Naomba ushauri juu ya huyu boss

WAR

Member
Dec 16, 2016
49
36
Ni jitiahad zipi zilikufanya kumshawishi mwajiri wako kuweza kukupandisha cheo?
 
Mimi ni mwajiliwa wa taasisi fulani inayohusika na maswala ya ununuzi, nimeajiriwa tangu mwaka juzi. Tatizo nililonalo ni huyu boss wangu amekuwa ni mtu wa hasira sana ukikosea kidogo tu lazima achukue siku nzima kukusema na yupo radhi hata wekeend akupgie simu mtoke wote ila mkifika kwanye huo mtoko lazima akuanzishie mambo ya ofisini na kukusema tena kibaya zaidi ukimjibu ndo anazidisha mara ooh mpumbavu we hutumii akili yani inshort napata wakati mgumu natamani kuacha kazi ila nashindwa kwan familia inantegemea.

Nimejiuliza kwa watu wake wakaribu wanadai sio wewe tu ndivyo alivyo kwani ni mtu anayeamini yuko sahihi kwa kila kitu na pia jeuri ya fedha inampa kiburi

Tafadhari naomba ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuendana na huyu boss wangu.
Acha kazi
 
Tatizo unafikiri ukiacha kazi hapo unahisi hutopata kazi kwengine
dawa yake unampa mitusi ili aone hujali.

au kama bosi demu anakutaka
 
Mpotezee, mradi watoto wanaenda chooni... Stress zake anamalizia kwenu, jifanye kama hujali piga kazi kila sehemu mabosi wana shida zao.
 
Pole,wapo watakaokubeza ila yakiwafika watakumbuka post yako na kuja kusoma ushauri uliopewa. Maboss wa namna hiyo wengi ni attention seeker. Na anataka awe juu tu. Hivyo ili uendane nae inabidi uishi kama mtumwa.
 
DC hapi alisema kuajiliwa ni sehemu ya utumwa, kwa hiyo ukikubali utumwa vumilia, ukitaka uhuru kuwa mjasiriamali
 
Watu wake wa karibu wapi hao! Mie nadhani nyie na wewe ukiwemo mnae shinda nae nae ofisini ndio watu wa karibu.tena kwa miaka 3 uponaye ofisi moja kwa kila siku mpo nae masaa zaidi ya 9 huo ni ukaribu tosha
 
Watu wake wa karibu wapi hao! Mie nadhani nyie na wewe ukiwemo mnae shinda nae nae ofisini ndio watu wa karibu.tena kwa miaka 3 uponaye ofisi moja kwa kila siku mpo nae masaa zaidi ya 9 huo ni ukaribu tosha
Namaanisha baadhi ya ndugu zake nao waliwahi kuniuliza unaishije na boss wako, ndo ikapelekea kumjua kiundani
 
Msome hulka zake kisha uishi nae kwa jinsi alivyo. Ujue mtu ukishayajua madhaifu yake mchukulie kama mlemavu tu. Wewe mpotezee tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom