Naomba Ushauri: Biashara ya Chumvi - Kusaga, Kupakia na Kusambaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Ushauri: Biashara ya Chumvi - Kusaga, Kupakia na Kusambaza

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Maruku Vanilla, Jun 23, 2012.

 1. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Wana Jamii,

  Habarini ya mapumziko?

  Naomba msaada wenu kupata maelekezo juu ya Biashara ya Chumvi.

  Nataka kuwekeza kwenye usagaji na upakiaji wa chumvi ya baharini kwa matumizi ya binadamu na mifugo. Shughuli yangu itakuwa kununua chumvi toka kwa wamiliki wa mabirika ya chumvi halafu nitasaga, niweke Iodine na kupakia katika vifuko vya ujazo mbalimbali, kisha nitasambaza kwa wauzaji wa Jumla. Soko langu tarajiwa ni Kanda ya Ziwa

  Naomba msaada wa uzoefu toka kwa yeyote aliyewahi kufanya Biashara katika sekta hii. Na mambo ambayo sina ufahamu nayo ni pamoja na:

  • Nahitaji machine (mfano grinder) za aina gani, nitazipata wapi na vigezo gani nitumie kuzichagua?
  • Nahitaji leseni na vibali vya aina gani kufanya hii Biashara rasmi?
  • Mambo gani ni muhimu kuzingatia toka awali ili kuepuka hasara?

  Natanguliza shukrani kwa wale woote watakao nipa mwangaza.  Maruk Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd,
  P.O Box 1361, Bukoba
  Mob: 0717972957/0786972958
  E-mail: marukuvanilla@gmail.com
  [​IMG]
   
 2. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Biashara hii inapoteza tija, koz wengi siku hizi wanatumia mbadala wa chumvi kama limao nk kutokana na ongezeko la ugonjwa wa BP
   
 3. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Aren't you going the other way round na maswali yako especially hilo la tatu kabla ya kuuliza hasara utakayo ipata wewe kwanza ulitakiwa binafsi uwe umeshafanya risk assessment ya hilo soko kabla ujaingia kichwa kichwa kupoteza hela zako au kujipatia faida zako hiyo ndio ingekuwa sababu yako kuu ya kufanya hiyo biashara au la.

  Maana hayo maswali yamekaa kama mtu aliyeona tu chumvi akapata idea ya biashara, bila ya kujua kama soko lipo ama la, ya chumvi ya kusaga. Ungekuwa umefanya kazi yako tayari ungejua ni wapi target zako zipo kwa sana, kama kwa wanyama au binadamu na bei za soko zikoje na gharama zako za uzalishaji zipoje hapo kaka ndio unajua kama unafiada au hasara. Inaonekana auna hata business plan kutokana na maswali yako.
   
 4. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Elewa vema ombi langu

  Pamoja na ukarimu wako kuchangia hapa, yawezekana hukuwa mlengwa. Maana mlengwa angetoa uzoefu na ushauri wa kisekta zaidi ambao hata academician angetambua kuwa hiyo ni sehemu ya vyanzo vya kufanya assessment na kisha kuchukua maamuzi. Nani akiisha chagua mchumba ndo anaenda kuomba ushauri kama mchumba anafaa au hafai?


  Asante kwa mtazamo na ushauri. Nami nitakushauri kuwa uzoefu niliojifunza kwenye uwanja wa biashara, ni kwamba mtu aliye too academic hawezi biashara. Akijaribu ataishia kuandika huo mpango wa biashara na kila akifika kwenye mizania ya mahesabu anaona hasara tu au faida kiduchu. Na hatma yake ni kuja na hitimisho "hakuna bishara inayolipa"
  Kwa ushauri wako hii article itakufaa http://blogs.hbr.org/tjan/2012/05/great-businesses-dont-start-wi.html
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu hii biashara sijawahi kuifanya lakini nafaamu mwambao wa bahari wa bagamoyo ukivuka mitaa ya majani mapana kuna wenyeji wanatengeneza chumvi ya bahari kwa njia za asili.. best way kwako ni kufanya nao mazungumzo ili ufahamu undani wa gharama from ground level, baada ya hapo utaweza kufahamu ile raw salt ipo ktk kiwango gani, inahitaji nini cha ziada kuwa chumvi kamili na hivyo itakuwezesha kufahamu na kuplan aina ya processing machine itakayohitajika.

  Chumvi pendwa asili huwa ina bei nzuri sokoni kuliko za wiwandani kwahiyo na wewe ni lazima ushirikishe mbinu asili kwa kuwatumia wenyeji ili uweze kumantain % kubwa ya uasili na mahitaji makubwa ya soko.

  Mkuu product dispaly yako imenivutia sana na zaidi ni hili zao la vannila wish tutajifunza kupitia kwako
   
 6. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mkuu Narubongo

  Nakushukuru sana kwa mchango wako muluha. Nilifahamu fika kuwa ukija hapa utanipa mawili, matatu ya kuniongoza kwenda mbele. Ndo sababu ya kukaribisha kwa tag.

  Sijafanya mazungumzo na watu wa B'moyo bali niko katika majadiliano na wamiliki wa Mabirika ya chumvi pale Kilwa-Pwani. Na kila kitu kimeenda sawa katika hatua za awali. Nawategemea wao waniuzie chumvi ikiwa bado haijasagwa halafu mie nitasaga, nitapaki na kusambaza. Hivyo hitaji langu kubwa zaidi liko katika kujua aina za machine za kusaga na mambo mengine katika mlolongo wa biashara hii.

  Asante kwa kusifia display yangu na unakaribishwa kujiunga katika ukilima na usindikaji wa viungo vya vanilla.

   
 7. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kaka hiyo ni venture yako na wewe umekuja hapa kuomba ushauri ndio umeweka specifics za watu ambao ungeomba wachangie. Lakini kuna walakini kwenye msaada ulioutaka sasa kama kuna mtu hajui biashara zinaanzishwa vipi (kuna mambo mengi ya msingi umwemwachia). Mfano unaposema mashine, leseni na kuokoa hasara tayari kuna financial risks hapo. Huyo jamaa anaekwambia huhitaji business plan tayari anakuongopea.

  Wewe unaweza vipi jua hasara zako au faida zako kama una hata projection za quantity utazo zalisha, gharama zako za biashara na faida zako, maana source ya income inatoka wapi kama ni hela yako si tatizo na kama kuna loan then lazima ujue where your heading, especially when debt is called. Sasa kweli unaweza vipi kumuuliza mtu mambo gani ya kuzingatia hasara wakati mtu ajui hiyo bidhaa hipo aimed kwa nani na sokoni inategemewa kuuzwa kiasi gani na ushindani ukoje.

  Halafu unasema huitaji business plan, maana huto mshauri mzushi anasema hata huyo jamaa aliekuwa anataka kuuza sabuni alishalenga for 0.5% of chinese market na alikuwa anajuwa ukubwa wa soko lake na targeted consumers before that. Sasa sisi tutajuaje una aim wapi na gharama za bidhaa zako zikifika dukani ili watu wakushauri kama kwa bei hiyo utaumia unless uzalishe kiasi gani na mambo mengine meeengi katikati. Si ajabu hata huyo Mengi anashindwa kulipa madeni yake kwa kuvamia tu vitu.
   
 8. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Zinjathropus,
  Asante kwa maoni yako mazuri.
  Naendelea kusoma na kusubiri ya wengine huku nikilinda dhima kuu ya uzi huu isiamishwe.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
 10. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Asante sana Mkuu.

  Nikufahamishe tu kuwa niko Alibaba na katika e-commerce sites nyinine kitamba kidogo. Tatizo katika technology sourcing ni jinsi ya ku- specify kwa usahihi machine au technology inayokufaa na ambayo si obsolete na wala haitakuwa na idle capacity kubwa au low capacity. Hapa lazima uhitaji ushauri wa mtu aliyebobea katika nyanja husika. Ni bahati mbaya sana katika Tanzania, Wajasiriamali tusio na elimu ndo tunazifundisha Taasisi kama SIDO, TIRDO, TATEMDO, CoET (Chemical Processing Eng) katika nyanja ya Teknolojia kujua ipi inastahili na kufaa katika mazingira yetu badala ya wao ndo watuongoze na kutufundisha sisi.


   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Inasemkekan gharama kubwa ni kupata Madini joto IODINE amabayo unabidi uagize nje!
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Maruku Vanilla, Wazo zuri katika kujitafutia kipato na hali tuliyonayo inapotokea mtu anakuja na wazo kama hili ni vema tukamuunga mkono.Ningependa kukushauri kwenye yafuatayo:

  • Kuna delegation ya wa taiwan watakuwa Serena Hotel Leo kuna makampuni mengi yanayojihusisha na Mashine za kuprocess na packaging.Ukienda kwenye huo mkutano(B2B) unaweza pata vitu vizuri vitakavyo fanikisha wazo lako. Lakini pia kuna delegation kubwa sana ya wachina watakuwepo saba saba na katika group hiyo kuna watu wa Machines ambazo zinaweza kukufaa so please take you time tembelea saba saba kuanzia tarehe 1st June......
  • Kuhusu Vibali na Leseni unatakiwa kuwaona Brela,TBS,TFDA Pamoja na leseni ya uchimbaji wa hiyo wizara ya madini
  • Mambo gani ni muhimu kuzingatia: Jua Test ya soko kwanza kabla ujaanza kuzalisha ni vizuri kwanza ukafanya simple survey or Needs Asssement ilikuwajua nini hasa soko linataka angali chumvi zilizoko sokoni nini limepungua(Gap) then wewe product utakayoleta lazima iwe inatoa solution. lazima uwe na unique selling point ambayo ndiyo itakuwa inaitofautisha bidhaa yako na washindani.
  Kwasasa ngoja niishie hapo.

   
 13. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ninakushukuru sana Ndugu KOMBAJR


   
 14. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Kuna machine nimetumiwa picha zake na Wachina. Kwa faida ya Wajasiriamali wenzangu naziweka hapa:

  back of 30-B.JPG DSCF0935.JPG DSCF6360.JPG SALT.jpg DSCF6356.JPG
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Maruku Vanilla,
  kupata machine si tatizo kwa ulimwengu wa sasa, tatizo linakuja kwenye kuamua machine ipi ya kununua, Vigezo vya kuchagua machine nzuri ni hapo chini

  - machine yenye uwezo wa kutumia different sources of energy eg electrical power & kerosene & diesel & mechanical power. Hii kitu ni muhimu c'se umeme wa tz hautabiriki.. haipendezi ku_stop/ delay production kipindi cha mgao au hitilafu za umeme, ukiwa na machine ya namna hii utakuwa na uhakika wa kufanya kazi wakati wote. Pia itakusaidia kufanya kazi kipindi ambacho umeme hauna nguvu ya ku run machine [capable to move from one energy source to another]

  - power consumption, machine nzuri ni ile inayotumia nguvu ndogo ya umeme, machine ya namna hii itakusaidia kupunguza gharama za uendeshaji. Ukishafahamu machine inatumia nguvu kiasi gani ndio utaweza kujua gharama za uzalishaji na uendeshaji na mwisho utaweza kujua faida/hasara utakayoipata. [eg machine A --4600kwh, machine B ---4750kwh ukiaudit hizi machine 2 kwa mwaka utakuta "B" imepoteza kiasi kikubwa sana cha faida even though energy difference was only 150kwh]

  - efficiency nayo ni kitu muhimu, i.e unasaga kg ngapi kwa saa, granules rate etc

  - machine nzuri ile yenye yenye blocks 2/3 na isiyo na internal components nyingi(electrical components, connectors etc) c'se unapokuwa na components nyingi ndio unavyoongeza defect chances... & due to electrical instability of tz.. utakuwa unaunguza internal parts kila siku --> need to buy more spare parts & hence rise in maintenance costs. [too manual machine is better than auto ones].

  - upatikanaji wa spare parts, ukizingatia hapo juu halitakuwa tatizo kwako, usinunue complex machines itakuumiza kwa mazingira ya tz. Products za china si za kuamini sana, nakumbuka SIDO walikuwa na machine za namna hii zisizo na makolombwezo mengi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. MIAMIA.

  MIAMIA. JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ...it shows continuity!!!

  what naeza kunena kwa sasa,1stly sory for being late kuchangia hii kitu but nitakapo pata rasmi muda nitachangia kwa kina though sina kabisaaaaaa uzoefu katika biashara ya chumvi lakini nachoweza sema you did the right choice at right people ambao kwa jicho ama fikra ya biashara mimi siwaiti people nawaita potential buyers...
  go on...ata akitokea nani leo akakwambia he/she will pay you ones you stop or quit doing it coz u got potential sana...
  ningefunguka but muda kidogo i promise will be be back nikikumuka kwa thread hii,u may PM me...
  thanks...GO GO GO GO GO GO........................
   
 17. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2017
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 8,613
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  Any Feedback ??
   
 18. a

  antimatter JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2017
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 448
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Chumvi nyingi zinatoka mombasa. Labda anauza kanda ya ziwa
   
Loading...