Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

David webb

Senior Member
Nov 20, 2011
159
84
Banda umizani.jpg

Wanandugu, naombeni msaada tafadhali.

Mimi ni kijana mwenzenu nimebahatika kuchanga pesa zangu na nimefanikiwa kupata milioni moja na nusu; nataka kufungua biashara ya kuonesha mpira kwa jijini Dar (hasa mpira wa Ligi Kuu ya Uingereza). Je, vipi ni biashara nzuri kufanya au niachane nayo nifikirie kingine cha kufanya?

Wadau naombeni msaada wetu please. Kufanikiwa kwa hili ndo mwanzo wa biashara nyingine.

Asante, natanguliza shukrani.

Wenu mdau katika JamiiForums

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UELEWA WA BIASHARA HII
Wanandugu,

Naombeni msaada tafadhari, mimi ni kijana mwenzenu nimebahatika kuchanga pesa zangu na nimefanikiwa kupata milioni moja na nusu nataka kufungua biashara ya kuonesha mpira kwa Dar(hasa mpira wa ligi kuu ya Uingereza)je vipi ni biashara nzuri kufanya au niachane nayo nifikirie kingine cha kufanya.Wadau naombeni msaada wetu please.kufanikiwa kwa hili ndo mwanzo wa biashara nyingine.

Asante natanguliza shukrani

Wenu mdau katika JamiiForums.
Tafadhali wale wenye uelewa kuhusu hii biashara watujuze, hasa kuhusu taratibu zake na kampuni za TV zenye haki ya kurusha mechi hizo kama azam TV na DSTV.
Nataka nifungue biashara ya kuonesha mpira live ligi na makombe ya ulaya.

Nimekua nikifikira kununua dekoda 2 za dstv na vifurushi vyao ila nikawaza hui gharama naweza kuikwepa kwa kutumia laptop, website za mechi live na internet ya smile 4g niwe nazirusha mechi live kwenye flat screen mbili na hii itakuwa sio gharama.

Je, kuna changamoto zipi nazoweza kuzipata nikitumia internet kuoneshea mechi
Kwenye hyo milion 2 nahitaji Screen 1 kubwa, projector na king'amuzi cha DSTV chenye uwezo wa kuonesha mechi mbili kwa pamoja. Je kwa mtahi huo nitaweza?
Nahitaji mwongozo kwa anayefahamu hii biashara. Nampango wa kufungua banda la mpira Tabora ila uhalisia wa vitu muhimu kwenye hii biashara ndo sifahamu kama gharama za kufungua banda,faida na hasara zake.Ahsanteni


MAJIBU NA MICHANGO MBALIMBALI YA WADAU
BIASHARA HII NI FURSA NZURI NYUMA YA PAZIA
Kufanya biashara ya kuonesha mpira wa miguu; Fursa pekee iliyoko nyuma ya pazia!

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana hapa duniani. Ni mchezo pekee ambao unawashabiki wengi tena wa Lika zote hasa hasa vijana wakiongoza.

Hapa nchini Tanzania; Wanaume ndio wanaongoza kwa kushabikia mpira kuliko wanawake. Hapo zamani; simba na Yanga zikicheza; ulikuwa unakuta watu wengi kwa makundi wakisikiliza mpira huo kwenye radio. Walikuwa wakipata burudani kwa njia ya masimlizi na si kutazama.

Kwa miaka ya sasa baada ya technologia kukuwa na utandawazi wake; mambo yamebadilika. Kwa sasa radio si ishu tena kusikilizia mpira imebaki ziliendwa! Kwa maeneo mengi sana ya mijini na vijijini mpira huangaliwa kwenye Luninga ( TV).

Kwa sasa; watanzania hufatilia kwa ukaribu lingi maarufu sana na pendwa zenye virabu vikongwe na vikubwa duniani. Ligi hizo ni kama :

1. Ligi za Uingereza:
Premier Ligi
Championship ligi
ligi one
ligi two
Community ligi . etc

2. Ligi za Hispania:
Laliga
1st segunda
2nd segunda
3rd secunda . etc

3. Ligi ya Ujermani
Bundasliga. etc

4. Ligi ya ufaransa
Ligue 1
ligue 2
Nati0nal conferance. etc

5. Ligi ya Italiano
Serie A
Serie B. etc

6. UEFA Champion League

Haya ni mashindano ambayo hukutanisha virabu vikuu ( top 4) za kila ligue la nchi fulani barani Ulaya. Kumbe UEFA huchezwa na virabu vilivyopo barani Ulaya kwa sharti kuwa kira kirabu kitakachoshiriki ligi hii lazima kiwe kwenye top 4 kwenye ligi ya nyumbani. (kwenye nchi za Uingereza)

Kwa sharti hili; EUFA huwa mashindano matamu na ya hasa kuangalia kwani hukutanisha virabu vyenye uwezo mkubwa wa kusakata kandanda (Big clubs) hivyo kuleta big matches.

Mashindano hayo toka yanaanza yanakuwa na hamasa kubwa sana mpaka yanatia nanga mwezi wa tano.

Wapenzi wengi wa mpira kwao bora wakose chakula kuliko kukosa kuangalia kwenye TV mechi hizi hata kama zinacheza mida mobovu ya usiku mida ya saa tano ila utakuta watu wakifurika maeneo ya kuoneshea mpira.

7. Ligi kuu bara. ( Simba Vs Yanga)

8. Cecafa tournerment

9. Europa championship

10. Copa America Centanerio

11. World Cup (Kombe la Dunia)
N.k

Ndugu Msomaji; kama urikiwa ujui ni kwamba kupitia mpira wa miguu watu wengi hutengeneza sana pesa kila Week end ( juma mosi na juma pili) kwani virabu vyote nilivovitaja hapo juu hushuka viwanjani kila week end. Na watazamaji hulipa kwa kawaida sh. 500 kwa mechi ndogo yaani mechi isiyo na ushindani au mvuto kwa mfano: Barcelona VS Eiber; Chelsea VS QPR au PSG vs Rennes.

Kiingilio cha sh. 1000 hutozwa kwa big matches yaani timu mbili kubwa zinapokutana. Kwa mfano: Barcelona VS Real Madrid; Arsenal VS Man U; Man City VS Liverpool au Germany VS Brazil.

Watazamaji hufulika sana kwenye vibanda vya kuoneshea mpira. Iwe mchana au usiku wa manane. Watu huacha familia zao na kwenda kuangalia mpira.

Kwa sasa mpira umekuwa starehe kuu kwa jamii. Mpira umekuwa burudani kuu kwa jamii za kitanzania.

Ujio wa kamari wa Kubashiri ( betting) nako kimenogesha sana mapenzi ya mchezo huo. Watu wengi kwa sasa hubeti ( betting nayo fursa nyingine) na wanapokuwa wamebeti wengi hupenda kwenda kutizama mechi walizozibetia.

Kama una ndoto za kufungua kibanda ( Soccer academy) ya kuoneshea mpira; basi fata hatua hizi:

1. Andaa mtaji wako yaani budget.

2. Chagua jina zuri na la mvuto la kuita Center yako.

Hii inaitwa Brand Name. waweza kuita centa yako majina kama haya: Amsterdam Academy; Soccer Academy; Laliga; Football Academy; Old Traford; Jina la sehemu ulipo ikifatiwa na Academy; Soccer Academy. Mfano: Kyela Soccer Academy; Mererani Soccer Academy; Tandale Soccer Academy; Arusha Academy; Bukoba Academy n.k.

3. Tafuta sehemu ya kujenga banda la kuoneshea mpira. Eneo hilo lazima liwe center au liwe la kufikika na la usalama.
- Banda lako lazima liwe la kisasa lenye kuingiza na kutoa hewa. Weka Fane kila mahal; Viti waweza kutumia vya plastic au ukatumia banch. Epuka kuwa na upungufu wa viti maana wateja wanaposiama huchoka maana mpira unachukua zaidi ya lisaa moja na nusu. Weka sakafu nzuri chini na ukiweza weka marumaru ( tiles)

Vifaa.
- Nunuwa Flat Screen TV 2; 3; 4 au 5 kubwa kubwa ( pana na kubwa kwa ajili ya utazamaji mzuri) na ziweke mahara pa kuonekana kwa wote. Unaweza ukaweka nyingine kati kati ya ukumbi ili kuwawezesha watazamaji wa mbali kuona vizuri. Lipia king'amzi chako na inasauliwa kutumia DST decorder na lipia king'amzi chako kwa wakati

- Nunuwa Generator kwa ajiri ya emergency ya katizo la umeme.

Vitu vingine vya ziada
  • Weka vinywaji baridi kama vile:maji na soda.
  • Uza Vocha hasa hasa za Halotel kwani watazamaji wengi hukuta wako bize wakichezea simu zao upande wa Internet wakicheki taarifa za mpira hivo huhitaji Data zaidi na walowengi hutumia mtandao wa halotel.
  • Mwanga wa kutosha uwepo maeneo ya sehemu ya kuangalia mpira kuepuka vibaka usiku maana mechi nyingi huchezwa usiku.
Mbinu na mikakati ya kuwashika wateja

Toa free matches.


Yaani kama kuna big match ambayo itacheza saa 12 na kuanzia saa tisa saa kumi kuna match ndogo inacheza basi wateja usiwatoze pesa. wache waangalie hiyo mechi huku wakijiandaa kuangalia hiyo big match inayofata. Kwa mfano: Kama saa moja na nusu usiku kuna mechi kati ya Arsenal Vs Barcelona na kuanzia saa kumi na mbili kunacheza mechi baina ya Celtic vs Porto basi wateja walokuja kuangalia mechi ya Arsenal vs Barca waache waingie na usiwacharge pesa waangalie hiyo mechi huku wakisubili kuangalia mechi ya Arsenal.

Vile vile kama saa 11 jioni kuna mechi baina ya Chelsea na Man United na huku kuanzia saa kumi kuna mechi ya Crystal palace vs Burnley inacheza basi wateja waruhusu waingie waangalie hii mechi bure huku wakisubiri mechi inayofata ya Chelsea.

N.b Epuka kukaba kila kona hata penati! Maana yake Epuka kuonesha kuwa wewe una uchu wa pesa na unakaba kila senti. Vimechi vingine wala havina mvuto na mashabiki hivo toa kama free entry kwa wateja.

Weka mapaparazi. (wanapropaganda)

Chagua vijana watano washabiki wa ligi za uingereza au wanaojua vizuri mpira na waache wawe wanaingia bure kila siku. Vijana hao chagua washabiki wa: Arsenal, Chelsea; Man U; Liverpool; Barcelona; Real Madrid ; PSG; n.k wale ambao ni wakereketwa wa timu zao. Kwa kufanya hivo unakuwa umetengeneza wakaribisha wateja kwenye center/ Acadeny yako. Hao vijana watakufanyia kazi nzuri tu ya kukusanya wateja mitaani. Pia wapenzi wa mpira wa miguu walowengi hupenda kwenda kuangalia mpira sehemu ambapo kuna makelele na mabishano. Ndo maana utakuta mechi fulani inaoneshwa bure kwenye Runinga za kawaida majumbani ila utakuta bado watu wanaenda kibandani kulipia mpira sh. 1000 au 500 ilhali nyumbani angeangalia bure tena akiwa na familia yake!

Makelele na Tambo za mashabiki ndo huwavuta wengine kuja kuangalia mpira kibandani.Usione noma kupoteza hiyo 5000 ya kiingilio cha hao watu 5 huku umeingiza Laki moja na nusi kwa mechi moja

Utapataje Faida

Kama kawaida; kifurushi champira kwenye DST huanzia elfu 80 hadi 150000 kwa mwezi.

Kwa wanaofanya biashara ya kuonesha mpira hii pesa huirudisha kwenye kiingilio cha mechi moja tu. Hebu ona kwa mfano: Mechi ya Manchester united Vs Arsenal. Utapata watazamaji zaidi ya 150. Na kwa kuwa hii ni big mechi basi kila mmoj atatoa kiingilio cha sh 1000 hivo basi utapata zaidi ya laki na nusu. Na hapo ni Mechi moja kwa siku. Sasa mwezi mmoja una big mechi ngapi? Una mashindano mangapi maarufu!?

Kwa taarifa yako; Wanaofanya biashara ya kuonesha mpira siku za Week End ( Jumamosi na Jumapili) kwao ni siku za mavuno kianzia mchana hadi usiku. Pia kati kati ya wiki kunakuwaga pia na mashindano mbali mbali hivo huvuna mapesa pia maradufu.

NB: Pengine una mtaji na hujaona ufanye buashara gani; basi usiwaze kununuwa bajaji; kununua Noah; kujenga nyumba za kupangisha au kufungua duka n.k. Biashara nzuri na ambayo haina ushindani mitaani ni biashara ya mpira. Ili kufungua biashara hii yakupaswa kuwa na mtaji wa Milioni 7 hadi 10 kama kweli utakuwa umedhamilia kuifanya vizuri na kisasa hii biashara. Nakuhakikishia hii hela yako utairudisha ndani ya muda mfupi sana. Fungua biashara kisasa ili upate wateja wengi na wa kisasa ambao wako smart.

Hapa nchini biashara nyingi ni za kuigana. kwamba mmoja akifungua duka hapa na mwingine anafungua tena duka hopo hapo jirani. Mmoja akifanya hiki na mwingine anaiga anafungua the same business pembeni hali ambayo inapelekea uhasama na kununiana mpaka naenda kwa waganga wa kienyeji kufanyiana mbaya. Nakuhakikishi; biashara ya mpira iko special na si ya kuigana maana waliowengi hawajui hii fursa na kwa taarifa yako watanzania hatujajua kuwa mpira ni biashara bali hujua kuwa mpira ni burudani.

Viva Football!
UNAWEZA KUIANZA KWA MTAJI WA MILIONI 5

Biashara nzuri kwanza unatakiwa uwe na banda kubwa lenye hewa pia ufunge mafeni (mapangaboi) pia mabenchi ya kutosha kwa mbele unaweza utandika maturubai tv unatakiwa uwe nazo kuanzia mbili mimi ninazo inch 43 na vinga'muzi unatakiwa uwe navyo kuanzia vinne vya DSTV viwili utamtafuta fundi atakuungia mfumo wa extra view yaani utaonesha mechi mbili kwa wakati mmoja pia unatakiwa uwe na kinga'muzi cha startimes kwa ajili ya mechi za uefa ndogo na cha azam kwa ajili ya mechi za ligi kuu tanzania bara na mechi nyingine mbalimbali.

Mtaji kwa biashara hii unaweza ukaanza na sh m5 ujenzi wa banda milioni 2 tv za flatscreen mbili milioni 1.4 vinga'muzi vinne I mean vya dstv viwili cha startimes 1 na cha azam 1 vitakucost kama laki 7 plus na vifurushi vyake fedha itakayobaki kuna vitu vingine mafeni ya mtumba moja linauzwa sh40,000/*3 itakuwa sh 120,000/ kwa ajili kupunguza joto bila kusahau generator kubwa sh 400,000/ fedha iliyobaki utalipa kodi eneo ulilokodi.
MAKADIRIO KABLA YA KUANZA BIASHARA HII

Moja kati ya michezo pendwa sana kwa vijana na hata wazee na watoto kwa ujumla ni mchezo wa miguu, mpira (Football). Ligi nyingi sana zimeanza na zinatarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu, huku tayari ligi pendwa ya EPL imeanza kutimua vumbi huku ligi ya Tanzania soon kuanza nayo.

Napenda kuanza biashara hii ya kuonyesha mpira hasa kwa ving'amuzi vya DSTV na AZAM ikiwa kuonyesha mechi za nje ya nchi na ndani hasa timu pendwa za watani wa jadi (Simba na Yanga).

Huu ndo uchambuzi wangu ambao nategemea kufanya makadirio kabla ya kuanza ujenzi na biashara kwa ujumla:

Ujenzi wa Banda kwa kutumia Mabati pamoja na umeme hasa kutokana na sehemu niliyopo ni ya kijijini (sio sana) itanigharimu Tshs 900,000.

TV ya Kisasa (LED Inch 43) itanigharimu Tshs 900,000.

Manunuzi ya Ving'amuzi vyote viwili (AZAM - Tshs 135,000 & DSTV - Tshs 109,000)

Jumla = Tshs 244,000.

Vifurushi Vya Kujiunga Ndani husika (AZAM PLUS - Tshs 23,000 & DSTV Compact - Tshs 69,000)

Jumla = Tshs 92,000.

Kabati kwa ajili ya kuwekea/kuhifadhi TV itanigharimu Tshs 85,000.

