Naomba Ushauri - Kufuga ng'ombe wa maziwa na kupack maziwa

Heshima kwenu wana JF,

Naombeni mchango wenu katika kuboresha wazo langu la uwekezaji ambalo natarajia kuanza utekelezaji miezi ya karibuni.
Mimi ni msomi wa kawaida nilifanya kazi kwenye NGO kwa miaka kadhaa, nikaacha na kwenda shule na sasa natarajia kumaliza shule karibuni lakini kwa bahati mbaya field yangu siyo miongoni mwa well paid jobs kwa hapa TZ. Hivyo sijisikii kurudi tena mtaani na kuomba ajira za watu aidha serikalini au kwenye NGO kwa ufupi nataka kujiajiri.


Nimetafakari na nikaona niwashirikishe katika wazo hili ili nipate michango yenu ya kuliboresha. Natarajia kuanzisha ufugaji wa ngombe wa maziwa Mtwara , eneo km 20 kutoka Mtwara mjini. Natarajia kuanza na ng'ombe atleast 10 ambao nategemea watatoa lita takribani 120 kwa siku kwa kadirio la chini kulingana na mazingira.

Kikwazo kinachonikabiri ni kwamba sina uhakika wa soko lakini pia bei ya maziwa yasiyoongezwa thamani ni ndogo 800/=kwa lita kwa sasa.
Hivyo ninawazo la kujaribu kutafuta technology rahisi ya kuyaongezea muda wa kuhifadhi hadi siku 10 angalau na kuyapack katika mifuko ya kawaida ya Nylon yenye ujazo wa ¼, ½ na lita 1. Kwa kufanay hivi nitakuwa kwanza nimeyaongezea thamani lakini pia nitakuwa na fursa ya kuuza hadi kwenye miji jirani.


1. Naombeni ushauri je ni technolojia gani rahisi naweza kuitumia kwa wale wenye utaalamu au uzoefu.

2. Ni wapi naweza nikapata mitambo/mashine ya kuongeza muda wa hifadhi na Ku-pack. Ikiwezekana nikipata na makadirio ya gharama itakuwa vizuri zaidi.

Angalizo:

Mashine yenye uwezo wa kuprocess maximum Lita 2,000 kwa siku siyo mbaya itafaa sana kwani nitakuwa nanunua maziwa mengine kutoka kwa wafugaji wadogo ili kutosheleza mahitaji ya kiwanda.

STRENGTH

MTAJI TZS 40,000,000/= (MILLIONI AROBAINI)
Tayari nina biashara ya kijiduka.

Naishi hapa Mtwara kwa miaka 6 sasa.
Field niliyosomea kwa mbali inahusiana na hiki ninachotaka kukifanya hasa kwenye uzalishaji siyo processing and packaging.


Tafadhali naombeni michango yenu.


Biashara hiyo Ni exhausted sana, Kama huna uhakika na masoko please drope it, and you also have all wrong reasons to start that business, kwanza sababu Ni kwamba field uliyosoma haina Ajira, sasa sijui uliisomea nini, Ni vyema ukaingia kwenye biashara Kama a mare choice na sio last option, kabla ujaanza soma hizi facts:

- Una nini cha tofauti unacholeta kwenye hii Biashara?
- Kwa nini umeichagua?
- Umeshawahi kufuga kabla?
- Una order yeyote uliyo na uhakika nayo.
- itachukua mda gani mpaka ufanye sales, can you survive mpaka huo mda ufike?

Mafanikio ya biashara Ni sales, bila kuuza Ni Ngumu sana sana sana!
 
Biashara hiyo Ni exhausted sana, Kama huna uhakika na masoko please drope it, and you also have all wrong reasons to start that business, kwanza sababu Ni kwamba field uliyosoma haina Ajira, sasa sijui uliisomea nini, Ni vyema ukaingia kwenye biashara Kama a mare choice na sio last option, kabla ujaanza soma hizi facts:

- Una nini cha tofauti unacholeta kwenye hii Biashara?
- Kwa nini umeichagua?
- Umeshawahi kufuga kabla?
- Una order yeyote uliyo na uhakika nayo.
- itachukua mda gani mpaka ufanye sales, can you survive mpaka huo mda ufike?

Mafanikio ya biashara Ni sales, bila kuuza Ni Ngumu sana sana sana![/QUOTE


Usimkatishe tamaa mwaachee akae
 
Back
Top Bottom