Naomba ushauri juu ya mfanyakazi wa duka la copy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri juu ya mfanyakazi wa duka la copy

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by wanan, Mar 14, 2012.

 1. w

  wanan Senior Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Nimiezi sita ss tangu nifungua duka mkoani,nimeajiri wafanyakazi wawili ila mmja hana majibu mazuri kwa wateja mpaka biashara kimapato imepungua sana.juu ya tabia yake wateja ndio wamenipigia simu sbb nimeweka business card zangu pale.pia sio mzuri katika utanzaji wa document nafikiria kuchua uamuzi wa kufukuza kazi sbb kama unavyo juwa mtaji wanyewe ni watabu mpaka nimepata wana jf nifanyaje sbb inanifanya kichwa kinauma sana.naomba ushauri kwa hili juu ya tatizo hili
   
 2. mimi05

  mimi05 Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  (kwenye red)Bado unafikiria tuu,kwa nini usichukue hatua?
   
 3. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kupata mwaminifu,mchapakazi, mkarim kwa wateja ni kazi sana.Kabla biashara haijaharibika nakushauri tafuta kijana atakayekufanyia kazi vizuri.Namshukuru Mungu nina kijana anayenifanyia kazi vizur sn.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Usiajili Mchaga dukani utalia. You have been warned
   
 5. w

  wanan Senior Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  ndio maaan naomaba ushauri mkuu,
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Suluhisho la matatizo hayo si kumfukuza kazi. labda kwanza nikuulize wewe binafsi umeshachukua jitihada gani za kutatua hayo matatizo yao, tofauti na hilo wazo la kufukuza kazi? Mkuu, mapungufu hayo yote yanarekebishika, sasa badala ya kufukuza nakushauri uwekeze katika uelewa na perfomance wa wafanyakazi wako.

  Wasipofundishika na kuelewa, na kuyakataa mabadiliko basi find her replacement, lakini nawe ubadilishe vigezo ulivyotumia kumpata huyo mfanyakazi wako
   
 7. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duka liko wapi?
   
 8. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ni PM nikusaidie...
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Tahadhari mkuu, kama mfanyakazi ni binti na jamaa ameishamla ni vigumu sana kurekebishika...

  Huenda hata kiburi na majibu ya hovyo kwa wateja ni kwa kuwa anahisi ana shea na boss wake. Dawa yake ni kufukuza tu na kuokoa biashara
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hili ni Tatizo kubwa sana kwa Watanzania wengi/wafanya biashara, Watanzania wengi tumekuwa tukijairi watu kiholela sana kisa

  1. Tunawafahamu
  2. Ni ndugu zetu
  3. Ni majirani
  4. Gilr/Boy friend

  Unapo taka kuajiri jaribu kwanza kufanya haya.
  1. Tafuta mfanyakazi ambaye ana kiasi fulani cha elimu kulingana na kazi atakayo fanya,

  2. Mpe semina ya umuhimu wa Biashara yako na mwambie hii biashara ndo itakayo endesha maisha yako na yangu

  3. Mpatie elimu ya kuwahudumia wateja, kama huna elimu hiyo tafuta kampuni au NGOs zinazo dili na elimu ya Ujasiriamali wambie wakufundishie wafanya kazi wako jinsi ya kuwahudumia wateja,
  - Hapa usiogope kutoa pesa mkuu ni lazima utoe pesa ili wafanya kazi wako wapate orientation nzuri sana

  4. Mpatie elimu ya kutenganisha Mambo binafisi na Biashara, mwambie biashara haichanganywi na kitu chochote kile na inajitegemea kama biashara.

  KWA KIFUPI USIAJIRI MTU LEO NA KESHO UNAMKABIDHI OFISI NA MATOKEO YAKE NI HAYA

  1. Wafanyakazi kutimia muda mwingi sana kusoma magazeti ya Udaku kazini

  2. Muda mwingi ni kuchati na simu

  3. Kuweka Headphone masikioni

  4. Kupiga story za umbea na marafiki zake maeneo ya kazi

  5. Kutembelewa na wageni muda wa kazi

  6. Kuto kuwa mchangamfu wakati wa kuwahudumia wateja

  Haya na mengine mengi sana yanasababishwa na waajiri na si wafanya kazi, kwa sababu hukumpa elimu yoyote ya jinsi ya kudili na wateja, ya jinsi ya ku keep time, jinsi ya kupunguza ghalama za kuendesha biashara na kazalika
   
 11. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,333
  Likes Received: 6,675
  Trophy Points: 280
  vitu vingine havihitaji ushauri!!!kama wewe ushaona anatofautiana na wateja unachukua hatua mara moja!!!au ana hisa kwenye hiyo biashara!!!!USIMFUKUZE!
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hayo yote na mengine mengi, kama aliyoyasema Chasha yalikuwa kichwani, ndio maana nikasema
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Mfukuze of course ila fuata taratibu za kisheria za kumfukuza mtu.
   
Loading...