Matumizi mengine ya dharura (Emergency) ndani ya ujenzi ni Tshs 200,000.

Jumla ya Mahitaji na Gharama kwa Ujumla Itanigharimu Kiasi Cha Tshs 2,421,000

Nakaribisha maoni na mapendekezo yenu yaweze kunisaidia mimi pamoja na wanajukwaa wengine wenye malengo kama yangu ya kuanzisha biashara hii.

Asanteni
TAZAMA WAPINZANI UFANYE ZAIDI. ZINGATIA UWEPO WA NISHATI USIO NA SHAKA

Nyongeza, angalia wenzio wana vitu gani then wewe boresha uwe zaidi yao.

Jitahidi mafuta yawemo muda wote kwenye jenereta kama itatokea umeme kukatika unawasha haraka kabla ya mechi hakika jenereta linakuwa nje tayari ili umeme ukikatika unawasha chap kwa haraka.

usiweke viti vya plastic utakula hasara kubwa sana.

Mkuu usisahu kitambulisho cha mjasilimali kama uwekezaji wako hauzidi 4M.

NB: kwa Tv moja huwezi kufanikiwa, chukulia kwa mfano

15:00 Nyumbu vs Arsenal

15:00 Chelsea vs Spurs

utaweka ipi na utaacha ipi?
VITU VYA MUHIMU KUWA NAVYO
Vitu muhimu vya kuwa navyo flatscreen kuanzia inch 43 uwe nazo kuanzia mbili vinga'muzi vya Dstv unatakiwa uwe navyo viwili kimoja kinaunganishwa mfumo wa extra view vinga'muzi vya azam navyo viwe viwili kwa ajili ya mechi za ligi kuu tanzania bara na mechi za klabu bingwa afrika,mapinduzi na mechi zingine n.k pia usisahau startimes kwa ajili ya mechi za europa league upande wa banda linatakiwa liwe banda kubwa la kutosha lenye mabenchi na ikiwezekana ufunge feni chini unaweza ukawawekea turubai wateja wakakaa usisahau Generator ili kupambana na kero za umeme.
BIASHARA HII NI NZURI UKIPATA ENEO SAHIHI

Biashara yakuonyesha mpira inalipa kama itakuwa karibu na maeneo haya.

1. Chuo

2. Shule za boarding

3. Vituo vya magari hasa dalala na parking za magari makubwa.

4. Mijini sehemu yoyote yenye kusanyiko kubwa la vijana.

Vijijini watu wanafuatilia ligi ya Tanzania tu na mechi za mashindano kama AFCON EURO na World cup.

Kama anataka kuweka vijijini simshauri kupeleka supersport labda ajiridhishe hapo anapopeleka anauhakika walau wa watu hamsini kila mechi wanaweza ingia kuangalia EPL.

faida atakuwa anaipata kunapokuwa na mechi kubwa kubwa kwani zina mashabiki wengi maeneo mengi.

Siku ya simba na yanga anapandisha kiingilio kuwa 1000 watu wataingia wengi bila kujali kiingilio na atapata faida.
KAMA UNATUMIA INTERNET KUONESHA, ZINGATIA HAYA
Kuna vitu vitatu ambavyo inabidi uzingatie.

1. Speed yako ya Internet. kama speed yako ipo slow ni lazima itanata tu.

2. Quality ya video (144p 240p 360p 480p 720p 1020p).

hapa 360p - hii ni standard, 720p - ni HD, 1020p - hiini full HD. Jinsi hizo namba zinavyoshuka mahitaji ya internet pia yanashuka lakini muonekano unakua mbaya.

3. Speed ya link yako ya kustream. Hapa ndipo kunawachanganya wengine, inaweza ikawa speed yako ya internet ipo vizuri sana na bado video ikawa inanata vile vile. Hii inawezekana kusababishwa na speed ya link husika, kuna uwezekano wakati huo unaangalia kukawa na watu wengine ambayo wanaangalia kwa kupitia link hiyo hiyo matokeo yake hiyo link ikawa busy sana kiasi kwamba haiwezi kuwarudishia frame za video wote kwa wakati mmoja.

