Naomba ushauri jamani

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Hii ni serious sana.

Nina Mke na mtoto mmoja, ndoa yenu inamiaka mitano sasa, katika swala la uaminifu katika ndoa sijawahi kumhisi mke wangu kutokuwa mwanaminifu, inawezekana ni kwa sababu nimeamua hivyo au inawezekana ni sahihi kabisa kwamba ni mwaminifu mpaka nilipokutana na kitu cha ajabu majuzi.

Naposema namuamini inajumuisha ukweli kwamba,sijawahi kupata kusikia wala kuhisi juu ya tabia mbaya juu yake,kiasi kwamba sikuwahi kufikiria kumfanyia uchunguzi wa namna yoyote ile.

Kwa upande wake, naweza kusema ama haniamini au anawivu sana na mimi, hataki hata nikae na rafiki zangu, ikitokea nimefanya hivyo atanisumbua sana kwa simu na kunikera kiasi cha kufanya hata hayo mazungumzo nayofanya kuwa hayana maana, sababu concentration inakuwa zero kwa ajiri ya kujieleza niko wapi,niko na nani,nafanya nini,kwa nini tuwe hapo na tusiende nyumbani,narudi saa ngapi, na vitisho vingi, na mimi natoka, na mambo mengine mengi tu, haiishii hapo nikirudi nyumbani ndio inakuwa tabu ni ugomvi usio wa kawaida. for five years now.Hiyo ni tisa.

KUMI
MATUMIZI YA PESA
Sijui nilielezeje hili. wakati namtongoza, nilimuona kama mtu mmoja makini sana kwenye mambo ya pesa, kwanza hakuwa tayari tutumie pesa nyingi tukiwa nae, kuna siku tulienda disco tulipotoka disco tukaenda kulala Kilimanjaro kemplinski, kesho yake ilileta ugomvi mkubwa sana, kwamba ninamatumizi makubwa na mabaya ya pesa ukizingatia tulipokuwa disco (maisha club) nilikutana na marafiki kadhaa nikawapiga pombe vibaya sana, so aliweza mpaka kunieleza kwenye pombe tu tumetumia kiasi gani (alichukua bili zote nilizolipia).

Na katika swala la Pombe akanilazimisha niache, nami nikapunguza kiasi.

Kabla ya Kufunga ndoa, tayari nilikuwa na maisha safi kabisa, nasomesha ndugu zangu, nimejenga nyumba yangu LockCity na nikawa naendeleza kiwanja viwanja viwili DAR.

Baada ya Kufunga ndoa, kila kitu kikasimama.

Nyumba moja niliyokuwa najenga, nilimpatia bwana mdogo wangu aimalizie alafu akae yeye, mimi nikaendelea kupanga nikiamini with my economist wife, ntamalizia hiyo nyumba nakuamia ndani ya mwaka mmoja. wapi, hiyo nyumba nimeishia kuiuza mwaka huu.

PESA ZINAKWENDA WAPI.
Nampa yeye, kwanza nilimpa kazi ya kusimamia hiyo nyumba iishe, kwa mantiki kwamba ni nyumba yake,aimalizie kwa namna roho yake inavyopenda na kuifurnish kwa umaridadi wa aina anayoiota yeye.

Kwanza alianza kunieleza anazungusha hizo pesa, na kweli nyumbani akawa na mahela mengi kwelikweli, japo nilikuwa namkanya, lakini aliendelea kusisitiza kwamba biashara anazofanya zinahitaji awe na pesa wakati wote, anakaa na zaidi ya milioni ishirini ndani, anatembea kwenye gari na si chini ya milioni tano, nikastudy biashara husika nikaona kuna ukweli wa kuhitaji kuwa na pesa mkononi, lakini nikimuambia tukae nimsaidie kupiga hesabu tujue anapataje faida anakataa tena anakuwa mkali kwelikweli.

Mwisho wa siku, ananiletea story inayoonyesha kwamba kuna watu wanachelewa kumlipa pesa zake, namuongezea, wakati huo asilimia themanini ya mshahara nampatia.

Ni mengi Jamani, kuna mambo positive anafanya, lakini ndio kama kubadirisha thamani za ndani,kubadirisha gari,n.k

Mwaka huu mwezi wa saba, nikaachana na mambo ya kuajiriwa, nikaanza kufanya mambo yangu mwenyewe, niliamini kwamba, mambo ya chakula, nyumbani hayawezi kumshinda, pango la nyumba siwezi kushindwa kulipa.

Mwaka huu nikapata matatizo ya kiafya, nikalazimika kuuza haraka sana nyumba iliyokuwa haijaisha (ambayo alishindwa kuiendeleza kwa asilimia zaidi ya tisini), nikauza na kiwanja changu, magari mawili niliyokuwa natumia, nasikia gari analotumia yeye ambalo ndio lenye thamani kubwa kulinganisha na yale niliyokuwa natumia mimi alikataa kuuza, japo ndilo nilimuelekeza aliuze nikijua litauzika kwa haraka, yeye aliniambia hakuna mtu aliyejitokeza japo kuliulizia.

Naomba msaada, najua atapita hapa kusoma na ataelewa ni mimi nimepost, na namzungumzia yeye, lakini kwa kweli kabisa, nafikilia kulifikisha swala hili kwa wazazi na ndugu zangu ndani ya wiki mbili hizi nikiwa mwanza, nafikiria kuachana na huyu mwanamke.

Nimeamua kulileta hili hapa, kwanza ili kupunguza pressure na hazira nilizonazo, na zaidi kupata ushauri usioegemea upande wowote, sababu najua nilifikisha home, uwezekano wa kupita hata bila kujadiliwa ni asilimia zaidi ya mia, na nimejizuia kufanya hivyo kwa muda mrefu nikijua matokeo ndio yatakuwa hayo.
 
Nina Mke na mtoto mmoja, ndoa yenu inamiaka mitano sasa, katika swala la uaminifu katika ndoa sijawahi kumhisi mke wangu kutokuwa mwanaminifu, inawezekana ni kwa sababu nimeamua hivyo au inawezekana ni sahihi kabisa kwamba ni mwaminifu mpaka nilipokutana na kitu cha ajabu majuzi.

...hapo <bold> ndipo ninapopangojea kabla ya kutoa neno lolote!
 
Kwa nilivyosoma na kuelewa ni kwamba wewe na mkeo kama familia mmefanya what is called 'bad business' na hii hutokea kwa binadamu wote.
Umesema ni mfujaji hela ila sijaona sehemu yenye ushahidi wa hilo...kwa sababu labda alikosa muda wa kuindeleza nyumba.
Kingine ni kwa nini mmeuza vitu vingi hivyo kwa wakati mmoja...Pole mkuu kama una tatizo linalotibika kwa shida kiasi hicho.
Mi naona mkae chini mrudishe mapenzi, kuaminiana na kutegemeana kama mke na mume ili muanze tena kujenga vilivyobomoka. Ila sasa hivi mfanye pamoja. Haya mambo ya kila mtu kufanya kivyake ndo mtu anafanya 'Genuine mistake' kabisa ila mwenzie hamuamini.
 
nimesoma kwa makini nikagundua hapo kuna shida kama si ya mawasiliano basi huyo mkeo kuna sehemu anapeleka pesa,maana uwezi sema kabla ya kuoa ulikuwa na nyumba mwanza,na zingine mbili ukawa unajenga,sasa ulivyo oa tu uka mpa mdogo wako nyumba 1 akamalizia na wewe unapanga,sasa nachoo ona huyo mkeo anamatumzi makubwa sana ya pesa au nimuite mfujaji wa pesa na anahuruma na wewe,maana mnapanga na mna magari zaidi ya 3 hapo si kwako au kwake mkeo kunashida mahali,baba ni kichwa,sasa kama kichwa unakabidhi mshshara kwa mkeo na usha mjua mkeo ni mtu wa ku spend na kwako ipo shida tena kubwa
 
Pole sana, ila kwa mim sijaona sababu ya kufanya uachane na mkeo, au hii ya kutokubali kuuza gari lake? Please mkuu kaa jipange uongee na mkeo
 
Mkuu nimeisoma habari yako mwanzo mwisho lakini bado nashindwa kuelewa tatizo au kadhia i wapi...

Tatizo ni mkeo kushindwa kuuza gari lake kwa tatizo lako lile la kiafya ulilotuhabarisha hapa JF ama?

Kuna jambo nahisi hujatueleza na binafsi nina hisia chanzo cha hayo yote ni wewe kutosimama kama mwanaume kichwa cha familia.
 
Mkuu nimeisoma habari yako mwanzo mwisho lakini bado nadhindwa kuelewa tatizo au kadhia i wapi...

Tatizo ni mkeo kushindwa kuuza gari lake kwa tatizo lako lile la kiafya ulilotuhabarisha hapa JF ama?

Kuna jambo nahisi hujatueleza na binafsi nina hisia chanzo cha hayo yote ni wewe kutosimama kama mwanaume kichwa cha familia.

Tatizo la msingi, ambalo limeoccupy ubongo wangu kwa muda mrefu ni kwamba, toka nimekuwa naye maendeleo yamesimama kabisa, maendeleo niliyofanya nikiwa mwenyewe miaka miwili kabla ya kuwa naye sijatafikia hata kwa asilimia tano kwa miaka mitano niliyokuwa naye. hayo mengine ni bonus tu. Na majibu ambayo amekuwa akinipa juu ya kutokuonekana kwa mamilioni ya pesa ni majibu ambayo huwa yananitoa machozi, sometimes anasema "mi sijui we fanya unalotaka kufanya"

swala la kukataa kuuza gari wakati nikiwa katikati ya kifo na uzima, naambiwa na ndugu zangu ambao najua wako biased naye pia, kwa hiyo sio issue, sababu inawezekana lilikosa mteja kweli.
 
Anyway. Nimekuta anachat na wanaume wawili tofauti, akiwatumia na picha kuonyesha mwili wake.

Hili ndilo suala ulilopaswa kuliweka mezani maana ndipo kadhia ilipo, hayo maelezo mengine ni ziada tu.

