Mkuu sijakusoma!!SMH....
Michango ya wataalam imeniacha hoi.Mkuu sijakusoma!!
Daah yaani BMW unailinganisha na vitu vya kijinga?
HahaaaDaah yaani BMW unailinganisha na vitu vya kijinga?
Duh!Nunua BMW tu kama una pesa za service na spare parts,,. Nina experience na vw aisee siwezi kumshauri mtu anunue. It's the worse car kuwahi kuimiliki manake taa ya check engine ilikua inawaka kila wiki na gari inashinda garage kuliko home. Usiombe DSG transmission ianze kusumbua, hainaga fix ni msiba. Kwa mtu anaetaka kununua vw beware,,.
Yani jamaa unachambua hizi gari hadi raha.Ni vitu 3 ndivyo vinavyowafanya binadamu kuamua ktk manunuzi au machaguo yao ya vitu
1 Brand name
2 Models
3 Performance
Brand name kigezo kikubwa cha kuuza bidhaa au kitu ni brand name yake hii ndio inayoongoza kwa kuuza bidhaa mfano kwenye nguo,simu,viatu,etc kwenye magari watu wengi wananunua magari kwa kufata brand names mfano Tanganyika brand name tunayonunua sana ni TOYOTA mtu akinunua toyota anaona kama spare zitapatikana kwa wepesi sana kumbe sio ni mazoea tu na kwa kenya ni NISSAN
Models hii ndio kigezo cha pili cha kuuza bidhaa au kitu watu wananunua vitu sana kutokana na model ya hyo bidhaa mfano ww umechagua subaru legacy B 4 na BMW 3 series za mwaka 2006 japo zipo subaru na bmw nyingi na za model mbalimbali
Performance hii ni hatua ya tatu ktk ununuzi au kuuza kwa bidhaa au kitu hii mala nying waafrica hatuijali sana lakini kwa wenzetu wanaijali sana mfano leo unataka kununua kitu kwa matumizi gani na matumizi yako yataitaji Performance gani ya hyo ndo maana kwenye gari kuna aina ya Performance kwa matumizi yake
Sasa inategemea kwa ww unaangalia nini ktk kununua magari hayo
1 brand name kwa maswala ya BN BMW is best
2 Model zote ni sawa kwani zote ni sedan na mwaka 2006 So hapo ni 50/50
3 Performance sasa inategemeana unataka Performance ya upande gani
A Stability & Maneuverability BMW is best
B speed Subaru is best
the choice is urs
aiseeBMW The Best
Dah! inanitoa udenda aiseee ila ngoja nikomae kujichanga nichukue SubaruBMW The Best
hiii ni kama tsh ngapi hiviBMW The Best
Kwa hiyo unanunua gari kwa ajili ya heshima mtaani?!Hahah kweli chief ndio maana wanaiita BLOW MY MONEY(BMW) kama huna huna fat wallet usijaribu Bmw,lkn ile gari ni heshima mtaani aisee.
Katika magari ambayo mjapani kayatengeneza aina ya sedani yenye comfortability yenye wazifa wa magari ya ulaya ni Toyota Crown mengine ni kawaida tu labda yale yanayouzwa Ulaya na Marekani kwani mjapani anatengeza magari kwa ajiri ya masoko ya Ulaya na Marekani lakini majina yanatofautiana na majina ya huku lakini muonekeno wa gari ni sawa sawa
BMW 3 series na Subaru legacy b 4
FUEL CONSAMPTION
Magari mengi ya ulaya ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana ila yanatumia umeme ktk ops zake nying tofauti na magari ya japani so ktk swala la mafuta BMW ni best kwani
BMW kama gari aina tatizo lolote ktk mfumo wa mafuta ni 15 km/1 liter na full tank yake ni 57 liter so unaweza kwenda Km 855 kwa full tank
Subaru legacy b 4 kama aina tatizo ktk mfumo wa mafuta ni 8.9 Km/1 liter na full tank yake ni 64 titer so unaweza kwenda Km 569.6 kwa full tank
So umeona matumizi ya mafuta BMW 3 series is the best
SPEED
bmw
Transmision =6 speed outo
Horsepower @ RPM = 215@6250
Torque @ RPM = 2750
0-60 time = 6.7 sec
subaru legacy b 4
Transmision= 6 speed outo or manual
Horsepower @ RPM = 243@6000
Torque @ RPM =3600
0-60 time= 4.5 sec
Note RPM ni revolutions per minute inapatikana kwenye dashbord na inakazi ya kuonyesha speed ya engine kwa dakika
So katika speed subaru legacy is best
SPARE PARTS
katika ulimwengu huu hofu ya kuogapa kununua gari kwa kuhofia spare ilishakwisha hofu iliyobaki ni kupata mafundi wazuri wa gari tu spare unaagiza leo baada ya siku 3 au 4 umeshaipata
KUDUMU
kudumu kwa gari inategemea utunzaji na matumizi yako pia barabara unazotumia pia na uendeshaji kwani nimegundua Tanganyika madereva ni wachache sana ila waendeshaji wa magari wapo wengi unaweza jiuliza watu wanaagiza gari za mpaka miaka ya 1990 japani au Ulaya lakini zinaonekana mpya ikifika huku ndo zinachakaa pia hali ya hewa Africa inatuangusha sana gari aipatani na joto
KUTULIA BARABARANI
kuna kutulia barabarani kwa aina mbili
1 Stability ya gari
2 Maneuverability ya gari
BMW ikikimbia na kufika speed kuanzia 100 inashuka chini na ni kama ilivyo benz na unaruhusiwa kukata kona kali hata ukiwa na top speed ya 80Kmh
Subaru inakimbia sana lakini ipo kama Toyota Altezza na unaruhusiwa kukata kona kali hata ukiwa top speed ya 50 kmh zaidi ya hapo do @ your own risk