Mwisho utakuja kugundua kuwa links ambazo ni shared na free kwa baadhi ya mechi huwa zipo busy na slow (Ukistream video inaganda lakini ukiingia youtube unaona vizuri tu video bila mnato).

Pia utakuja kugundua ukitaka kuangalia FHD itakutoka zaidi ya GB 1.5 kwa mechi, sasa unaweza ukafanya maamuzi sahihi zaidi.
MAHITAJI MUHIMU KWA BIASHARA HII

-Tv zisiwe chini ya mbili

-Dstv' set + dekoda ya extra view + Bando lao + 27,500 charges ya extra view

-Azam set +Fundi + Bundle

-Viti/Mabenchi

-Gharama ya kujenga ukumbi au kuukodisha

-Jenereta + wiring yake

-Fundi wa welding na nondo za kuchomelea tv ukutani ili isiwe rahisi sana kumtamanisha mwizi.

-Mlinzi wa eneo
NI BIASHARA NZURI, MAUMIVU YAPO KWENYE VIFURUSHI TU
Kwa wenye mabanda bei za vifurushi ni kubwa sana hasa Dstv ili upate ligi ya Uingereza EPL hapa inakulazimu ununue kifurushi kuanzia hiki cha dstv compact plus 122500 (laki moja na ishirini na mbili mia tano) hapo una kimoja kama una Tv mbili inakubidi uwe na decoder mbili na zote uzilipie ile huduma ya kuunganisha tv mbili kwa decoder moja na ionyeshe mechi tofauti wanadai ilitolewa anaejua mautundu tusaidiane.

Binafsi baada ya kuona hizo gharama hiyo ya kifurushi bado hujalipa kodi na umeme na kibaya eneo nilipoweka hii biashara haijachangamka kivile NILIFANYA HILI KUJIPUNGUZIA GHARAMA.

Nikanunua sattellite dish lile kubwa na receiver ili nipate chanell za bure kweli sport 24 Hd inarusha karibu mechi zote inanisaidia japo hapa karibuni imesumbua sana hii sport 24 Hd signal zilikuwa chini sana now ipo vizuri ila changamoto yake kuu NIONAVYO HII INAFAA KWA MATUMIZI YA NYUMBANI SIO KIBIASHARA.

SOLUTION NYINGINE KUNA HAWA WANAWEKA channell za mpira katika azam au star times hawa sijawajaribu kama yupo anaezitumia tusaidiane.

ILA NI BIASHARA NZURI UKIWA NA LOCATION NZURI INGAWA MAUMIVU VIFURUSHI wageni karibuni katika hii bussiness leteni na maswali.
CHUKUA USHAURI HUU
Jamani mimi naonesha mpira toka 2011 hii biashara ngumu sana ila inaitaji uwe na eneo lako kama mimi itapunguza cost ghalama zipo juu lakini ili upate faida unatakiwa ukae mweyewe 2 usifanye malipo mwisho wa mwezi lipa kila mechi kidogokidogo kadili unavyoingiza 3fungua dicoda Ya biashara toka dstv utapewa dicoda 3 kwa malipo ya mwezi 294000 utakua unaonesha game 3 kwa Wakati mmoja mtajisumbua bule kufunga hayo madish mi nimefuatwa mara nyingi sana lakini sitaki kwanza wenye haki ya kurusha premium league ni DSTV ukionekana ama kwa bahati mbaya mtu kachoma imekula kwako utakwenda mahakamani izo dicoda za mipango tu hazina mda uwa zinafungwa katikati ya game
 
Kaka andaa vijana wawili utakaofanya nao kazi wawe good movie wachers nitakupa idea Nadhani itafunction.
 
Hiyo biashara tafuta kuweka kwenye eneo lenye umati wa watu wasio na uwezo wa kufunga dstv. zaidi uswazi. Screen iwe kubwa iwezekanavyo na clear kabisa bila chenga.

Funga DSTV na uweke viti au mabenchi ya kutosha. Premier League itakuingizia hela. Kama upo uswazi wakati hamna ligi utapata hela kwenye video za movies
 
Wadau nilikuwa na wazo la kununua Projector na satelite dish ili kuonyesha mipira ya ulaya ninaeneo langu kubwa linaweza kuingiza watu mia mbili naombeni msaada wa kujua gharama ya projector na satelite dish nianze hii biashara kwa yoyote mwenye uzoefu na biashara hii anisaidie kunipa ushauri zaid ni vitu gan vya kuongeza hapo.

