Naomba uniruhusu kusema hili neno''baadhi ya wanasiasa ni wapumbavu''tazama kenya


NEW NOEL

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Messages
853
Likes
136
Points
60
NEW NOEL

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined May 21, 2011
853 136 60
Leo hii mbunge wa Kenya ambaye amechaguliwa kipindi ambacho hata akizidi miezi 4,tayari anataka kuongezwa mshahara kwa kisingizio cha kufanya kazi sana.
Kenya ni nchi maskini na hao wabunge pasipo na shaka waliomba ridhaa kwa wananchi wao ili kuwaongoza katika kupunguza umaskini wao. Lakini leo mbunge huyo akiwa hajafikisha hata mwaka mmoja anadai kazi ni ngumu na anahitaji malipo zaidi.
Leo anataka kulipwa kiasi cha shilingi za tanzania zaidi ya Milioni 16 ambazo ni sawa na shilingi za kenya zaidi ya laki nane. Na hii iwe ni funzo kwa Watanzania kamwe tusikubali ujinga kama huu.
Yaani Kenya ni miongoni mwa nchi duniani ambazo Wabunge wake wanalipwa pesa nyingi kuliko nchi nyingine.
Usishangae mimi kuzungumzia Kenya ilihali ni Mtanzania,kumbuka ule msemo unaosema ''mwenzio akinyolewa na wewe tia maji''.
Nimeipenda na kauli ya Rais Kenyatta ya kuwataka kufanya kazi kwanza na mengine yatafuata. Kwani unafikiri ingekuwa Kenya wanasiasa wetu wanafanya kazi basi hata wangejiongezea mishahara isingekuwa shida.
Tazama hiyo chart hapo chiniJe sisi Tanzania?

Samahani katika heading nimetumia neno baadhi,kwasababu sio wanasiasa wote.Natambua kuna wanasiasa wanaofanya kazi na hata matokeo ya kazi yao yanaonekana.
 

Forum statistics

Threads 1,273,260
Members 490,343
Posts 30,475,692