Naomba ufafanuzi wa taratibu za kufuata endapo mwanafunzi ambaye ni mnufaika wa mkopo na ambae ameshasajiliwa chuo kingine kama anaweza kuomba upya

Dnmunisi

Member
Nov 11, 2020
17
45
Habari za wakati huu, ni matumaini yangu kuwa mnaendekea vizuri na shughili za kujenga taifa..hongereni sana
Kuna mdogo wangu yupo chuo kikuu mwaka wa kwanza chuo kikuu cha dodoma (udom) anasomea environmental science kufikia hapo alipo anasema anachokisomea hakipendi na kwamba alikubali tuu kwenda kusoma hiyo kozi ili tuu asibaki mtaani...anataka aache chuo ili aanze tena upya kuapply mwaka huu. Ninaombeni ushauri wenu ndugu zangu juu ya taratibu za kufata na pia ni mnufaika wa mkopo.

1. Je, afate taratibu gani ili aweze tena kuapply chuo upya.

2. Kwa mfano asipopata anachotaka kukisomea ataweza tena kurudi kuendelea na kozi ile ile aliyokua anaisomea?

3. Kuna uwezekano wa kuweza kupata mkopo kwa mara nyingine?

Nitangulize shukrani zangu za dhati kwa wote watakaotoa maoni yao asanteni sana na Mungu awabariki
 
Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
520
1,000
Akidrop out na bodi wanamdrop out vilevile, ila akisitisha mwaka na bodi wanasitisha vilevile, akiresume masomo na bodi wanaresume mkopo vilevile ingawa kwa taabu sana. Sasa cha kufanya hapo afate taratibu zote za kusitisha masomo mwaka huu na aombe kubadilishiwa course kwa mwaka wa masomo ujao. Hivyo akirudi chuoni kwa mwaka wa masomo husika atafata utaratibu uliowekwa ili aendelee kula mkopo wake, cha kuzingatia hatapata sehemu ya mkopo ambao alishapewa hapo awali. Environmental science ni hesabu kwelikweli
 
Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
520
1,000
Na Jambo lingine la muhimu sana ni kwamba huko chuoni Kuna academic advisor kwa kila mwanachuo. Hivyo ni vyema ukamshauri huyo ndugu yako amuone huyo mtu ili apate ushauri mzuri zaidi.
 
Immanuel Simon Mathew

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
353
1,000
Envaromental science ni kipengele, inahitaji kujitoa sadaka kwelikweli. But on that case la kufanya ni kupostpone mwaka na kwa technical assistance zaidi Ni vyema akawasiliana na mshauri wa wanafunzi wa chuo (Dean of students) akampa namna bora ya kutatua changamoto hiyo.
 
Dnmunisi

Member
Nov 11, 2020
17
45
Na Jambo lingine la muhimu sana ni kwamba huko chuoni Kuna academic advisor kwa kila mwanachuo. Hivyo ni vyema ukamshauri huyo ndugu yako amuone huyo mtu ili apate ushauri mzuri zaidi.
Asante sana kwa ushauri wako ndugu yangu
 
Dnmunisi

Member
Nov 11, 2020
17
45
Envaromental science ni kipengele, inahitaji kujitoa sadaka kwelikweli. But on that case la kufanya ni kupostpone mwaka na kwa technical assistance zaidi Ni vyema akawasiliana na mshauri wa wanafunzi wa chuo (Dean of students) akampa namna bora ya kutatua changamoto hiyo.
Ndio kitu hasa anachotaka kufanya
 
Ezekiel Mbaga

Verified Member
May 28, 2018
7,521
2,000
Hiyo namba 2 nadhani hamko serious na elimu nyie.

Mm navojua, ili apate tena mkopo itabidi alipe 25% ya mkopo aliochukua ili apate mkopo mpya (hi ni incase ya wale waliomaliza degree ila wanataka kupata degree nyingine, ila kuhusu hiyo ishu yenu bc cjajua itakuaje)
 
Ezekiel Mbaga

Verified Member
May 28, 2018
7,521
2,000
Envaromental science ni kipengele, inahitaji kujitoa sadaka kwelikweli. But on that case la kufanya ni kupostpone mwaka na kwa technical assistance zaidi Ni vyema akawasiliana na mshauri wa wanafunzi wa chuo (Dean of students) akampa namna bora ya kutatua changamoto hiyo.
Jamaa anasema mhusika yupo UDOM, halafu UDOM sa hv hakuna Dean
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom