Naomba ushauri juu ya matumizi ya mbolea/ samadi katika uzalishaji wa mchicha

EZZ CHEZZ

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
1,230
1,352
Hello JF.

Nimeanza uzalishaji wa mchicha lishe miezi michache iliyopita hapa Kyela mjini. Takribani kola kitu kinaenda sawa. Mimi hutumia samadi na kuvuna mchicha kila baada ya siku 15 - 20.

Sasa nimeanza kupata changamoto kwenye upatikanaji wake. Mbali na kutumia muda mwingi kuzunguka kwenye mabanda ya watu ambao wengine huiuza, sasa tunaelekea masika ambapo kuipata itakuwa shughuli.

Hivyo ninaomba ushauri/maarifa na uzoefu juu ya matumizi ya mbolea za dukani.

Je ni sahihi kutumia?
Gharama zake zikoje?
Ni mbolea gani hasa?
Zinatumikaje?
Vipi kuhusu ubora wa mazao?
Athari zake kwenye udongo ni zipi?

Nawasilisha.
 
Pichani ni kama,
IMG-20191020-WA0009.jpeg
 
Mkuu unaweza kufuga mbuzi ukatumia mbolea yake maana hata garama za uendeshaji wa mbuzi ni ndogo

Pia unaweza kufuga kuku na mbolea ukaitumia

Kuhusu mbolea ya dukani wengi wanatumia KAN ndio huwa wana rushia siku ya sita toka kupandwa kwa mbegu
 
Komaa na samadi, mahitaji ya soko la sasa ni mbogamboga na matunda yanayozalishwa kwa kutumia mbolea na madawa ya asili. Ukiwaelewesha wateja gharama za uzalishaji wa kilimo hai watakuelewa na kukupa bei nzuri yenye faida.
 
Ahsante. This is taken.
 
Asante kwa ushauri, japo mimi cjauliza swali. Kwa faida ya wengine ana changamoto 2. Moja ni upatikanaji haswa kipindi cha mvua kinachokuja na shida ya pili ni utunzaji wa mbolea hyo asili?
Komaa na samadi, mahitaji ya soko la sasa ni mbogamboga na matunda yanayozalishwa kwa kutumia mbolea na madawa ya asili. Ukiwaelewesha wateja gharama za uzalishaji wa kilimo hai watakuelewa na kukupa bei nzuri yenye faida.
 
Weka na mborea inaitwa CAN utarudi kunishukuru nakwambia.
mimi pia nalima mchicha lishe unanilipa balaa naweka mbolea ya broiler baada ya wiki 2 napiga urea basi unanawili afu unarefuka nikipereka sokoni unaisha kwa dk 20 urea kg 25 ni sh 30
 
EZZ CHEZZ naam unaweza kutumia mborea aina ya UREA pamoja na CAN hizi unachanganya kwa pamoja kisha unafanya kurushia kwenye tuta lako. Mborea hizi zina matokeo mazuri mno, zote kwa pamoja zinasaidia mmea kukua na kunawiri vizuri mno. Zote kwa pamoja Kilograms 25 ni Tsh 30,000 kama utahitaji ni pm.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu. Hiyo mbolea ya briler ndiyo ipi na huwekwa kabla au baada ya kurusha mbegu?
 
Umetisha mkuu. Mchanganyiko huu unawekwa tutani siku ya ngapi? Pia kiasi hicho chafaa kwa eneo la ukubwa gani?
EZZ CHEZZ naam unaweza kutumia mborea aina ya UREA pamoja na CAN hizi unachanganya kwa pamoja kisha unafanya kurushia kwenye tuta lako. Mborea hizi zina matokeo mazuri mno, zote kwa pamoja zinasaidia mmea kukua na kunawiri vizuri mno. Zote kwa pamoja Kilograms 25 ni Tsh 30,000 kama utahitaji ni pm.
 
Mmhh! Mbolea ya chumvi chumvi na mboga za majani ?
CAN na urea zinakiwango kikubwa cha nitrojeni ambayo ni sehemu muhimu ya amino acids zinazojenga mmea na kuufanya ukue kwa haraka.

Ikumbukwe kuwa tunachohitaji kwenye mboga ni majani hivyo majani mengi yanaondoa kiasi kikubwa cha nitrojeni udongoni ambacho kinarudishwa kwa kuweka mbolea ikiwemo hizo za chumvi.
 
Hizo mboga zilizotumia Mbolea ya kiwandani haziliki.

Ladha inakuwa sio.
 
EZZ CHEZZ naam unaweza kutumia mborea aina ya UREA pamoja na CAN hizi unachanganya kwa pamoja kisha unafanya kurushia kwenye tuta lako. Mborea hizi zina matokeo mazuri mno, zote kwa pamoja zinasaidia mmea kukua na kunawiri vizuri mno. Zote kwa pamoja Kilograms 25 ni Tsh 30,000 kama utahitaji ni pm.
Bei yake kwasasa ni kasheshe
 
Back
Top Bottom