Naomba ushauri kudhurumiwa kiwanja

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,441
2,000
Usinunue njia kwanza fuatilia ramani ya eneo husika mipango miji Kisha Kama Ni kweli eneo limerasimishwa lazima Kuna njia halafu UKINUNUA ARDHI ILIYOPIMWA AU KURASIMISHWA NI LAZIMA UKAANDIKISHANE KWA MWANA SHERIA ANAE TAMBULIKA TENA ILI KUTHIBITISHA UHALALI WA MWANASHERIA UNA GOOGLE ID YAKE!
Mkuu umesema sahihi kabisa. Mimi huku ninahangaika na kesi iliyoamliwa kipumbavu na Mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya, eti ametoa mapendekezo hati yangu ifutwe. Nimeipeleka mahakama kuu, nina uhakika wa kushinda maana yule aliyeuziwa hicho kiwanja hana vielelezo vyovyote vinavyothibitisha kwamba aliyemwuzia ni mmilki halali wa kiwanja hicho. Na kosa kubwa kununua kiwanja kwa kusainishana na serikali ya mtaa tu bila kuwahusisha watu wa ardhi wala mwanasheria. Kwa kweli ndiyo maana watu wanafikia hatua ya kumiminia watu risasi! Niliomba sana Mungu anisaidie nisijekuwa na hasira na mwenyekiti wa baraza na wazee wake wa baraza, ningewaua!!
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
9,808
2,000
Kwani huyu mshikaji amesema amenunua kwenye squatter area? Huyu si anasema eneo li a ramani kabisa? Squatter area gani inakuwa na ramani?
Ukisoma maelezo yake kwa kina ni squarter na ndio kuna huo ujinga wa kuuziana njia,surveyed areas kuna hati ya wizara kama kitabu fulani ndani yake kuna ramani na coordinates za kiwanja husika
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,369
2,000
Kila siku tunatoa ELIMU mitandaoni ya namna ya kununua kiwanja lakini hamfuatilii..

Kwa usalama wako siku nyingine hakikisha kiwanja unachotaka kununua kiwe na ramani ambayo ni surveyed na kwa kuhakikisha zaidi nenda hata wizarani kafanye search ya eneo unalonunua

Kwa stage uliyofikia cha kukusaidia hatuna zaidi ni kukuambia siku nyingine ukitaka kununua kiwanja fuata ushauri uliopewa hapo juu.

Not necessarily eneo liwe surveyed, 90% ya maeneo TZ are not surveyed, does that mean people should not buy land Not at all. Katika unsurveyed areas hakikisha majirani wote wanaopalana na kiwanja hicho wameshujudia mipaka, njia na lolote unaloona Lina maslahi kaktika kiwanja hicho. Washirikishe viongozi wa mtaa wako , wao wanajua Hali halisi ya ardhi katika maeneo yao.
Kwa hili ambalo huna njia ya kutokea, Ni kuongea kiungwana na aliyeziba njia akupe njia hata kwa kumlipa otherwise utakiacha kiwanja maana huna pa kupitia kufikia kiwanja chako. Kuna case law inayosema Kama huna njia si jukumu la jirani kukupa njia.
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
33,500
2,000
Huko kinyerezi si ndo walikomuuwa mwalimu kisa kiwanja?

Umeshanunua, umeingizwa mkenge yote sawa, angalia namna utakavyouziwa njia ya kufika kwako.

Kama haiwezekani kupata njia amua upauze, hapo ujue utapata hasara kidogo kwani pesa yako haiwezi kurudi yote.

Then tafuta eneo lingine nunua.

Makosa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku,

Jitahidi usiingie hasara zaidi.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,369
2,000
Huko kinyerezi si ndo walikomuuwa mwalimu kisa kiwanja?

Umeshanunua, umeingizwa mkenge yote sawa, angalia namna utakavyouziwa njia ya kufika kwako.

Kama haiwezekani kupata njia amua upauze, hapo ujue utapata hasara kidogo kwani pesa yako haiwezi kurudi yote.

Then tafuta eneo lingine nunua.

Makosa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku,

Jitahidi usiingie hasara zaidi.
umemshauri vema kabisa! Hawezi kumalazimisha jiraji ampe njia, ni kuelewana naye au auze.....
 

Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
868
1,000
Jaribu kwanza kuongea na huyo aliyeziba njia kwa kumlipa sehemu hiyo ya njia. Ikishindikana jaribu kutafuta tu njia ya kupita watu kwa miguu kuinigia hapo kwako halafu unajenga nyumba ya kupangisha au unakiuza kwa bei rahisi kufidia hasara.

Lakini huyo aliyekuuzia kwa kuwa alikuwa anajua anafanya nini mburuze polisi kisha mahakamani yeye na hao wenzake wa serikali za mitaa kwa sababu ya kukupa ramani feki. Na hao wenye ramani feki wanatafutwa sana na serikali kwani ndio wanaleta migogoro ya ardhi kiasi wizara ya ardhi na seriakli kwa ujumla inalaumiwa. Nina hakika wakifika polisi/mahakamani wataeleza vizuri hiyo ramani feki waliitolea wapi ili upatikane mtandao wote.
 

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
2,136
2,000
Ninyi wanunuzi wa viwanja mnatusumbua sana, sasa hivi hapa nilipo nahangaika na kesi mahakamani! Jitu limejipeleka tu kwa mwenyekiti wa mtaa kulipia kiwanja bila kujiridhisha kwa ofisi ya ardhi Manispaa likajikuta linauziwa kiwanja ambacho tayari kina hati kwa jina langu. Sasa na wewe ilikuwaje ukatumia ramani ya mwuzaji wa kiwanja? Kwa nini hukuenda kupata ramani halisi kule mipango miji? Kosa umelifanya wewe mwenyewe, ulitakiwa ukawachukue mipango miji waje wachukue coordinates za eneo hilo halafu wakakuangalizie kwenye ramani yao ambayo imetokana na survey ya eneo husika. Sasa nenda Manispaa ukawaone maafisa mipango miji watakusaidia (ila lazima hapo wakupige hela kidogo za usumbufu) kama kweli hakuna njia ya kuingia uwanjani kwako! Ukikuta kweli hakuna njia itakuwa imekula kwako! Ukikuta kuna njia itabidi ufungue kesi mahakamani na mashahidi wako watakuwa hao hao serikali ya mtaa pamoja na watu wa ardhi!
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,441
2,000
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
Ila mkuu hujaelewa nilichokuwa namaanisha! Fikria huyu mwamba kununua kiwanja kwa kutumia ramani aliyooneshwa na mwuzaji, sasa kama mwuzaji alijitengenezea ramani fake ikapishana na ile ya mipango miji atakuwa na haki gani hapo? Mimi nimemshauri aende mipango miji waje walianganishe huo mchoro na hicho kiwanja kuona hiyo njia imekaaje! Tusipende kuamini hizi ramani za wauzaji nyingi wanajitengenezea! Unaweza kuuziwa hata open space!
 

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
2,136
2,000
Ila mkuu hujaelewa nilichokuwa namaanisha! Fikria huyu mwamba kununua kiwanja kwa kutumia ramani aliyooneshwa na mwuzaji, sasa kama mwuzaji alijitengenezea ramani fake ikapishana na ile ya mipango miji atakuwa na haki gani hapo? Mimi nimemshauri aende mipango miji waje walianganishe huo mchoro na hicho kiwanja kuona hiyo njia imekaaje! Tusipende kuamini hizi ramani za wauzaji nyingi wanajitengenezea! Unaweza kuuziwa hata open space!
Sawa mkuu nimekuelewa
 

A.Ngindo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
214
225
naomba kujua hili likoje mkuu maana kesho naenda kwenye ofisi za hawa jamaa kwa ajili ya kuwapelekea shauri langu
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
 

Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
7,702
2,000
Habarini wana jamvi,Nina shida kuhusiana na kichwa cha habari husika hapo juu.

Iko hivi Miezi 6 iliyo pita nilinunua kiwanja cha makazi maeneo ya Kinyerezi Dar es Salaam, Baada ya kua nimeonyeshwa mipaka ya eneo na michoro ya kiwanja katika ramani ya mipango miji na mhusika wiki moja badae nikaenda ofisi za serekali ya mtaa za eneo husika ili kujiridhisha na mmiliki wa eneo pamoja na uhalali wa kiwanja.

Nakukuta kua jamaa anatambulika kama mmiliki halali wa eneo kupitia hati ya serekali ya mitaa na eneo limerasimishwa kama eneo la makazi,nikampigia jamaa simu ilikesho yake tuka andikishane nilipie.

Kesho yake mimi na mashahidi wangu wawili ambao ni ndugu zangu pamoja na mmiliki wa kiwanja na shahidi wake mmoja tukaenda ofisi za mtendaji ili watuandikie hati ya mauziano mimi na mmiliki wa eneo pamoja na mashahidi wetu tuka sign ile document na ikapigwa mihuru na mtendaji.

Baada ya hapo tukatoa copy kadhaa za ile hati ya mauziano na kuacha copy mbili ofisi za mtendaji baada ya hapo tukaenda bank nikamlipa mmiliki wa kiwanja na akanipa ile hati ya mauziano,kila mtu akaendelea na maisha yake sasa shida imekuja juzi nimeenda sight nimekuta kuna jirani yangu mmoja kaweka uzio kwenye eneo ambalo ndio njia ya mimi kuingilia kiwanjani kwangu yani kama ni nyumba itajengwa basi njia ya mimi kuingia nyumbani kwangu itabidi iwe hapo sasa ikabidi nimfate na kumuuliza KULIKOONI na jamaa akanitolea ramani yake ya mpango miji ikionyesha kua kile kiwanja changu ni kiwanja kisicho kua na njia na kua ile ramani niliyopewa na jamaa aliyeniuzia ni fake japo inafanana asilimia 98 na ramani halisi ya eneo lile kwa kua kasoro iliyopo ni hicho kipande cha njia tu ndio kime editiwa kutoka kwenye ramani halisia.

Naombeni mnishauri nini naweza kufanya maana nilivyo enda serekali za mitaa nilionyeshwa ramani na nikapewa copy ikionyesha kua njia itafika mpaka ndani ya eneo langu kumbe sivyo huyu jamaa kanifanyia usanii.Naombeni kujua nini natakiwa kukifanya maana najaribu kumpigia jamaa kuhusu hili ila kila tukiongea ananiambia nipe muda kidogo walau wiki ntakuja tuta yamaliza lakini naona kila ifikapo hiyo wiki ninapo mtafuta ana leta usanii sanii tuu na sasahivi hapokei simu zangu kabisa ndugu na rafiki zangu wakaribu wananiambia nirudi kuwaeleza serekali ya mtaa kilicho tokea kupitia baraza la ardhi ili wamuite tujadili maana alipo niuzia kiwanja ramani aliyonipa na aliyotoa serekali yamtaa ilikua ikionyesha njia inafika mpka kwenye kiwanjani sasa sahivi nagundua ilikua ni mchezo ,jamaa nyumbani kwake ni meter 100 tu kutoka hapa kwenye kiwanja lakini kila nikija sight ananikwepa hatuonani na naambiwa huwa yupo tu kila siku saa 10 anakua kashatoka kazini yupo mtaani watu wanamuona,Naombeni mnishauri nifanyeje
Nenda wilayani ofisi ya ardhi ili upate ramani ya eneo husika. Hakikisha unapewa the most current one, kwa sababu kuna kubadilishwa kwa michoro kila uchao na hawa jamaa ukiwapa pesa tu wanafanya "amendment".

Katika michoro yote halali ya makazi rasmi, kila kiwanja (plot) lazima kiwe na barabara angalau upande mmoja. Ukiona ramani ya mipango miji ina plot ambayo haina barabara hata upande mmoja, nenda wizarani uka-dispute uhalali wake, na uweledi wa town planner. They will settle with you.

Nakusisitizia tena, kama una registered plot number bila njia hata upande mmoja, basi hiyo plan siyo halali kwa makazi, na hakuna namna eti zijengwe nyumba kukuzunguka wewe bila kuwa na njia.

Pia, nahisi kuna njia kenye ramani ila wewe unajichagulia njia unayoitaka wewe. Hii nishawahi kukutana nayo na ni mtu mkubwa serikalini nikamtolea nje kisa anataka nichangie kwenye njia. Nikaombwa na planner wa halmashauri nikatoa nje nikaomba permit ya fence, nikaipata kwa mbinde nikaweka ua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom