Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Mkuu Tripo9
Endapo kama unatumia satelite dish inayotumia ving'amuzi vya Free to Air(FTA channel) kama Media com au strong vp matangazo ya mpira pale siwezi kupata free au kama ni ya kulipia naweza kupata kwa kiasi gani??

Kwa kweli hapa sina utaalamu. Lakini mambo ya free to air. yaani neno free, neno promotion neno lipia upate bure ni maneno sitakagi wala kuyasikia kwa sababu ni uzushi wa kijinga. Na wala usiwasikilize wajinga wa startimes au ting au wajinga wowote eti wataonyesha mpira wa majuu. Ni upuuzi mtupu. Jipige weka dstv simamia biashara yako hii waweza toka.

Kuna kitu nasikia sijui Arab sat sijui nini nasikia hii kitu ni nzuri na cheap pia. Ila gharama za mwanzo za kufungiwa ni za juu sana.

Unalipa kama laki tisa, wanakufungia upuuzi woooote halafu baada ya hapo kila mwaka, narudia tena kila mwaka unakua unalipa kama dolla 40 na unalipiA KWENYE MTANDAO hiyo pesa.

Ila hii kitu nimesikia tu, kuna ndugu yangu anajishughulisha na dili hizi A-town, ila kokote anafunga. Mimi hii huduma siiitumii

Mimi ntumia tu dstv kwa matumizi yangu binafsi
Thanx
 
Nakushauri ufungue bar ambapo pia utakuwa unaonyesha mpira ligi mbalimbali, namaanisha biashara yako kubwa iwe ni hiyo ya bar na mpira iwe ni njia tu ya kuwavutia wateja, lakini hakikisha kila anayeingia hapo ananunua kinywaji ikiwezekana kwa kuwauzia coupons mlangoni wakati wa kuingia ambazo zitatumika kulipia vinywaji.

Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu
 
Shukran mkuu Tripo9 kwa kunifungua macho zaid . Unaweza kunipm contact za jamaa yako wa A-town??
 
Wazo zuri sana kwa mtoa mada. Je, kwa mazingira ya huku vijijini inakuwaje gharama yake maana huku hata umeme hakuna. Nipo Tabora.
 
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa! Ni wazo tu mkuu.

Mimi nadhani kwenye baa hapanogi maana makelele ya wanywaji na pia sana sana pale wanaokwenda ni wanywaji lakini mkuu huyu akitenga sehemu decent watakaohudhuria ni wengi kuliko kwenye baa.
 
Mkuu kweli we ni borngain! Lakini embu niambue huu usemi huwa una maana gani kwenye biashara? don't put all your eggs in one basket? Au diversification kwenye biashara lengo lake huwa ni nini?
Mimi nadhani kwenye baa hapanogi maana makelele ya wanywaji na pia sana sana pale wanaokwenda ni wanywaji lakini mkuu huyu akitenga sehemu decent watakaohudhuria ni wengi kuliko kwenye baa
 
Bado naendelea kufuatilia maon wadau maana nimeshaanza kukarabati eneo nimefikiri na kufungua na library ya kukodisha mikanda maana kuna mtoa maoni mmoja alinishauri pia nionyeshe picha za Mkandala Lufufufu watakaokuja kuona wanaweza kuvutiwa na kukodisha kwenda kuiona nyumbani...
 
Kumbuka kama unataka kuonyesha DSTV kwa uma kama unavyotaka kufanya wewe, hauwezi kulipia bei hii ya kawaida sawa na ambayo unalipia ukiweka private nyumbani kwako.
Inabidi ulipie commercial package kutoka DSTV, hii ni gharama kubwa zaidi. Cheki Pubs & Clubs - DStv Commercial
 
Unatakiwa utoe taarifa kwa details sababu wengine hatuna uzoefu lakini tunataka kujua huenda tukawa wateja wako
 
nimeona kigoma inalipa sana yani unaweza pata pesa ya kulipia malipo ya mwezi ya dstv ndani ya mechi moja, cjui kwa mwanza..
 
Ina lipa makali tena unaweza boresha eneo.lako ukawa una toa uduma nzuri nzuri hata kiingilia kikawa juu zaidi na ukapata faida nzuri tu
 
Inategemea huko eneo gani mkuu,,,sio unaishi kule kwenye majengo ya ukweeeeeeli ambayo kila mtu ana kauwezo then utegemee utapata watu, fanya research kwanza mkuu, wangapi wapenzi wa mechi? Then hope utafanikiwa..wengi hufanikiwa.
 
Kama ukumbi njema ila sio cable unasambaza mtaani watakufunga Dstv uwa wanapita kukagua mikoani, pale Tabora kuna muhindi tajiri alinyea debe sana na faini kubwa tu.
 
Kama ukumbi njema ila sio cable unasambaza mtaani watakufunga Dstv uwa wanapita kukagua mikoani,pale Tabora kuna muhindi tajiri alinyea debe sana na faini kubwa tu.

Huyo Muhindi hadi sasa bado anatoa huduma ya kidijitali. Tunaona Channels zaidi ya 60 kwa 10,000 Tshs kila mwezi zikiwemo Stations za DSTV, Abudabi Sport na station za vingamuzi vingine.
 
Back
Top Bottom