kitoto wa vitoto
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 360
- 386
Nawasalimu kwa pamoja ndugu zangu,
Mimi nimejiunga huku kwa nia ya kujifunza, kwa namna ya kipekee sana mmenipokea na kunionyesha ushirikiano hasa pale nilipohitaji msaada wa mawazo. Asanteni sana kwa hilo.
Pili, nilisema awali ndoto yangu ni kilimo japo wachache walinidhihaki ila azma yangu ipo palepale. Kwa jasho na kujinyima nimefanikiwa kupata shamba Hekari 15 maeneo ya Chalinze barabara ya Kwa Mwarabu.
Nilinunua kupitia utaratibu ambao ni muongozo nilioupata hapa JF. Ombi langu tena, naomba mnielekeze, naweza kulima zao gani maeneo hayo?
WAZO LANGU
- Kulima maharage ya soya
- Kulima mahindi
- Kulima nanasi, au zao lingine mtakalolipendekeza.
Ukweli nina nia na hili suala. Natanguliza shukrani. Ni mategemeo yangu mtanishauri vema.