Naomba ushauri juu ya huyu trafiki

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,559
21,036
Jana nilikuwa nasafiri kutoka Dar kwenda Moro njiani maeneo ya karibia na Moro kwenye ofisi za TAFORI nilikamatwa na trafiki akaniambia nilizidisha speed maeneo ya Kingulwira na kuna askari alinipiga tochi.

Tulikamatwa kama magari 10 hivi ingawa mimi nilikuwa makini sana na spidi na nina uhakika sikuzidisha kwani hiyo sehemu aliyonitajia nilisimama kuangalia eneo langu kisha nikaendelea na safari

Je katika hali hiyo ni sahihi kumkamata mtu eneo ambalo kwenye camera ( ililetwa baada ya kugoma kulipa hela). Halionyeshi exactly ni sehemu gani maana hakuna nyumba na hakuna uthibitisho kama hiyo picha ilipigwa sehemu hiyo au lah. Nililipa hela faini baada ya kuona wameshikilia leseni yangu kwa saa nzima na mimi nilikuwa na haraka.

Askari aliyepiga picha hakuwa na unifomu na pia ndio aliyeniandikia faini. Nachofanya nataka nikamshitaki kesho natafuta ushauri wa kisheria maana aliandika jina lake na sahihi kwenye ile notification ambayo pia nitaenda kuikatia risiti.

Dhumuni la kumshitaki ni kukomesha uonevu huu
 
Ushauri wangu kwako kuwa shauri lako litatupiliwa mbali maana ulishakili kosa ndiyo maana ukalipa faini .pia askari kuwa kiraia ni moja tu ya mbinu za kipelelezi ili kukamata wahalifu.kumbuka kukubali kulipa faini ni kukiri kosa kama usingeridhika ungekataa ili mfikishane mahakamani.
 
Ushauri wangu kwako kuwa shauri lako litatupiliwa mbali maana ulishakili kosa ndiyo maana ukalipa faini .pia askari kuwa kiraia ni moja tu ya mbinu za kipelelezi ili kukamata wahalifu.kumbuka kukubali kulipa faini ni kukiri kosa kama usingeridhika ungekataa ili mfikishane mahakamani.
Lakini si kwa trafiki mkuu na utaratibu upo wazi trafiki hawezi kukusimamisha akiwa hajavaa uniform
 
Ili ithibituke kwamba umetenda kosa la kuzidisha mwendo....
Kwanza ni lazima uoneshwe picha yenye kithibitisho cha wazi kwamba ulikua meendo mfano 70 with 50 k/h area.
Na ili uweze kusimama, lazima askari awe amevalia sare za polisi wa usalama barabarani unless eneo ilo pawe na roadblock.
 
Ulikosea kulipa fain

Nenda Takukuru wakupe pesa zao
Pita hapo hivyo hivyo wakikumata wahonge pesa za Takukuru tu

Kingine usitembee na leseni original
Tembea na copy
 
Back
Top Bottom