abdulhamis
JF-Expert Member
- Aug 2, 2019
- 1,436
- 2,292
Habari wadau wa JamiForums,
Mara nyingi huwa napenda ku-share mambo ili niweze kupata mawazo kutoka katika akili tofauti tofauti ili nipate majibu mengi tofauti na jibu ambalo huwa ndio limejibiwa na wengi basi huwa naliangalia na mimi tena kwa umakini then nalifuata.
Mimi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 27 nimebahatika kupata mtoto mmoja nampenda sana na mimi kama Baba nataka nijitaidi kuwa Baba bora kwa Mtoto wangu kwa kusimamia kila kitu.
Nimekuja kwenu kuwauliza fikra zenu juu ya Malezi ya mtoto yatakayo kua Mazur kwa kwa afya yake ya mwili mpaka akili.
Kuna malezi aina mbili tuliyo nayo.
Moja ni malezi ya wazazi wa Kiafrika ambayo yana sifa nyingi sana nzuri na mbaya na malezi haya ndio niliyolelewa hata mimi moja ya mambo ambayo yalikuwa ni msingi katika malezi ya mtoto na ilikuwa lazima afuate zikiwemo sheria za kama mkubwa hakosei mtoto kwa wazazi hakui, mtoto haombwi msamaha, na mtoto hayupo huru kufanya jambo kisiri bila wazazi kujua
Malezi ya wenzetu wazungu kwanza mtoto anakua free Sana, mtoto akitaka kufanya kitu kwa wazazi anaomba ushauri tu na wala sio ruhusa pia mtoto akifiksha miaka 18 basi wazaz mkimuingilia kwenye mambo yake anaweza hata akawashtaki.
Pia mimi kama Baba kumwambia Mtoto wangu nakupenda ni sawa au kumuomba radhi mtoto wangu.