Nawatakia mafanikio mema wote ndan ya mwaka huu Mungu awe pamoja nanyi. Nasubiri msaada wa mawazo yenu.
 
Dstv kila kitu ukilipia kwa hapa bongo dar es salaam ni kama laki 2 na elf 80 kama sijasahau, hapo unakua pia umelipia kuona machannel yote ya mipira na kila kitu dish na fundi wa kukuwekea dishi na pia king'amuzi na nini na nini na kila kitu.

Kila mwezi gharama ni shs 129,000 kuona machannel yote yenye mupira. Uonyeshe hata video ikiwezekana si unajua mambo ya vibanda umiza? ili upapate pate na pesa za ziada.
 
Itakuwa zaidi ya laki tatu kwani kama unaonesha mpira wenye uwezo wa channel 3 kwa wakati mmoja au wanaita commercial package ni dolla 115 kwa mwezi. king'amzi na package zake ikiwemo ufundi ndani ya radius ya 10km ni kama Tshs 135,000. hivo kwa kuanza unahitaji takribani laki 400,000.
 
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa! Ni wazo tu mkuu.
 
Dstv kila kitu ukilipia kwa hapa bongo dar es salaam ni kama laki 2 na elf 80 kama sijasahau, hapo unakua pia umelipia kuona machannel yote ya mipira na kila kitu dish na fundi wa kukuwekea dishi na pia king'amuzi na nini na nini na kila kitu.

Kila mwezi gharama ni shs 129,000 kuona machannel yote yenye mupira.

Uonyeshe hata video ikiwezekana si unajua mambo ya vibanda umiza? ili upapate pate na pesa za ziada .

Ubarikiwa mkuu nitafuata maelekezo yako.
 
itakuwa zaidi ya laki tatu kwani kama unaonesha mpira wenye uwezo wa channel 3 kwa wakati mmoja au wanaita commercial package ni dolla 115 kwa mwezi. king'amzi na package zake ikiwemo ufundi ndani ya radius ya 10km ni kama Tshs 135,000. hivo kwa kuanza unahitaji takribani laki 400,000.

Shukrani ubarikiwe mkuu.
 
Mawazo mazuri, kwa siku ambazo hakuna mpira onyesha movie asa ambazo zimetafsiliwa kiswahili na Mkandala

Ahsante na hilo ndilo lengo langu pia kuonyesha picha za Kaptain Gasper Mkandala Lufufu ahahaha hahaha kumbe unajua watu wanampenda huyu mjasiliamali eeeh kwan nimefikiri hvyo kutokana na wengi uswahilini kwetu wanapenda kukodi mikanda yake na wanakosa pa kuangalia mpira.
 
Hivi hii biashara bado inauzika, kweli Tanzania ni kubwa, maana huku kwetu Mpitimbi watu wanaonesha mpira kwenye Bar kiingilio bia yako; unaonaje hilo eneo ukifungua bar ukawa unaonesha mpira ligi zote kubwa! Ni wazo tu mkuu.

Wazo zuri nitalifanyia kazi mkuu shukrani ubarikiwe
 
Mkuu Tripo9

Endapo kama unatumia satelite dish inayotumia ving'amuzi vya Free to Air(FTA channel) kama Media com au strong vp matangazo ya mpira pale siwezi kupata free au kama ni ya kulipia naweza kupata kwa kiasi gani?
 
Wadau nashukuru kwa maon yenu nakaribisha mwenye maoni pamoja na ushauri kuhusu aina ya projector na ubora wake ninayoweza kutumia kwa shughul hii
 
Kama ni EPL na unatumia dstv wakijua unaweza kufungwa.

Labda utumie Arab sat etcl
 
Nakushauri ufungue bar ambapo pia utakuwa unaonyesha mpira ligi mbalimbali, namaanisha biashara yako kubwa iwe ni hiyo ya bar na mpira iwe ni njia tu ya kuwavutia wateja, lakini hakikisha kila anayeingia hapo ananunua kinywaji ikiwezekana kwa kuwauzia coupons mlangoni wakati wa kuingia ambazo zitatumika kulipia vinywaji.
 
Back
Top Bottom