Naomba ushauri: Kati ya Kluger V na Harrier ni gari ipi ni nzuri zaidi?

Wakuu, nimejipanga kwa muda wa kutosha na sasa naona naweza kujipatia usafiri wangu wa kueleweka. Kuna gari hizi mbili zote nazipenda sana. Naomba kushauriwa na wenye uzoefu na uelewa mkubwa wa hizi gari mbili ni ipi wanaona ni nzuri zaidi? Suala la mafuta sio tatizo, lakini uimara wa gari na hadhi ya gari na gharama ya gari. Nimetenga bajeti ya milioni ishirini na tano mpaka thelathini kwa mchakato wote.

Karibuni tushauriane.
Kwa nijuavyo Harrier na Kluger:

Ni kitu kimoja, ukiwa na Kluger, jua kwamba ni sawa na una Harrier tu maana ni gari ile ile tu, ila wameitofautisha kwenye muundo wa nje tu pamoja na majina basi!

Lakini kila kitu ni kile kile yaani. Kuanzia engine capacity & machenically etc

So, ni wewe tu uchague ni aina ya muundo unaouopenda. (I mean, muundo wa Harrier au Kluger)

By the way, okoa fedha nyingi kwa kununua gari yoyote unayohitaji kupitia ecarstanzania
Sisi ni waingizaji wa magari bora na kwa gharama nafuu kabisa.

Tupo Kinondoni, Ada Estate.

Email : ecarstanzania@gmail.com

Karibu
 
Mkuu, siku hizi kuna Subaru Forester SUV, engine 2.0L iko juu kama Kluger.
Tatizo lingine la Subaru ni kuwa se-sale value yake iko chini. Kwa hiyo siku ukitaka kubadilisha gari, litanunuliwa kwa bei ya chini.
 
Nimewahi panda Kluger, Harrier sijawahi. Ila kwa muonekano zile Harrier new model zinaita sana
Hivi hizi new model zinaanzia mwaka gani? Je bajeti yangu ya 30M itaweza kunipa hiyo new model lakini kilometa zake zisizidi 100,000?
 
MAGARI7, Hapo umetupa kitu tofauti ambacho sikuwa nakifahamu kabisa! Ina maana tofauti ya Harrier na Kluger ni body tu? Zina injini sawa, gear box sawa, nk? Hebu fafanua kidogo. Ina maana kwa kiasi kikubwa hata spea zake zinaingiliana?
 
Hapo umetupa kitu tofauti ambacho sikuwa nakifahamu kabisa! Ina maana tofauti ya Harrier na Kluger ni body tu? Zina injini sawa, gear box sawa, nk? Hebu fafanua kidogo. Ina maana kwa kiasi kikubwa hata spea zake zinaingiliana?
Trust me, hizi Harrier na Kluger, kila kitu ni kile kile, kuanzia engine na kila kitu. Wametofautisha majina na muundo tu basi.
 
Kluger nadhani huwa zina gia 4, so expect fuel consumption to be high. For me Harrier ndio mpango mzima haza zile zenye engine ya vvti
Kluger 4 ni very economical kwenye mafuta, ina piston nne! Sawa na Carina
 
sina gari sijawai kumilika hata baiskeli ina hamuwezi kuamini ni magari machache sana sijawai kupanda.yaani machache . hizi lift hizi saa zingine ukute kuna watu wanaiba nyota yangu ya kumiliki gari wakinipa lift.kwanini nipande magari makali makali ya wenzangu na kuishia kupiga honi tu na kupungia watu? why?
Kwa sababu unawakimbia
 
Kasimame pale Tazara au Magomeni au Salender Bridge. Angalia gari ipi kati ya hizo zipo nyingi barabarani, Nunua hiyo. Harrier wamemuacha mbali sana Kluger. Kluger haina mvuto, bodi yake ni kama gari ndogo tu (saloon).
 
Tupa kule, mzigo huo hapo ushidwe wewe.

59356677_2330970973892487_2495554008847866652_n.jpeg
 
Mrejesho: Baada ya kupitia post nyingi humu na kwa kuzingatia ushauri wa family members tayari nimeshanunua Kluger V nyeusi: Cylinder 6, CC 3,000. Nimeshaitumia kwa zaidi ya miezi 5.

Kwenye highway haitumii sana mafuta, japo huwezi kuilinganisha na utumiaji mafuta wa gari ndogo. Kwenye mizunguko ya mitaani na mjini hapo ulaji wake wa mafuta uko juu kidogo. Ila nimeipenda sana na sijajuta.

Nashukuru sana kwa michango yenu.
 
Back
Top Bottom