Naomba ushauri; inafaa kumpeleka mwanangu wa miaka 5 shule ya boarding?

misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
13,642
9,338
Habari wanajukwaa

Nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano(5yrs) kutokana na pilika pilika zangu za kibiashara kutotulia sehemu moja,je umri wake unafaa kumpeleka shule ya boarding?

Asanteni nasubiria ushauri wenu wakuu.
 
Kimsingi, mtoto anapaswa kupata malezi sahihi kutoka kwa wazazi wake, hasa anapokuwa na umri mdogo walau miaka 1-10. lkn mzazi anapokuwa na mambo mengi na hakuna mtu wa kukaa na mtoto nyumbani hii ni changamoto kubwa na inawakumba wengi. mabinti wa kazi nao nyakati hizi walio weng ni pasua kichwa. kama umeshindwa options zote peleka tu bweni ndugu kuliko uharibiwe mwanao na wapitaji, ni heri akae bweni lkn kuwa makini bweni wap? tafuta shule kwa umakini sana
 
Ok asante kwa ushauri wako mkuu
 
pole sna !kwani huna dada zako au ndugu wa kukaa naye!aise boarding ni majanga sana !bas tafuta shule za KISABATO huwa wana maadili mazuri ! JAMAN borading hata mtoto wa miaka 20 bado ni majanga
Wengi wapo mikoani na wengine wana familia zao kupeleka mtoto wangu kukaa nao naona kama nawapa majukumu ya lazima,shule ipi ya boarding ya kisabato nzuri mkuu?
 
Back
Top Bottom