Naomba ushauri kuhusu biashara ya kuonyesha mpira

panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Wadau nilikuwa na wazo la kununua Projector na satelite dish ili kuonyesha mipira ya ulaya ninaeneo langu kubwa linaweza kuingiza watu mia mbili naomben msaada wa kujua gharama ya projector na satelite dish nianze hii biashara kwa yoyote mwenye uzoefu na biashara hii anisaidie kunipa ushauri zaid ni vitu gan vya kuongeza hapo.

Nawatakia mafanikio mema wote ndan ya mwaka huu Mungu awe pamoja nanyi..nasubir msaada wa mawazo yenu

================================================

Kwa wenye mabanda bei za vifurushi ni kubwa sana hasa Dstv ili upate ligi ya uingereza epl hapa inakulazimu ununue kifurushi kuanzia hiki cha dstv compact plus 122500(laki moja na ishirini na mbili mia tano) hapo una kimoja kama una Tv mbili inakubidi uwe na decoder mbili na zote uzilipie ile huduma ya kuunganisha tv mbili kwa decoder moja na ionyeshe mechi tofauti wanadai ilitolewa anaejua mautundu tusaidiane.

Binafsi baada ya kuona hizo gharama hiyo ya kifurushi bado hujalipa kodi na umeme na kibaya eneo nilipoweka hii biashara haijachangamka kivile NILIFANYA HILI KUJIPUNGUZIA GHARAMA.

Nikanunua sattellite dish lile kubwa na receiver ili nipate chanell za bure kweli sport 24 Hd inarusha karibu mechi zote inanisaidia japo hapa karibuni imesumbua sana hii sport 24 Hd signal zilikuwa chini sana now ipo vizuri ila changamoto yake kuu NIONAVYO HII INAFAA KWA MATUMIZI YA NYUMBANI SIO KIBIASHARA.

SOLUTION NYINGINE KUNA HAWA WANAWEKA channell za mpira katika azam au star times hawa sijawajaribu kama yupo anaezitumia tusaidiane.

ILA NI BIASHARA NZURI UKIWA NA LOCATION NZURI INGAWA MAUMIVU VIFURUSHI wageni karibuni katika hii bussiness leteni na maswali.

Mliopo humu na mna mabanda ya mpira tushaurine tufanye nini tuendeshe kifaida zaidi.

Je, Bien Sport au super Sport hizo zinazowekwa kwenye decoder zinadumu kwa muda gani?
Jamani mimi naonesha mpila toka 2011 hii biashara ngumu sana ila

1. Inaitaji uwe na eneo lako kama mimi itapunguza cost gharama zipo juu lakini ili upate faida unatakiwa ukae mweyewe

2. Usifanye malipo mwisho wa mwezi lipa kila mechi kidogokidogo kadili unavyoingiza 3 fungua decoda ya biashara toka dstv utapewa dicoda 3 kwa malipo ya mwezi 294000 utakua unaonesha game

3. Kwa wakati mmoja mtajisumbua bure kufunga hayo madish mimi nimefuatwa mara nyingi sana lakini sitaki kwanza wenye haki ya kurusha premium league ni DSTV ukionekana ama kwa bahati mbaya mtu kakuchoma imekula kwako utakwenda mahakamani hizo decoda za mipango tu hazina muda huwa zinafungwa katikati ya game
 
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Messages
2,282
Likes
205
Points
160
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2009
2,282 205 160
Dstv kila kitu ukilipia kwa hapa bongo dar es salaam ni kama laki 2 na elf 80 kama sijasahau, hapo unakua pia umelipia kuona machannel yote ya mipira na kila kitu dish na fundi wa kukuwekea dishi na pia king'amuzi na nini na nini na kila kitu.

Kila mwezi gharama ni shs 129,000 kuona machannel yote yenye mupira.
Uonyeshe hata video ikiwezekana si unajua mambo ya vibanda umiza? ili upapate pate na pesa za ziada .
 
S

sikuyaja

Member
Joined
Feb 21, 2012
Messages
47
Likes
0
Points
0
Age
41
S

sikuyaja

Member
Joined Feb 21, 2012
47 0 0
itakuwa zaidi ya laki tatu kwani kama unaonesha mpira wenye uwezo wa channel 3 kwa wakati mmoja au wanaita commercial package ni dolla 115 kwa mwezi. king'amzi na package zake ikiwemo ufundi ndani ya radius ya 10km ni kama Tshs 135,000. hivo kwa kuanza unahitaji takribani laki 400,000.
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Likes
428
Points
180
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 428 180
mawazo mazuri,kwa siku ambazo hakuna mpira onyesha movie asa ambazo zimetafsiliwa kiswahili na mkandala,lufufufufufufufufufufufufufufufuf
 
Amoeba

Amoeba

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
3,324
Likes
135
Points
0
Amoeba

Amoeba

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
3,324 135 0
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa!!..ni wazo tu mkuu.
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Dstv kila kitu ukilipia kwa hapa bongo dar es salaam ni kama laki 2 na elf 80 kama sijasahau, hapo unakua pia umelipia kuona machannel yote ya mipira na kila kitu dish na fundi wa kukuwekea dishi na pia king'amuzi na nini na nini na kila kitu.

Kila mwezi gharama ni shs 129,000 kuona machannel yote yenye mupira.
Uonyeshe hata video ikiwezekana si unajua mambo ya vibanda umiza? ili upapate pate na pesa za ziada .
Ubarikiwa mkuu nitafuata maelekezo yako
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
itakuwa zaidi ya laki tatu kwani kama unaonesha mpira wenye uwezo wa channel 3 kwa wakati mmoja au wanaita commercial package ni dolla 115 kwa mwezi. king'amzi na package zake ikiwemo ufundi ndani ya radius ya 10km ni kama Tshs 135,000. hivo kwa kuanza unahitaji takribani laki 400,000.
Shukran ubarikiwe mkuu
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
mawazo mazuri,kwa siku ambazo hakuna mpira onyesha movie asa ambazo zimetafsiliwa kiswahili na mkandala,lufufufufufufufufufufufufufufufuf
Ahsante na hilo ndilo lengo langu pia kuonyesha picha za Kaptain Gasper Mkandala Lufufu ahahaha hahaha kumbe unajua watu wanampenda huyu mjasiliamali eeeh kwan nimefikiri hvyo kutokana na wengi uswahilini kwetu wanapenda kukodi mikanda yake na wanakosa pakuangalia mpira
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa!!..ni wazo tu mkuu.
Wazo zuri nitalifanyia kazi mkuu shukran ubarikiwe
 
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
23,823
Likes
698
Points
280
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
23,823 698 280
mawazo mazuri,kwa siku ambazo hakuna mpira onyesha movie asa ambazo zimetafsiliwa kiswahili na mkandala,lufufufufufufufufufufufufufufufuf
halafu huku uswahilini ndio kunafaa, wengine wanaangalia mpira , wengine wanakuja kushangaa projector.
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Mkuu Tripo9
Endapo kama unatumia satelite dish inayotumia ving'amuzi vya Free to Air(FTA channel) kama Media com au strong vp matangazo ya mpira pale siwezi kupata free au kama ni ya kulipia naweza kupata kwa kiasi gani??
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Wadau nashukuru kwa maon yenu nakaribisha mwenye maoni pamoja na ushauri kuhusu aina ya projector na ubora wake ninayoweza kutumia kwa shughul hii
 
Viper

Viper

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2007
Messages
3,669
Likes
80
Points
145
Viper

Viper

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2007
3,669 80 145
Kama ni EPL na unatumia dstv wakijua unaweza kufungwa..

Labda utumie Arab sat etcl
 
Kivumah

Kivumah

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Messages
2,424
Likes
80
Points
145
Kivumah

Kivumah

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2008
2,424 80 145
Kuhusu Projectors cheki na huyu jamaa No.0752-858693 anaziuza, bei inaanzia Tsh 450,000.
 
Micha

Micha

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2011
Messages
269
Likes
4
Points
0
Micha

Micha

JF-Expert Member
Joined Sep 12, 2011
269 4 0
Nakushauri ufungue bar ambapo pia utakuwa unaonyesha mpira ligi mbalimbali, namaanisha biashara yako kubwa iwe ni hiyo ya bar na mpira iwe ni njia tu ya kuwavutia wateja, lakini hakikisha kila anayeingia hapo ananunua kinywaji ikiwezekana kwa kuwauzia coupons mlangoni wakati wa kuingia ambazo zitatumika kulipia vinywaji.
 
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2009
Messages
2,282
Likes
205
Points
160
Tripo9

Tripo9

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2009
2,282 205 160
Mkuu Tripo9
Endapo kama unatumia satelite dish inayotumia ving'amuzi vya Free to Air(FTA channel) kama Media com au strong vp matangazo ya mpira pale siwezi kupata free au kama ni ya kulipia naweza kupata kwa kiasi gani??
Kwa kweli hapa sina utaalamu. Lakini mambo ya free to air. yaani neno free, neno promotion neno lipia upate bure ni maneno sitakagi wala kuyasikia kwa sababu ni uzushi wa kijinga. Na wala usiwasikilize wajinga wa startimes au ting au wajinga wowote eti wataonyesha mpira wa majuu. Ni upuuzi mtupu. Jipige weka dstv simamia biashara yako hii waweza toka.

Kuna kitu nasikia sijui Arab sat sijui nini nasikia hii kitu ni nzuri na cheap pia. Ila gharama za mwanzo za kufungiwa ni za juu sana.
Unalipa kama laki tisa, wanakufungia upuuzi woooote halafu baada ya hapo kila mwaka, narudia tena kila mwaka unakua unalipa kama dolla 40 na unalipiA KWENYE MTANDAO hiyo pesa.
Ila hii kitu nimesikia tu, kuna ndugu yangu anajishughulisha na dili hizi A-town, ila kokote anafunga. Mimi hii huduma siiitumii

Mimi ntumia tu dstv kwa matumizi yangu binafsi
yhanx
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Nakushauri ufungue bar ambapo pia utakuwa unaonyesha mpira ligi mbalimbali, namaanisha biashara yako kubwa iwe ni hiyo ya bar na mpira iwe ni njia tu ya kuwavutia wateja, lakini hakikisha kila anayeingia hapo ananunua kinywaji ikiwezekana kwa kuwauzia coupons mlangoni wakati wa kuingia ambazo zitatumika kulipia vinywaji.
Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu
 
panyabuku

panyabuku

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
81
Likes
2
Points
15
Age
114
panyabuku

panyabuku

Member
Joined Apr 2, 2012
81 2 15
Shukran mkuu Tripo9 kwa kunifungua macho zaid
Unaweza kunipm contact za jamaa yako wa A-town??
 
Forum statistics

Threads 1,275,229
Members 490,947
Posts 30,536,233