Naomba ushauri katika kuagiza gari. Je, nitumie mitandao mikubwa au niende kwa dealers

afrique

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
509
135
Habari zenu,

Nataka kuagiza gari naona hata hao makampuni ya kuagiza wanacwanachukua picha za beforwad na Japanese autocom.

Sasa si heri ninunue tu huko beforwad au autocom!

Ushauri wenu experts na experience zenu zitanisaidia
 
Nunua kwenye hayo Makampuni makubwa kama Beforward, Japanese, SBT, hata mimi naagiza kupitia hizo Kampuni. Najua watakuja na mapovu kwenye hii thread.
 
Nenda/agiza mwenyewe. Omba aina mbali mbali (idadi kubwa) ya aina unayoitaka. Mfano Kama umetaka Premio. Waambie wakutumie mawili, matatu au zaidi. Hata hivyo si lazima utakapotumiwa, si lazima ununue hilo hilo. Jipe muda wa kujielimisha Kama linakidhi mahitaji yako.

Jielimishe kuhusu ushuru wa gari hilo. Magari yanaweza kuwa na mwonekano ule ule lakini ushuru tofauti. Watu wengi wanaumizwa na hili na wengine kuishia kushindwa kuyaondoa bandarini. (ingia tra calculator for used vehicles).

Nimewahi kununua na kununulia wengine magari kwenye kampuni zote kubwa. Hivi sasa naona kampuni bora ni SBT. Usiafiki mtu yeyote kukufanyia malipo. Fanya/kamilisha miamala wewe mwenyewe kwa jina lako. Hakuna ugumu wala usumbufu. Gari la nje unakuwa na hakika ya kutumia muda mrefu.

Nilinunua 2013 nikaanza kutumia 2014 lakini hadi leo sijagusa injini hata maji sijaweka mapya ingawa nimeshatembea zaidi ya km.100,000.
Bei utakayopewa si lazima kuikubali. Omba punguzo.
Nakutakia kila la heri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda/agiza mwenyewe. Omba aina mbali mbali (idadi kubwa) ya aina unayoitaka. Mfano Kama umetaka Premio. Waambie wakutumie mawili, matatu au zaidi. Hata hivyo si lazima utakapotumiwa, si lazima ununue hilo hilo. Jipe muda wa kujielimisha Kama linakidhi mahitaji yako...
Umempa ukweli, nimevuta kitu mwezi january toka sbt japan kama kilivyo kwenye mtandao ndivyo nilivyoletewa hata ushuru ikawa hiyohiyo.La kuongezea unapoagiza gari uwe na subira ya kutosha wanaosema mwezi 1 au siku 40 ni waongo.
 
SBT na be forward Wana ofisi zao hapa Tanzania. Kama unataka kuagiza gari Bora ufanye biashara na hizo kampuni mbili
 
SBT na be forward Wana ofisi zao hapa Tanzania.
Kama unataka kuagiza gari Bora ufanye biashara na hizo kampuni mbili

Faida ya kuagiza gari mwenyewe unapata discount kubwa..ukienda kwenye hayo maofisi unapigwa bei hata discount utapewa ya kishikaji tu lakini ukikomaa mwenyewe discount inafika hadi dola 500 kutegemea na T&C applied.
 
Be forward nao wanakuwa na punguzo kuanzia USD 200-300
 
Ni heri ukaagiza tu mwenyewe, na kuna makampuni kama Sbt, enhance ama be forward. Wapo vizuri sana.

Kipindi fulani, kuna mtu aliwahi kuagiza ila changamoto ikawa ni namna sasa ya kulipa ushuru wa hiyo gari.

Katika kuhangaika huku na kule, akakutana na mtu ambaye huwa anasaidia kwenye ulipaji wa ushuru, halafu wewe unamrejeshea kwa awamu mbili.
Ila waliandikishiana, na gari kama sikosei jamaa alielipiwa ushuru alibakia nayo.
 
Hakikisha unaagiza mwenyewe. Heshimu/zingatia kikokotozi cha ushuru cha TRA. Unaweza pia kupata ushauri wa ziada humu jamvini au kwa mawakala wa kutoa mizigo bandarini.

Kama huwajui tushirikishe tukueleze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umempa ukweli, nimevuta kitu mwezi january toka sbt japan kama kilivyo kwenye mtandao ndivyo nilivyoletewa hata ushuru ikawa hiyohiyo.La kuongezea unapoagiza gari uwe na subira ya kutosha wanaosema mwezi 1 au siku 40 ni waongo.
Hii ni kweli, watu husema siku 45 tu lakini utasubiri hadi miezi miwili ndio kitu kitimbe mjini, patience is needed.
 
Vp Kama mtu atanitumia zawadi ya gari toka America ,& Germany anaweza ituma pitia kampuni na ushuru wake unakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushuru haujali gari umelipataje. Unazingatia thamani ya gari kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hi Ina maana kuwa ushuru utakokotolewa kwa kuzingatia thamani ya gari kwa mujibu wa Mamlaka. Mamlaka haikokotoi ushuru kwa kuzingatia bei uliyonunua.

Kampuni ya kukuletea haina ugumu. Waweza kuitafuta ama huyo anayekuzawadia huko aliko au wewe kwa kuwasiliana na wakala wa huku kwetu
.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kweli, watu husema siku 45 tu lakini utasubiri hadi miezi miwili ndio kitu kitimbe mjini, patience is needed.
Mara nyingi hazizidi siku 45 ingawaje zinaweza kuzidi au kupungua. Hii ni kwa sababu baada ya kununua gari wanaanza kutafuta meli iliyo na nafasi, ikiwaninapita hapa kwetu.

Pia wanaangalia nafuu ya gharama za usafirishaji. Sijawahi kuagiza gari likazidi siku 45. Hata hivyo kukawia ukapata kitu bora ji tofauti na kuharakisha ukapata boga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naweza kukufata DM kama hutojali?
Mara nyingi hazizidi siku 45 ingawaje zinaweza kuzidi au kupungua. Hii ni kwa sababu baada ya kununua gari wanaanza kutafuta meli iliyo na nafasi, ikiwaninapita hapa kwetu.
Pia wanaangalia nafuu ya gharama za usafirishaji.

Sijawahi kuagiza gari likazidi siku 45. Hata hivyo kukawia ukapata kitu bora ji tofauti na kuharakisha ukapata boga.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko Zanzibar kikazi na familia iko Dar, nataka kuagiza gari kutoka nje ili niipeleke Dar kwa wife. Ipi ni njia nzuri, kuagiza kupitia Zanzibar au Dar moja kwa moja kwa zingatia terms na conditions za TRA?

Msaada tafadhali kwa wenye ufahamu wa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom