Naomba ushauri: Goti la kushoto linauma baada ya kufanya zoezi

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
6,331
10,751
Habari,

Nimekuwa katika weight loss journey kwa muda kidogo... Mwaka 2018 nlikua na kilo 64 lakini Kuna Dawa nilitumia nikaongezka mpaka kilo 95.

Sasa nimejaribu kupungua nasaivi nakilo 79, mainly nlikua najog Kama KM 3 nakupunguza portion ya chakula

Mwezi mmoja uliopita wakati najog Goti Kama lilishtuka hivi. Hivyo nikawa napata Hali ya kuwa uncomfortable kwenye Hilo Goti...nikapumzika kujog.. ila juzi nimeanza Tena mazoezi ya YouTube nilipomaliza magoti yakawa yanauma japo maumivu sio makali Sana naweza kutembea na kufanya shughuli Ila naogopa Sasa kuendelea na mazoezi.

Je, shida itakuwa Nini Nini...naombeni ushauri wenu.

Miaka 27 Ke.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nashauri tembea tu kawaida litakuja kukaa sawa yaani hebu jaribu kutoka nyumbani hadi stendi kwa miguu kwa muda wa wiki ,nafikiri kwa sababu uzito wako umekuwa mkubwa kidogo ,ngoja nikupe kisa hiki mimi na rafiki yangu tulikimbia km 15 wakati wa kwenda tulipoanza kurudi nyumbani tumefika kilometa kama 9 hivi mimi goti langu likawa limistuka nikamwambia mwenzangu nipe nauli nipande gari,

akajibu wewe bado hujakomaa kwa umbali mrefu hivyo tembea taratibu tutakutana nyumbani ,basi mimi nilichechemea mdogomdogo mpaka nyumbani siku iliyofuata akashauri nenda uwanjani usikimbiae Bali tembea tu kawaida nilishangaa tu baada ya wiki moja goti lipo kwenye mstari,hivyo wakati mwingine ni kujilazimisha tu.,Natumaini utapona
 
Kilichotokea ni kuwa ulikimbia umbali mrefu km 3? Hapo bado hujageuza kurudi ulipotoka! Maana ulipiga km 6.

Lazima goti lipate hitilafu,

Mguu wa kushoto ni mzito kuliko wa kulia kwako ww ila kwa wengine ni kinyume chake,

Nakushauri anza kunyoosha viungo bila kukimbia,, baada ya wiki mbili anza kukimbi japo mita 200 mwisho km 1,

Alafu kesho yake upumzike kimbia tena kesho kutwa yake,

Kwa ujumla kimbia siku 4 pumzika siku 3 kwa wiki, baada ya miezi miwili leta mrejesho hapa




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halijavimba...Ila linakuwa uncomfortable nikikimbia...au Ni kikifanya aerobics mazoezi kwa kufuatilizia YouTube nikiwa nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kamavulivyoelekezwa hapo juu:

1: Kuwa na nidhamu kenye ulaji wa vyakula hasa vya wanga na vinywaji vyenye sukari.

2: Fanya mazoezi aerobic lakini yasiyoweka stress kubwa kwenye jointi zako za magoti maana kwa uzito ulionao unaweza kusaga viwambo/grinde layers zinazotengeneza jointi ie. tembea kwa mwendo mdogo na utakuwa unaongeza speed taratibu kadri mwili unavyopungua kidogo bila kukimbia na anza na umbali mfupi ukiwa unaongeza kidogo kadri mwili unavyoadjust.

3: Kunywa maji kwa wingi.

4: Kula zaidi matunda, mboga za majani, protein hasa ya mimea na nyama yeupe.
 
Kwa uzoefu wangu,ukikimbia kwenye lami kila siku kuna uwezekano mkubwa wa kuumwa magoti,
weka ratiba kwa wiki kimbia kwenye lami mara moja au mbili tu,siku nyingine kimbia kwenye mchanga au viweanjani...
 
Kuna kipindi hali kama hiyo ilinipata maana nilikuwa na kimbia sana(Jogging >7km per day) msuli wa goti ukawa napata maumivu.

Kila nikikaa kama week nikianza tu maumivu yanarudi.

Nilipumzika kama mwezi 1 nikarudi vyema kabisa.

Sijui kwako mkuu.
 
Na ulivo na msambwanda mtamu sipati picha ukiwa unajog walio nyuma yako wanakuwa na hali gani. Pona haraka uendelee na mazoezi am sure kuna watu wanamiss sana kampani yako
 
Back
Top Bottom