Labda kwanza nikuulize, umeshakaa kitako na mkeo na kuliongelea hilo suala la yeye mkeo kupiga picha za utupu?

Kwa nini suala jepesi kama hilo unafikiria kulishitaki kwa wazazi?

Kwa nini jukumu la maamuzi usilichukue wewe mwenyewe kwa kuwa una ushahidi makinifu?
 
nimesoma kwa makini nikagundua hapo kuna shida kama si ya mawasiliano basi huyo mkeo kuna sehemu anapeleka pesa,maana uwezi sema kabla ya kuoa ulikuwa na nyumba mwanza,na zingine mbili ukawa unajenga,sasa ulivyo oa tu uka mpa mdogo wako nyumba 1 akamalizia na wewe unapanga,sasa nachoo ona huyo mkeo anamatumzi makubwa sana ya pesa au nimuite mfujaji wa pesa na anahuruma na wewe,maana mnapanga na mna magari zaidi ya 3 hapo si kwako au kwake mkeo kunashida mahali,baba ni kichwa,sasa kama kichwa unakabidhi mshshara kwa mkeo na usha mjua mkeo ni mtu wa ku spend na kwako ipo shida tena kubwa

Nakubali kosa langu, lakini pesa nilizokuwa nampa kwanza alinieleza anakusanya ili akianza kujenga ajenge amalize mara moja, kisha ghafla akaziweka kwenye biashara (by then nikiwa nje ya nchi kwa kama miezi miwili nimerudi na kukuta tayari yuko busy vibaya sana na biashara), sikuweza kumzua abruptly sababu tayari pesa zingine ziko mikononi mwa watu nakadharka.

Pili, siwezi kukaa na mwanamke nisiyemuamini, na hata napofikiria kumuacha, ni kwa sababu baada ya kuacha kumshirikisha kwenye mambo ya pesa, mahusiano yetu yamehabika sana, sio kwa upande wake tu, ila hata mimi, kwa nini nisiweze kumuamini mke wangu??
 
Hili ndilo suala ulilopaswa kuliweka mezani maana ndipo kadhia ilipo, hayo maelezo mengine ni ziada tu.

Labda kwanza nikuulize, umeshakaa kitako na mkeo na kuliongelea hilo suala la yeye mkeo kupiga picha za utupu?

Kwa nini suala jepesi kama hilo unafikiria kulishitaki kwa wazazi?

Kwa nini jukumu la maamuzi usilichukue wewe mwenyewe kwa kuwa una ushahidi makinifu?

Ndugu Yangu, hili ni la juzi tu, inawezekana ndio linanikumbusha haya yote japo hazikuwa picha za utupu kiivyo, kwa hili niliita ndugu zake tukalimaliza, na kwa kweli sio linaloniumiza sana, hili ni gumu kulifiatilia,
 
Mmeshawahi kuyajadili haya kama familia?
Kikubwa ambacho mimi nakiona hapo ni ukosefu wa mawasiliano na umoja kama familia,inaonekana kuna yanayomhusu mke tu ambayo mume hashiriki na yanayomhusu mume tu ambayo mke hashiriki hata kushauri ndio maana ulipomkabidhi nyumba amalizie akaamua pesa kuizungusha hukushiriki,na ndio maana unahisi alifanya hila gari yake isiuzwe!
Usilifikishe kwenye kikao cha familia kama unajua wataelemea upande gani,rudi ukae na mkeo muizungumzie hii hali kwa pamoja maana nyote mme play part kufika hapo mlipo sasa.
 
Biashara alianzisha nikiwa safarini, mawasiliano huvunjika pale anaposhindwa kutoa accounting ya pesa, nimeishamkaliza zaidi ya mara mia moja, mpaka nimempleka nje ya nchi kupumzika, na huko nikalianzisha, in a friendly and lovely manner, kwamba pesa zinatumika vipi, biashara fulani inaendeleaje, imekufakufaje, nikakuta baadhi ya partiners ni family members wake, kwa pesa alizokili watu wamekataa kumlipa ama kwa kutokuonekana au kwa kudai hawana nikamuomba anipe details zao za kutosha ili niwachukulie hatua za kisheria hata kwa ubabe sababu i have networks hakutoa ushirikiano mpaka leo.

Leo jioni naondoka moshi (nyumbani kwao), kakataa kwenda Mwanza kwamba atakuja baada ya mwaka mpya, bado hili sio tatizo sababu as long as atakuja na anabaki kwa wazazi wake natambua damu ni nzito, sio issue.

bado hapo ninatatizo la mawasiliano?
 
Mkuu nimeisoma habari yako mwanzo mwisho lakini bado nashindwa kuelewa tatizo au kadhia i wapi...

Tatizo ni mkeo kushindwa kuuza gari lake kwa tatizo lako lile la kiafya ulilotuhabarisha hapa JF ama?

Kuna jambo nahisi hujatueleza na binafsi nina hisia chanzo cha hayo yote ni wewe kutosimama kama mwanaume kichwa cha familia.

Nadhani ukichwa wa familia ni uwezo wa kutafuta pesa, huo uwezo ninao mkubwa sana na unaongezeka kila siku,
 
Back
Top Bottom