dumbi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2018
- 989
- 1,523
Habari zenu wakuu?
Nina dada yangu alizaa watoto wawili na mwanaume wa nchi fulani ya jirani hapa Africa na walifunga ndoa halali. Lakini badae wakaja kutengana na watoto akabaki nao mama yao, jamaa anahudumia kila kitu aliwajengea nyumba na shule wanasoma hizi za english medium.
Tatizo lilipo na kuwaomba ushauri ni kwamba huyu dada hana muda wa kuangalia hawa watoto, yeye akitoka asubuh kurudi usiku hajui watoto wameshindaje hapo nyumbani, hii imepelekea watoto kutokuwa na maendeleo mazuri shuleni mfano huyu mkubwa alitakiwa awe form 2 lakin yupo la sita amerudishwarudishwa.
Juzi juzi nilikuwa nao yule mkubwa akaniambia mjomba mimi nataka nikae na wewe sitaki kurud kwa mama muda mwingi tunakaa na njaa mpaka mama arudi usiku ndio tunakula na mengine mengi ameniambia.
Kibaya zaidi huyu mdogo amekuwa ana tabia za kike kike juzi kati nilipata kesi kwamba watoto wenzie wanamwingilia, mama yake alivyosikia hivyo alimpiga na marungu mpaka akawa hawezi kutembea na hii sio mara ya kwanza kumpiga manake ni mtundu sana mama anajua kupiga tu.
Mimi nilienda nikaongea nae mtoto kweli akakubali lakin anadai ni mara 2 tu. Huyu dada tumemshauri watoto waje waishi kwangu lakin yeye hataki, tena anatukana matusi mengi sana ukimgusia swala la watoto wakati anaona wanamshinda.
Baba yao ndio aliniomba zamani sana nikae na watoto lakini kwasabu dada ni mtata nilikataa sasa nimeamua niwachukue tatizo mama yao hataki je nifanyeje ili niweze kuchukua hawa watoto?