati tunaona makaburi ya Wakristo yamejaa, sawa tu na wasiyo Wakristo, unachekesha wewe.
Hebu nenda Mburahati ukaone, angalau mngedanya, kuwa wakristo mtafufuliwa baada ya kufa, maana kufa lazima ufe hivyo hakuna uzima wa milele.
.
 
Ukifuatilia historia yako...
Umezaliwa kwenye Familia ya Kiislam na kupata ile basic knowledge ya kusoma ( kama Nursery) ambapo kule ni mambo basic na pale ambapo ungetakiwa Usome Quran na kuelewa kilicho andikwa na kilichokusudiwa namaanishwa kuanzia umri wa miaka 13 hivi (ukiwa matured) ukawa umeenda kwenye Shule ya Kikatoliki
Ulipo kwenda sekondary ya wakatoliki, hapo ndio uliweza kupata Mafundisho ya Dini (Kikatoliki) ambapo ukawa ndio mwanzo wako wa kupata mafundisho ya Dini kwa undani na kuelewa kwani pale umekua (matured). Nimeandika hivyo ili ujue kuwa, hakuna kitu cha ajabu sana hapo.
Kwa mtu mwenye hekima nilitegemea uulize kuwa; nimepata mafundisho ya kikatoliki shuleni na natamani Kusoma Elimu ya Kiislam tofauti na ile ya Chekechea ya Kufundishwa/ku kremu kusoma na kuandika; namaanisha mwanafunzi wa Chekechea hawezi kujisifia eti na yeye ameelimika kisa tu amejua kusoma na kuandika
Kwa kufanya hivyo ungeweza kusoma indetail sio ile ya kukremu hata mimi nilisoma hiyo pia ila baadae nikajiona nilipata pengine kama 6% ya nilichotakiwa kujua; baada ya hapo ungeweza kufanya uamuzi sahihi
KWA ELIMU YAKO YA UISLAM LEVO YA CHEKECHEA USIJIWEKE KWENYE KUNDI LA WATU WANAOJUA UISLAM; SOMA!
Nimekuelewa ila sijasoma shule za katoliki nimekaa hostel tu za wakatoliki ambazo hazitoi mafundisho ya dini labda uwe unaenda kanisani kwao na ukumbuke wakat naenda hiyo hostel tayar nilishabadili jina kuwa la kikristo na kusema baba yangu ni mkristo!
Kweli elimu ya chekechea ndiyo niliyonayo kwenye dini zote mbili
 
Kwanza nakupa pole sana,umesema umesoma madrasa na unaijua Dini ya kiislamu?kwa mtu anayeijua Dini ya Kiislam hawezi kuja kuomba msaada hapa jukwaani,naamini wewe ungekuwa msaada kwa wengine kuwaingiza kwenye Uisilamu.

Kama kweli ulichokifanya unakijua na malipo yako utakuwa unayajua baada ya kufa kaburini na siku ya kiaama.Kibaya zaidi unadiriki hata kuwapotosha watoto zako unawaingiza kwenye Ukafiri wakati wazazi wako wamekupa kheri zote? Nimejaribu kuandika lakini nashindwa kuuendelea,angalia wanaokupotosha wanakwambia Dini zote ni sawa,wapi na wapi? Nenda kwa wazazi wako ukawaambie kuhusu msimamo wako nazani watakusaidia zaidi
Waislamu mwenzenu akibadili dini kwenda ukristo mna kasirika sana utafikiri mna hati miliki ya maisha ya kila mtu
 
Hata mimi nimeliona hili, angalia comment zake kwa wasio kua waislam anazipokea vyema ila ushauri unaotoka kwa waislam anautolea maneno yasiyofaa.
Ikiwa amesema kua anaujua uislamu vyema ili swala angepeleka kwa wenye elimu zaidi viongozi wake wa kiimani, au angeswali hata rakaa mbili kumwomba Allah amuonesha njia iliyo sahihi. Mtume muhamad s.a.w alituusia kuiiomba dua hii yaa muqalib, ....... Ewe mwenyezi Mungu zithibitishe nyoyo zetu ktk dini yetu ya haki. Mbali zaidi aya za mwenyezi Mungu zinatuonesha pia kumuomba Allah asizipotoshe nafsi zetu baada ya kuamini.
Inaumiza kuona muislam tena uliezaliwa ukisema maneno hayo.
Nakushauri katafute elimu zaidi.
Hakika dini ya Allah ni uislamu na kamwe sitojutia kuwa muislam. Allah aniongoze mimi na wewe ktk haqqi mpka mwisho wetu na siku ya kiyama atujalie tuwe miongoni mwa wale watakao pokea kitabu chake kwa mkono wa kulia. Amiin
Ninachopinga mimi ni kutishwa kupigwa mkwara kuhusu ukafiri sijui nini! Nimekuja kuomba ushauri wala sina shari na mtu sasa kwanini unijie na hasira? Lakini coment zote nazielewa na nachanganya na zangu! Aman!!
 


Mzungumzaji mbona tayari ulishabadili dini kitambo unatafuta ushauri gani kaka wa mie???

Kulingana na islamic theology, Kitendo tu cha wewe kwenda kuombea, kuwapeleka wanao Kanisani na kuitakidi kwako unajisikia amani kanisani kuliko kwingine WEWE TAYARI NI MKIRISTO.....


Wataka wajumvi ILA KWA KADRI NINAVYOJUA IMANI ya KIISLAM WEWE TAYARI ULISHATOKA KITAMBO NA WALA SIYO MUISLAM
Duh! Sikua najua hilo
 
Rafiki upo SEHEMU sahihi,ukristo haitoshi tu Bali taka kuwa ndani ya yesu kristo mwenyewe,aingie ndani yako atawale maisha yako.

Kinacho weza kukuokowa na hukumu ya Mungu ya milele kwenye ziwa la moto ni yesu kristo pekee ,si zehebu au mapokeo.

Historian Iko hivi

Ukristo=umepitia Kwa uzao wa Sara, mke mkubwa

Uislam= ni Kwa yule mjakazi bimdogo

Ko Mungu alimuahidi Ibrahim agano lake ni Kwa uzao wa bimkubwa, mpaka akazaliwa yesu.
Ahadi ya Mungu ikatimia.

Ko hapo ni sawa na kusema umetoka ule upande wa bimdogo ukaja upande wa bimkubwa .
Amen!
 
Kwanza nakupa pole sana,umesema umesoma madrasa na unaijua Dini ya kiislamu?kwa mtu anayeijua Dini ya Kiislam hawezi kuja kuomba msaada hapa jukwaani,naamini wewe ungekuwa msaada kwa wengine kuwaingiza kwenye Uisilamu.

Kama kweli ulichokifanya unakijua na malipo yako utakuwa unayajua baada ya kufa kaburini na siku ya kiaama.Kibaya zaidi unadiriki hata kuwapotosha watoto zako unawaingiza kwenye Ukafiri wakati wazazi wako wamekupa kheri zote? Nimejaribu kuandika lakini nashindwa kuuendelea,angalia wanaokupotosha wanakwambia Dini zote ni sawa,wapi na wapi? Nenda kwa wazazi wako ukawaambie kuhusu msimamo wako nazani watakusaidia zaidi
Haha muache aje kwa Yesu.

huenda hajapendezwa na ahadi ya mabikra
 
Siyo mimi,hilo jina alilowaita ni yule aliyewaumba mumuabudie,nyie mkaenda kuwaabudu wasiyostahili kuabudiwa, ole wenu siku yaja,Ebu jiulize shetani alifukuzwa peponi sababu tu,ya kukataa kumsujudia Adamu,je wewe unayekataa kumuabudu mwenyezi Mungu itakuwaje?
Allah alitaka kiumbe mwingine asujudiwe ?

ngoja nikuitie Kiranga upambane nae hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom