Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Hii ni serious sana.
Nina Mke na mtoto mmoja, ndoa yenu inamiaka mitano sasa, katika swala la uaminifu katika ndoa sijawahi kumhisi mke wangu kutokuwa mwanaminifu, inawezekana ni kwa sababu nimeamua hivyo au inawezekana ni sahihi kabisa kwamba ni mwaminifu mpaka nilipokutana na kitu cha ajabu majuzi.
Naposema namuamini inajumuisha ukweli kwamba,sijawahi kupata kusikia wala kuhisi juu ya tabia mbaya juu yake,kiasi kwamba sikuwahi kufikiria kumfanyia uchunguzi wa namna yoyote ile.
Kwa upande wake, naweza kusema ama haniamini au anawivu sana na mimi, hataki hata nikae na rafiki zangu, ikitokea nimefanya hivyo atanisumbua sana kwa simu na kunikera kiasi cha kufanya hata hayo mazungumzo nayofanya kuwa hayana maana, sababu concentration inakuwa zero kwa ajiri ya kujieleza niko wapi,niko na nani,nafanya nini,kwa nini tuwe hapo na tusiende nyumbani,narudi saa ngapi, na vitisho vingi, na mimi natoka, na mambo mengine mengi tu, haiishii hapo nikirudi nyumbani ndio inakuwa tabu ni ugomvi usio wa kawaida. for five years now.Hiyo ni tisa.
KUMI
MATUMIZI YA PESA
Sijui nilielezeje hili. wakati namtongoza, nilimuona kama mtu mmoja makini sana kwenye mambo ya pesa, kwanza hakuwa tayari tutumie pesa nyingi tukiwa nae, kuna siku tulienda disco tulipotoka disco tukaenda kulala Kilimanjaro kemplinski, kesho yake ilileta ugomvi mkubwa sana, kwamba ninamatumizi makubwa na mabaya ya pesa ukizingatia tulipokuwa disco (maisha club) nilikutana na marafiki kadhaa nikawapiga pombe vibaya sana, so aliweza mpaka kunieleza kwenye pombe tu tumetumia kiasi gani (alichukua bili zote nilizolipia).
Na katika swala la Pombe akanilazimisha niache, nami nikapunguza kiasi.
Kabla ya Kufunga ndoa, tayari nilikuwa na maisha safi kabisa, nasomesha ndugu zangu, nimejenga nyumba yangu LockCity na nikawa naendeleza kiwanja viwanja viwili DAR.
Baada ya Kufunga ndoa, kila kitu kikasimama.
Nyumba moja niliyokuwa najenga, nilimpatia bwana mdogo wangu aimalizie alafu akae yeye, mimi nikaendelea kupanga nikiamini with my economist wife, ntamalizia hiyo nyumba nakuamia ndani ya mwaka mmoja. wapi, hiyo nyumba nimeishia kuiuza mwaka huu.
PESA ZINAKWENDA WAPI.
Nampa yeye, kwanza nilimpa kazi ya kusimamia hiyo nyumba iishe, kwa mantiki kwamba ni nyumba yake,aimalizie kwa namna roho yake inavyopenda na kuifurnish kwa umaridadi wa aina anayoiota yeye.
Kwanza alianza kunieleza anazungusha hizo pesa, na kweli nyumbani akawa na mahela mengi kwelikweli, japo nilikuwa namkanya, lakini aliendelea kusisitiza kwamba biashara anazofanya zinahitaji awe na pesa wakati wote, anakaa na zaidi ya milioni ishirini ndani, anatembea kwenye gari na si chini ya milioni tano, nikastudy biashara husika nikaona kuna ukweli wa kuhitaji kuwa na pesa mkononi, lakini nikimuambia tukae nimsaidie kupiga hesabu tujue anapataje faida anakataa tena anakuwa mkali kwelikweli.
Mwisho wa siku, ananiletea story inayoonyesha kwamba kuna watu wanachelewa kumlipa pesa zake, namuongezea, wakati huo asilimia themanini ya mshahara nampatia.
Ni mengi Jamani, kuna mambo positive anafanya, lakini ndio kama kubadirisha thamani za ndani,kubadirisha gari,n.k
Mwaka huu mwezi wa saba, nikaachana na mambo ya kuajiriwa, nikaanza kufanya mambo yangu mwenyewe, niliamini kwamba, mambo ya chakula, nyumbani hayawezi kumshinda, pango la nyumba siwezi kushindwa kulipa.
Mwaka huu nikapata matatizo ya kiafya, nikalazimika kuuza haraka sana nyumba iliyokuwa haijaisha (ambayo alishindwa kuiendeleza kwa asilimia zaidi ya tisini), nikauza na kiwanja changu, magari mawili niliyokuwa natumia, nasikia gari analotumia yeye ambalo ndio lenye thamani kubwa kulinganisha na yale niliyokuwa natumia mimi alikataa kuuza, japo ndilo nilimuelekeza aliuze nikijua litauzika kwa haraka, yeye aliniambia hakuna mtu aliyejitokeza japo kuliulizia.
Naomba msaada, najua atapita hapa kusoma na ataelewa ni mimi nimepost, na namzungumzia yeye, lakini kwa kweli kabisa, nafikilia kulifikisha swala hili kwa wazazi na ndugu zangu ndani ya wiki mbili hizi nikiwa mwanza, nafikiria kuachana na huyu mwanamke.
Nimeamua kulileta hili hapa, kwanza ili kupunguza pressure na hazira nilizonazo, na zaidi kupata ushauri usioegemea upande wowote, sababu najua nilifikisha home, uwezekano wa kupita hata bila kujadiliwa ni asilimia zaidi ya mia, na nimejizuia kufanya hivyo kwa muda mrefu nikijua matokeo ndio yatakuwa hayo.